Monalisa Ndala: Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ajiuzulu mara moja

Chiston junior

New Member
May 7, 2021
4
28
GERSON MSIGWA AJIUZULU

Ndugu zangu waandishi wa habari, kwanza nawashukuru kwa kuitikia wito wangu na kufika hapa leo. Nimewaita kwa jambo moja tu ambalo niliona haitakuwa sawasawa likiachwa na kupita hivi hivi.

Kabla sijalitaja jambo hilo naomba niseme mapema kuwa ninazungumza katika mkutano huu wa waandishi nikiwa kama Mwanachama wa ACT Wazalendo mwenye uchungu na wivu mkubwa wa chama changu. Kwa hiyo mtu yeyote anayethubutu kukichafua au kukidhalilisha Chama au viongozi wangu wa Chama, mimi Monalisa nina haki na wajibu wote wa kushughulika naye mtu huyo. Kwa hiyo nimejitokeza kuhami heshima na taswira ya Chama na Viongozi wangu wa Chama dhidi ya udhalilishaji uliofanywa na mtu mmoja ambaye nitamtaja hapa hapa.

Ndugu waandishi, Juzi, Jumamosi ya tarehe 18 mwezi huu wa Septemba, Msemaji wa Serikali ndugu Gerson Msigwa alisikika kwenye Kipindi cha mahojiano kinachojulikana kama Medani za Siasa katika televisheni ya StarTV, kinachoongozwa na mtangazaji ndugu Edwin Odemba akiendeleza vitendo viovu vya kuwadhalilisha vibaya sana Kiongozi wa Chama changu Ndg. Zitto Kabwe na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama changu marehemu Maalim Seif Sharif Hamad (Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi).

Katika kipindi hicho Msemaji wa Serikali ndugu Msigwa alibanwa kwa maswali yenye mantiki ya kupima utendaji haki wa vyombo vya serikali ikiwemo ofisi anayoiongoza Msemaji huyo, ofisi ya Habari Maelezo, kwamba wamekuwa wakifanya upendeleo wa wazi wazi kwa sababu wanazozijua wao!

Msemaji wa Serikali aliulizwa, inakuwaje Gazeti la Raia Mwema linaloandika habari zake kwa kuzingatia misingi ya ukweli na weledi linachukuliwa hatua kwa kufungiwa lakini gazeti la Tanzanite linaloonekana dhahiri lilianzishwa kimkakati kwa ajili tu ya kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi wa upinzani na wakosoaji wa serikali linaachwa linadhalilisha watu ovyo na linavunja sheria na miiko ya uandishi wa habari waziwazi katika matoleo yake??

Mtangazaji alimuhoji Msemaji wa Serikali, kwamba Raia Mwema limefungiwa kwa kile Msemaji wa Serikali anachodai gazeti kushindwa kuthibitisha kuwa aliyedaiwa kuwa ni gaidi, bwana Hamza ni mwanachama wa CCM. Ni kutokana na hilo, mtangazaji akahoji, kama gazeti limefungiwa kwa sababu limeandika habari likimnasibisha bwana Hamza na uCCM ambao kila mmoja ameuona wazi dhahiri shahiri, ambapo enzi za uhai wake Hamza alionekana akiwa kwenye sare za CCM, akishiriki shughuli za Chama hicho kwenye kampeni za uchaguzi mkuu 2020 akimnadi mgombea urais wa CCM John Pombe Magufuli, akijitolea kujenga ofisi za CCM huko Chunya, akishiriki shughuli na michango mbalimbali ya hali na mali kwa chama chake cha CCM na wanaCCM wenzake kama kada mwaminifu wa Chama, dunia nzima imeona na inajua hivyo, Msigwa anawezaje kukana kuwa Hamza hakuwa mwanaccm?? Anamkana kwa kuwa tu Hamza amekumbwa na mkasa ambao umeacha sintofahamu na maswali mengi kwenye jamii?!! Hilo ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana. Kabla Hamza hajakumbwa na mkasa ule, alikuwa mwanaCCM, amekumbwa na mkasa, watu wanamkana! Hiyo siyo sawasawa na wala siyo haki kwa Hamza. Lakini hiyo siyo ajenda yangu hasa ya leo.

Msigwa aliulizwa, inakuwaje gazeti la Raia Mwema amelishughulikia mara moja kwa kumhusisha Hamza na CCM jambo ambalo liko wazi kila mtu anaona na anajua kama nilivyoeleza, lakini gazeti la Tanzanite lililoandika uongo na uzushi dhidi ya viongozi wa ACT Wazalendo kuwa wanagombea kijana mmoja ambaye gazeti lilisema ni shoga! Kwamba viongozi wa chama changu wanashiriki vitendo vichafu vya mapenzi ya jinsia moja! Hicho kilikuwa kiwango cha kupindukia cha ukiukaji wa maadili ya uandishi wa habari. Kilikuwa kiwango cha kupindukia cha udhalilishaji wa chama changu na viongozi wangu. Ajabu hiyo juzi alipoulizwa huyo Msemaji wa Serikali kwamba inakuwaje Tanzanite halikuchukuliwa hatua na halijachukuliwa hatua hadi sasa, Msigwa akasema inawezekana gazeti hilo lilithibitisha kuwa 'Zitto na Maalim' wanashiriki vitendo hivyo!

Ndugu waandishi, Jambo hilo halikubaliki mbele ya macho ya waungwana na wapenda haki.

Nina mambo manne yafuatayo;-

1. Msigwa ajiuzulu mara moja.

Namtaka Msigwa athibitishe madai yake dhidi ya viongozi wa Chama changu. Akishindwa kuthibitisha atapaswa ajiuzulu. Asipojiuzulu nitamuomba bosi wake, Rais Samia amuondoe kwenye nafasi hiyo kwani ameshindwa kazi. Kwa kitendo alichokifanya Msigwa, kwa upendeleo wa wazi anaofanya, si tu anawadhalilisha viongozi wa Chama changu cha ACT Wazalendo, bali pia anamdhalilisha bosi wake. Na kwa mantiki hiyo, anawadhalilisha watanzania wote wanaomlipa mahahara na marupurupu anayofaidi kwani yote ni kodi zetu watanzania. Kwa sababu watu tutaamini kuwa ni Rais Samia ndiye anayemtuma kuja kudhalilisha watu jambo ambalo mimi binafsi sitaki kuamini kuwa ni sahihi. Kwa hiyo ajiuzulu, au aondolewe awekwe kando na apatikane mtanzania mwingine mwenye maadili na staha ahudumu nafasi hiyo ya Msemaji wa Serikali.

2. Msigwa aache kuishi enzi za Magufuli. Aache Magufuli aondoke na ushenzi wake peke yake.

Inaonekana wazi Msigwa yuko chini ya Rais Samia lakini anamtumikia Magufuli na Umagufuli. Haya mambo ya kudhalilisha watu, tulidhani yameondoka na Magufuli. Lakini kumbe bado wateule wa Magufuli wanayaendeleza hata sasa. Sisi wengine tulidhani tumezika enzi mbaya na kufungua enzi mpya, lakini wateule wa Magufuli wanaendeleza umagufuli chini ya Samia. Hili linashangaza na kusikitisha. Samia ampumzishe huyu mtu, amepwaya. Ampumzishe aende akafanye umagufuli wake nyumbani sebuleni kwake na familia yake kama anavyofanya Humphrey Polepole. Hataguswa na mtu.

3. Serikali iache upendeleo na ukandamizaji. Msigwa alichokifanya ni kukandamiza ukweli na kushadadia uongo na uzandiki. Ni kukandamiza haki na kushadadia dhulma. Serikali haipaswi kufanya kazi kwa mtindo huo. Ikiendelea kufanya kazi kwa mtindo huo, raia wataichoka. Kwa sababu wananchi wana akili timamu. Wanajua ukweli ni upi na wanajua uongo ni upi. Msigwa asijidanganye kuwa watu hawajui pumba na mchele. Nasisitiza, Msigwa ajiuzulu kulinda heshima ya aliyemteua. Asipojiuzulu, yule aliyemteua aone haja na umuhimu wa kumpumzisha kwa heshima.

4. Msigwa aache kutamani kazi ya Shaka. Yeye siyo msemaji wa CCM. Msemaji wa CCM ni Shaka. Kwamba Msigwa anajua nani ni mwanaCCM na nani si mwanaCCM, hiyo siyo kazi yake, ni kazi ya akina Shaka na wenzake ndani ya CCM. WanaCCM wenyewe wapo. Wana uwezo wa kusema na kujisemea. Wana uwezo wa kujitetea. Kukaa kwao kimya kwenye sakata la Hamza ni kwa kuwa walikuwa wakiujua ukweli, kwamba Hamza alikuwa kada wao.

Yeye Msigwa aliwashwa nini mpaka akisemee chama Chama Mapinduzi? Aache kuwashwa. Analipwa pesa za umma wa Watanzania kwa kazi aliyoteuliwa nayo ya Msemaji wa Serikali. Halipwi na CCM. Asijisahau. Aache kudandia kazi za watu. Kama yeye ni mwanaCCM aseme.

Mwisho, namuomba sana Msigwa awe na heshima na adabu kwa watu. Ilitosha tu kuonyesha heshima kwa marehwmu Maalim Seif na Zitto Kabwe angalau kwa kuomba radhi, kwa sababu amewakosea. Uungwana ni kuomba radhi. Lakini hajafanya hivyo hadi leo. Jambo linaloonesha alivyo na kiburi na jeuri.

Namuhasa tu, jeuri na kiburi mwisho wake mtamu sana!! Tuliwaona. Na tutamuona.

Asanteni.

Monalisa Joseph Ndala,
Kada wa ACT Wazalendo
22 Septemba, 2021.
 
Huu upuuzi umetoka kwenye chama kinachounda serkali Zanzibar, ni ujinga kufikiri mwajiliwa wa serkali anweza kujiuzuru ,kile cheo sio Cha siasa Kama Cha zito


USSR
Acha kudhihirisha ujinga wako. Mtu yeyote anaweza kujiuzulu kama ni mtu mwajibikaji (a responsible person).

Tatizo nchi yetu hii uwajibikaji na uwajibishwaji ni zero ndio maana mpaka watu kama nyie hamjui nini maana ya kujiuzulu. Eti 'mwajiliwa' wa 'serkali' hawezi kujiuzulu? Amekuwa nani?
 
Huyu dada ndo alikuwa anaongelea habari za Martin na Meya mstaafu kuripoti kesi ya Mbowe kutokea mahakamani kwa kuwachomea -In short anaonekana hana political maturity kabisa
Anafaa kubakia chadema kwanza ndio aende ACT

USSR
 
Huyu dada ndo alikuwa anaongelea habari za Martin na Meya mstaafu kuripoti kesi ya Mbowe kutokea mahakamani kwa kuwachomea -In short anaonekana hana political maturity kabisa
Usilolijua na la kukushangaza zaidi, siku moja utamkuta kajaa tele ndani ya CCM!

Hapo ACT ni kituo tu cha kuelekea huko.
 
GERSON MSIGWA AJIUZULU

Ndugu zangu waandishi wa habari, kwanza nawashukuru kwa kuitikia wito wangu na kufika hapa leo. Nimewaita kwa jambo moja tu ambalo niliona haitakuwa sawasawa likiachwa na kupita hivi hivi...
Akisikia hali masikioni mkavu usiache kutuletea mrejesho
 
Back
Top Bottom