Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Magufuli alikuwa na matatizo tangu akiwa naibu waziri wizara ya ujenzi, wakati Balozi Mshangama akiwa Katibu Mkuu pale. Magufuli alijaribu kutumia "ujanja" kujipatia malipo ya kusafirisha mizigo yake wakati alipoteuliwa na Mkapa mara ya kwanza.

Ninawauliza wanamtandao, hizi vurugu za Magufuli ktk zoezi hili unaweza kuzilinganisha na vurugu za Sumaye kujipatia shamba la eka 7 kule kibaigwa?

Kwa upande mmoja nina furaha kwamba ukweli kuhusu Magufuli unajitokeza. Upande mwingine nasikitika kwasababu hizi ni kampeni zinazoendeshwa na watu wachafu--WANAMTANDAO.
 
Mzee ES,
Aminia babake! Naamini kweli wewe ni system ndani ya system, hizi news nakumbuka ulizitoa kipindi kile BCStimes, kwamba wameshaingia kazi inayokuja ni kumpiga kikumbo heavy huyu mbilikimo Magufuli. Nayaona kwa macho yangu sasa.
 
Cha kujiuliza ni kwa nini Gazeti la Rai linalomilikiwa na Rostam Azizi limemuandama Magufuli? Ni wazi huyu ni mawe katika mchele na itabidi apembuliwe hivi karibuni. Lakini kwa kupenda madaraka atasubiri hadi aumbuliwe!
 
Magufuri hatofautiani na Mrema, nje ya sura ni ushujaa huku ndani ni mla rushwa,
hata Bodi yenyewe ilikuwa na Udini naona wakristu watupu, tutafika?
watu wengi wanatumia kigezo cha kuwatetea wanyonge kinadharia, huku practically hawana huo moyo.
 
Ziwe mbinu za mtandao zisiwe, mimi nataka kujua haya maneno kweli?... Hilo tu kwani Magufuri kasifiwa sana huko nyuma kabla ya uchaguzi.
Mimi nasema Nyerere katuachia urithi mkubwa sana jamani leo hii kila kiongozi tajiri na mali kibao wanagombea utafikiri usafiri wa Daladala!..hata siku moja hakuna siku mtu mwenye nauli yake alikosa usafiri!..
Kuna rafiki yangu mtu wa Trinidad alikuwa huko hivi majuzi mwenyewe kachoka na Bongo...kabaki hoi!.. hajawahi kuona nchi maskini duniani wakichezea fedha kama Bongo!...
 
Mzee Bob,

Katika kikao chake cha mwisho na watanzania wa NY pale Hotel Inter, Mkapa aliulizwa swali na mtoto wa JM, kuhusu hii issue ya nyumba za serikali kuuuzwa kiholelal na faida yake kwa serikali,

Mkapa alimjibu tena kwa jazba, kwamba quote,

"........mimi Mkapa kama rais wa nchi nimeamua kuziuza nyumba hizo kwa sababu ya kuwasaidia wananchi wasiojiweza na baadhi ya viongozi wetu, sina mengi zaidi ya kusema na tena nimesikia kuwa rais anayejitayarisha kuingia ana mpango wa kuzirudisha nyumba hizo.....ninamtakia mafanikio mema au good luck........"

Sasa huoni hili swala kuwa ni la Mkapa, na Magufuli alikuwa anatekeleza amri?
 
Jamani habari kuhusu Mgufuli zimenistua kweli! Kumbe unaweza kumpenda mwanasiasa kumbe unajidanganya! Huyu jamaa hata kujibu tuhuma naona hataki! au kesha jibu jamani? JK naye sijui anafikiria nini. Magufuli kumbe ni pombe hivi!
Huyu dogo amekwisha kisiasa kaka kaka Sumaye!
 
Magufuli,

Kwa maoni yangu anayo matatizo, tena serious ones, lakini sio kwenye kuuza nyumba isipokuwa kwenye pesa za kutengeneza mabara bara, yeye na Keenja, walienda shue moja ya uongozi wakajifunza kuwa wabongo dawa yao ni kujenga kitu wakione,

halafu tumia hela zozote unazotaka hawatauliza zimetukaje, so far hawa waandishi hawajazigusa data zake vizuri, ila kuna siku watazikuta!
 
Asante Albinus Mboweto kutufumbua macho kuhusu Magufuri. Lakini bado nina maswali luluki kuhusu magufuri na Uuzaji wa nyumba za serikali. Kadri NIjuavyo suala la uuzaji wa nyumba ulikubaliwa na baraza la mawazili la awamu ya Tatu, kuthibitisha hilo hakuna hata waziri mmoja aliyepinga hazarani akiwapo raisi wa awamu ya nne. Sasa leo inakuaje lawama abebeshwe magufuri peke yake?Huu ni unafiki. Pili gazeti hili la RAI likikuwa linatumiwa kumtangaza vibaya SUMAYE na ulaji wake wa rushwa mpaka hakaonekana hafai kwa jamii .Nakubali Sumaye alikuwa sio kiongozi safi, lakini RAI ilizidi kumchafua kwa interest za kumbeba Kikwete.Viongozi wa awamu ya tatu wengi tu walikuwa wanaharibu kazi lakini RAI waliamua kusimama na Sumaye tu mpaka jamii ikaamini ni kiongozi mbaya kuliko kiongozi yoyote Tanzania, sasa wanambomoa magufuri. Tusisahau RAI sasa linamilikiwa na mwanamtandao wa kutupwa Rostam Hazizi lakini magufuri sio mwanamtandao na wanataka kumchafua kwa interest binafsi ili wananchi waone Tanzania hakuna Viongozi safi zaidi ya Kikwete na Lowasa. NaombaTuwe makini na Tanzania Press, vinginevyo wananchi tutayumbishwa sana.Hawa jamaa (RAI)wanatoa habari kwa Interest binafsi na sio kusaidia jamii.
 
suala la magufuri ni kiini macho kila mtu anajua jk hakumtaka,jk watu wake alishawaandaa kabla ya kuwa rais mf..tangu wakati wa kampeni tulisikia fununu mkurugenzi wa idara angekua RO ambaye hata kabla hajaenda uk walikua washkaji na wakibadilishana mademu,,IGP shemeji kila mtu alijua na ikawa...na mjue wana mtandao wanaakili sasa hivi urais na chama wameupata wenzenu wanaangalia 2015,,kwa hiyo watu wote ambao hawawataki wanandaliwa political suicides kwa kutumia mhimili wa habari waliouteka hatukata magufuli si malaika lakini hamshangai kweli rai tunalolijua lina tabia hiii? tulizoea rai zamani likichokoza mada na kuendelea na nyingine lakini sasa inaonekana limefanya u turn kiuandishi naona linatumiwa..masikini magufuli ,,tishio lingine la urais 2015 ni mwandosya naona baada ya magufuli iatakua yeye,sumaye pamoja na kuwa ziro alisema "mtu anayeingia madarakani kwa kupaka wenzake matope kwa kalamu ,atatumia bunduki kusalia madarakani.."tungoje tuone,yetu macho!!!
 
*Ataka wanaomzulia mumewe kuachana naye
*Asema kama ni kimada, yeye ndiye wa kuumia
*Yabainika mdogo wake Mussa aliuziwa kontena
*Tuhuma zahusishwa na urais baada ya Kikwete
*Asema wanaomfatilia 'Washindwe kwa jina la Yesu'

Follow this issue on: JamboTanzania.net
 
SECTION: BUSINESS INTELLIGENCE

LENGTH: 222 words

HEADLINE: Trouble ahead for Magufuli

BODY:


The current Tanzanian Minister for Land and Housing, John Magufuli, stands in risk of being involved in an affair concerning his brother Musa Joseph Magufuli. Last year the latter acquired a house from the State housing pool, as civil servants then were allowed to do.

It was sold to him by the Tanzania Building Agency (TBA) which reports to the ministry of infrastructure (then the ministry of public works), then headed by his minister brother. The trouble is that Musa Joseph Magufuli did not have the right to buy this house, because he was only employed by the ministry headed by his brother on a short term contract (90 days). From 26 September to 31 December 2005 he was a management officer in the TBA, a post which had not been advertised and which he left two days before his contract was due to expire. But not before buying from the State a governmental house located in the Ubundo Camp neighbourhood in Dar es-Salaam. The papers transfering ownership of the house to him had been ready since 27 October 2005. Better still, during the time he was employed at the TBA, Musa Joseph Magufuli did not do any real work because he was at the same time a full time student at Dar es-Salaam University, reading for an MA in sociology. In fact, he even gave the university post box as his address for the property transaction.

URL: www.IndianOceanNewsletter.com

LOAD-DATE: October 27, 2006
 
Hi ni kweli..?
Mi nilifikiri moja ya- wachapa kazi..wa serikari iliyopo madalakani ni Mgufuli...
Sasa Itabidi ahamishiwe Vizara gani? au aende east Africa..
 
Gigo, kwa hili usiwena wasiwasi ataundiwa wizara mpya na kupewa manaibu waziri watatu wa kumsaidia kazi.
 
wanamuonea hiyo ni strategy ya wanamtandao katika kujipanga kwa 2015.leo kwenye mtazania daima wametoa picha ya hivo vikontena wanavyoita njumba ni mkichekesho ,amenunua KWENTENA ya 40ft ambayo nafikiri ilikuwa ikitumika kama store kwenye kambi walipokua wanajenga barabara ya mandela miaka hiyo,liko pale ubungo..
pia wanaweza wakawa wanamtumia magufuli awe habari kama strategy ya kupooza malalamiko ya umeme[substution]
let us not be taken for a ride ,.what is merely containers in comparison to richmond and falling shillling [econommy]
 
wanamtandao hata humu wamo wanampiga vita sana!

Lakini ya kwao hayasemwi!!

Tunaelekea wapi? Mnadhani wote ni wajinga humu?kuwa mnaweza kutudanganya kama watoto?.

Nyumba zirudishwe zote hizo za ndugu zake na zenu mlizonunua au walizonunua ndugu zenu.
 
The point here ni kama amefanya au la, hii wanamtandao wanamuonea au la ni side issue tufanye tathmini ya kama kafanya anayodaiwa kufanya au la.

Na vile vile jingine la msingi ni kama ni kweli basi hatua gani zichukuliwe, kama ni uongo kuna vyombo vya sheria vinahusika na mambo ya libel anaweza kupata haki yake huko.

Habari nyeti kama hii bila shaka ina mtu wa ndani anaeitoa lakini chanzo sio muhimu kama the truth in these matters...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom