Mojawapo kati ya picha zako

Mojawapo kati ya picha zako

Hahaha, unaweza kua nazo lakini ex wako akakukomoa kuleta picha yako ulipokua kwa mganga 🙄
 
kweli aisee duh nakumbuka mmoja anayenihusu tulichukua kwenye picha alizotutumia whats app sababu simu yake likuwa na password .. kingine tuwatumie picha nzuri marafiki na ndugu
 
Sijaona hiyo sehemu ulipoandika "kwa wale wawekao picha"
Umesema tukuamini tu...
Watu tunaendaga kwa facts bwana mkubwa. Kubali kurekebishwa!!
Hapana nitakubishia milele si kila kitu lazima kiandikwe nini maana basi ya kuitwa great thinker?
 
Mr Mshana jr nakufuatilia sana hapa jf ila sijakuelewa ni mtu aina gana hasa!!! Macho huona mengi, ila si yote yanatazamwa pia tunajua mengi ila si yote tuyajuayo yanasemwa. Mf. Wengi walio saliti ndoa huenda wakafariki bila kufichua siri hiyo kwa wenza wao. Japo ni kweli mengine tuna amua kupotezea.
 
c9272bf51fab582d75515440aed91dc7.jpg
Najua ni wazi hujui ni ipi, na inaweza ikatokea umeipiga tu katika mazingira fulani yasiyo na matayarisho yoyote... Lakini niamini ni mojawapo kati ya picha zako ndio itakayotumika kuwekwa juu ya jeneza lako ama kama ikitokea unasafirishwa ndio itawekwa pale mbele kwenye coaster ...na unajua kwanini huijui? Ni kwa vile kwanza atakayeichagua si wewe na kwa vile unaogopa kifo na hujui utakufa lini
Unapotafuta ajira unatakiwa kuleta passport size zenye kuonekana vema! Yani sura yote mpaka masikio... Kumbuka ni picha hiyohiyo itakayotumika kuwekwa kwenye vyombo vya habari kwa kichwa cha habari chenye maandishi makubwa ANATAFUTWA siku ukilikoroga
Huwa nikiwaona watu wanapiga picha nakuwa nawaza mengi sana
9c2e03d9347f3f18c5f831d8abbfc161.jpg


Wabongo bwana... Mbwembwe nyingi kumbe bure kabisa.
Si umesema umeandika wewe??? Sasa hivi unasema sio kila kitu lazima uandike...
Which is which now!!! Umeandika hukuandika!!!
Usitufanye sisi watoto wadogo bwana....
Ukiona haikuhusu ujue si kwa ajili yako.. Usilazimishe kisichowezekana
 
Mr Mshana jr nakufuatilia sana hapa jf ila sijakuelewa ni mtu aina gana hasa!!! Macho huona mengi, ila si yote yanatazamwa pia tunajua mengi ila si yote tuyajuayo yanasemwa. Mf. Wengi walio saliti ndoa huenda wakafariki bila kufichua siri hiyo kwa wenza wao. Japo ni kweli mengine tuna amua kupotezea.
Na kumbuka wale wawekewao picha zao ni wale tu waliobarikiwa mazishi rasmi na ndugu zao! Kuna watu hufia ugenini na kuzikwa na serikali, wengine hufa katika mazingira ambayo huwezi kuwazika tena ama hata bila kujua kama wameshakufa
 
Una panic kwa sababu nimekuumbua... Hahaha
Watu tunaenda kwa facts bro!! Hatuendi kimbumbumbu!!
Mmh wapi nimepaniki Labda tu kama hujui maana ya kupaniki, na unapozungumzia facts ni zipi hizo hebu ziweke hapa... Kumbuka huu ni mjadala huru na mimi ndio kisababishi
 
Back
Top Bottom