ATCL: Si kweli kuwa ndege 6 hazifanyi kazi, ndege 2 zina shida ya Injini, ndege 1 imekamatwa Uholanzi

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) Eng. Mafundi anatolea ufafanuzi juu ya tuhuma zilizoletwa na Kiongozi Mkuu wa ATC Wazalendo, Zitto Kabwe kuwa ndege 6 za ATCL ni mbovu na zimeegeshwa bila kufanya kazi.

Anasema kuwa ndege mbili ndogo zina shida ya njini na spare zake zimeshaagizwa

Ndege moja imekamatwa Uholanzi na kufanya kuwa na jumla ya ndege tatu na sio sita

Itakumbukwa hizi ndege aina ya Bombardier ndizo zilinunuliwa mapema na Rais Magufuli kwa hiyo ndege 9 zipo zinafanya kazi

Zitto ni mwogo kama wanasiasa wengine

Kuhusu tuhuma alizotoa Zitto Kabwe, soma Zitto Kabwe: Katika ndege 12 alizonunua Hayati Magufuli, ndege 6 hazifanyi kazi, ziko grounded, zina kutu, ingawa tuliambiwa ni mpya


=====

UPDATES

======

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Evarist anasema: Hakuna ndege sita ambazo ni mbovu, si habari za kweli, ndege mpya zilizonunuliwa na Serikali ni 11, ndege ya 12 ni ambayo ilirithiwa kutoka ATCL ya zamani na ilikuwa ni ndege ya zamani.

Ndege hiyo ilisimamishwa siku nyingi kutokana na masuala ya usalama kwa sasa ipo Macca kwa matengenezo tunategemea makubwa mwezi Machi au Aprili itakuwa imemalizika, hivyo imekuwa haifanyi kazi muda mrefu nadhani tangu Mwaka 2016 au 2017.

Kuhusu Ndege 11, mchanganuo wake, kuna ndege 5 ndogo ambazo watu wanaziita Bombardier , zipo 4 aina ya Airbus, tuna 2 kubwa aina ya Dreamliner ambazo kwa sasa tunafanya safari nne kwenda India kwa wiki na safari moja kwenda China, na hivi karibuni tumeongezewa rudi moja kwenda China, maana yake tutakuwa na ruti mbili za China.

Kuhusu ndege zetu za kati ambazo nimesema ni nne, kama tulivyopewa taarifa zina matatizo ya Injini, watengenezaji wa ndege hizo waligundua kuwa kuna matatizo kwa hiyo baada ya muda injini hizo lazima zifanyiwe maboresho, zinapopelekwa kiwandani yule mtengenezaji anatakiwa kutuletea Injini za ziada.

Changamoto iliyopo ni kuwa mtegenezaji hana Injini za ziada kwa kuwa alitengeneza chache na watumiaji wakawa wengi, siyo suala la ATCL peke yake ni mashirika mengi.

Hivyo, kati ya ndege hizo 4 nilizozitaja za saizi ya kati, moja inafanya kazi, mbili zina matatizo ya Injini, moja ndio hiyo iliyokamatwa Uholanzi ambayo ni nzima, ilienda kwa ajili ya matengenezo wakati inarejea ikakamatwa kutokana na masuala ya kisheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshalitolea taarifa Bungeni.


CHANZO: WASAFI FM
 
Anaongea sasa hivi mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Tanzania Eng .mafundi na wasafi FM amesema ndege mbili aina ya ndogo zinashida ya njini na spare zake zimeshaagiwa...
Mkuu unapataje ujasiri wa kumsikiliza Zito. Huyu ni miongi mwa wachumia tumbo wakubwa nchi hii. Hana tofauti na kina Lipumba.

Ni mara 10 nimsikilize mzee wa ubwabwa angalau niweze kucheka, kuliko hawa wanasiasa uchwara wa vyama uchwara ambao uongo ndio sera zao.

Zito asome alama za nyakati. Uongo ulikuwa unalipa sana miaka ile kuvutia misukule chamani. Lakini leo haulipi na hauna maana yoyote maana kila mtu ni mjanja.
 
Uzuri wa zito alisha toa tahadhari kuwa usimuamini mwanasiasa, yanayoendelea ni kama umeenda mahali ukaona kibao “ park at your own risk” baadae ulalamike eti niliacha laptop, camera, fedha na bastola nimekuta vimeibiwa… huo ni ukichaa..
 
Zitto ni mlamba Asali na mnafiki wa Taifa!

Zitto ni mpigaji kama wapogaji wengine toka Msoga!

Zitto alimf8lisi Bernard Membe na kisha kumtupa kama ganda la muwa!

Kama Zitto yumo humu,abishe na tuweke mafaili wazi.
Unamaanisha mwanakitengo mbobevu kapunwa na yule kijana wa ujiji. Ama kweli ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom