AMEPOTEA AMEPOTEA AMEPOTEA
Pichani ni Oscar Robart Mgowole
Ana umri wa miaka 43, kazi yake ni Mhasibu,mkazi wa Dar es saalam.
Amepotea toka tarehe 20 May 2024 alipokuwa ameenda Dodoma kuripoti kwenye shitaka lake lililokuwa linakabiliwa ,Kituo cha Polisi Kati Dodoma.
Alifikia Lodge ya kulala wageni , ili siku husika (kesho yake) aeeze kuripoti kituo cha polisi Kati Dodoma,
Lakini haikuwa hivyo; kwani asubuhi kulipokucha iligundulika hayupo chumbani kwake alipofikia.
Polisi wa kituo cha Polisi kati, Dodoma, ambako alitakiwa kwenda kuripoti siku hiyo, wanasema hakwenda kuripoti na wala hawajui yupo wapi.
Simu za Oscar Robart Mgowole zikawa hazipatikani kuanzia siku hiyo hadi leo hii.
Yoyote atakayepata taarifa zitakazo fanikisha kumpata Bwana Oscar Robart Mgowole
anaweza kuwasiliana na familia yake kupitia namba ya mke wake Oscar ambayo ni +255 689 026 411
Watu wanaisha Jamani 😭😭😭😭😭