Moja ya ndege za ATCL Bombardia iko Zanzibar wiki ya pili sasa inatengenezwa

Mafundi wenyewe ndo hawa Wazanzibar!? Jamani msicheze na bahari hiyo
tapatalk_1566328573760.jpeg
 
Alafu unaambiwa kampuni hiyo kwa sasa haipo inasemekana huko kwao imepigwa marufuku
Duuuuu hapo lazima manager ataambiwa ajitokeze atoe ufafanuzi, japo hautakuwa ufafanuzi wa tatizo halisi, bali aliyenunua hizo ndege ndio atampangia aseme nini!
 
Hahaaa tunatunza tuu kumbu kumbu sie siku tutakapo mburuza Mbele ya mahakama ya ufisidi atalia na kusaga meno. Hatuja sahau kile Kivuko chake Fake alicho kificha kule jeshini na sasa kaongeza kununua li dege bovu.

Halafu utamsikia bwana Meko, "Watanzania tumeibiwa sanaa, wakati jenyewe ndio jizi kuu na genge lake linalo jificha ktk kivuli cha uzalendo.
aliyeruhusu picha kupigwa na aliyechukua hio picha watatafutwa mpaka watekwe sijui kwa nini jiwe anapenda kufichaficha habari kama hizo?
 
Hivi mazuri yanaweza kungoja kutangazwa?
Yenyewe yanakawaida ya kujitangaza kwa uzuri wake. Ukiona watu wana ng'ang'ania kukiremba kitu (mfano Jiwe) chunguza utagundua ni kibovu hakuna mfano.
Kwa maisha ya kawaida tu. Mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe.
Nyie wachache mnaosema Rais anapewa sifa asizostahili mnajisumbua bure.
Nakumbuka, siku za nyuma, nikiwa sekondari kuna mwalimu tulikuwa tunamchukia sana kutokana namna alivyofanya mambo yake. Tuliwa kumukandia akashushwa cheo. Baadae nilipokuwa nikajua yule mwalimu alikuwa sahihi kwa zaidi ya asilimia 100. Sasa nyinyi ndio kama mimi wa miaka hiyo, hii nafasi ichezeeni.

Naapa akitoka Magufuli hii nchi hakuna wa kuiongoza! Na kwanini atoke? Ikiwezekana akae mpaka pumzi yake ya mwisho.
 
Haha.. Hakuna kitu kinaniacha hoi kama wewe kutokujua kwamba Rais anashauriwa anunue nini na akinunulie wapi. Haamki na kwenda kama anaenda super market kuhemea.
Hio nayo inahitaji kuelezewa?
Unakumbuka siku anayakataa makampuni ya Waziri Mkuu ya kununua korosho live akasema nitapeleka jeshi, alishauriwa na nani.
 
Unakumbuka siku anayakataa makampuni ya Waziri Mkuu ya kununua korosho live akasema nitapeleka jeshi, alishauriwa na nani.
Kwani tokea ameanza kuiongoza hii nchi amefanya mambo mawili tu?? Kununua ndege mbovu(kama unavyoziita) na kuamuru jeshi likanunue korosho?? Think, bro! Think.
Ukiweka kwenye mizani - Binadamu yeyote anateleza kwa kujua au kutokujua ila kiuhalisia Magufuli ana mambo mengi mazuri kuliko hayo mabaya machache mnayoyaremba kwa lugha nzuri na za picha yajenge taswira mbaya.!!
 
Unasema kweli kabisa. Je tatizo la ndege kuharibika au kupata hitilafu nani anajua litatokea saa ngapi??

Maisha yako yote hujawahi kununua kitu na kikapata shida right away.??

Kama ni 100℅ perfect kwa sababu umenunulia bei kubwa ni kwanini kampuni zinaweka warranty??

Sasa hayo unasema ww, what if ungesema tu maybe iliharibika wakaenda kununua visaa China so now wanafunga, ingekuwaje?
 
Engine ambayo bei yake ni millions kadhaa replacement halafu imefunguliwa mahala holela ivyo let me guess likianguka vua watafunika na turubai.

Inataka uelewe watu wanavyoangalia biashara ya kutoa huduma na vitu gani uwekwa kwenye accounting za service costs kama maintainance both schedules and regular in line with expected hours za ndege au mileage za mabasi ndio uone ni kwa kiasi management ya ATCL ilivyo bomu kama ndege inaweza kufikia hatua hiyo halfway through its journey, achilia mbali uzembe wa hali ya juu kuacha ifanyiwe major repair nje hangar.

Sio chuki wala majungu serikari inataka ipate ushahidi gani management ya ATCL ni bomu ni kwamba tu wao wenyewe uelewa wao wa maswala ya biashara una utata ndio maana awaoni shida.
 
Unasema kweli kabisa. Je tatizo la ndege kuharibika au kupata hitilafu nani anajua litatokea saa ngapi??

Maisha yako yote hujawahi kununua kitu na kikapata shida right away.??

Kama ni 100℅ perfect kwa sababu umenunulia bei kubwa ni kwanini kampuni zinaweka warranty??
Mkuu huwezi kusema hujui ndege itaharibika saa ngapi, ikiwa angani je, kabla ya ndege kuruka internal system zote lazima zihakikishwe zinafanya kazi kwa 100%, usalama wa ndege ni tofauti na gari kuwa utaenda tu hata breki hazifanyikazi utasimama kwa hand break au mafuta yakiisha utabeba kidumu ukimbilie shell, service ya ndege huwa haisubiri hadi iharibike.
 
Haha.. Hakuna kitu kinaniacha hoi kama wewe kutokujua kwamba Rais anashauriwa anunue nini na akinunulie wapi. Haamki na kwenda kama anaenda super market kuhemea.
Hio nayo inahitaji kuelezewa?

Tupe udhibitisho wa kauli yako
 
Sasa hayo unasema ww, what if ungesema tu maybe iliharibika wakaenda kununua visaa China so now wanafunga, ingekuwaje?
Hicho ni kiashirio tosha ya kuwa Rais wetu anajali. Hajaamua kufanya siri na pili walipogundua ina shida ikapelekwa kukarabatiwa.. Au nyie mlitaka awafurahishe, aiache mbaki na dhana ni nzima, watu waanguke wafe?
 
Back
Top Bottom