Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,639
- 729,584
Najua ni wazi hujui ni ipi, na inaweza ikatokea umeipiga tu katika mazingira fulani yasiyo na matayarisho yoyote.
Lakini niamini ni mojawapo kati ya picha zako ndio itakayotumika kuwekwa juu ya jeneza lako ama kama ikitokea unasafirishwa ndio itawekwa pale mbele kwenye coaster ...na unajua kwanini huijui?
Ni kwa vile kwanza atakayeichagua si wewe na kwa vile unaogopa kifo na hujui utakufa lini.
Unapotafuta ajira unatakiwa kuleta passport size zenye kuonekana vema! Yani sura yote mpaka masikio.
Kumbuka ni picha hiyohiyo itakayotumika kuwekwa kwenye vyombo vya habari kwa kichwa cha habari chenye maandishi makubwa ANATAFUTWA siku ukilikoroga.
Huwa nikiwaona watu wanapiga picha nakuwa nawaza mengi sana