Moja wapo ya Fungu kwenye Biblia linalotafsiriwa vibaya: Matendo ya Mitume 10:15

Plaintiff

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
308
203
Watu wanalitumia fungu hili kuhalalisha kula wanyama ambao wamekatazwa katika kitabu cha Mambo ya walawi. Na kwa kuweka mambo sawa fungu hili halizungumzii vyakula, na kudhihirisha hili ukisoma hiyo matendo ya mitume 10 yote utaelewa.

Fungu lenyewe linasema "Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, vituvilivyotakaswa na Mungu usiviite wewe najisi." Mwisho wa kunukuu.

Kwa kifupi labda nisimulie hiki kisa kilivyokuwa,

Ukisoma Matendo ya Mitume 10 kuanzia fungu la 9 Petro alikuwa na njaa sana wakati msosi unaandaliwa alizimia na alioneshwa maono na katika maono hayo Kilishushwa Chombo chenye pembe nne kutoka mbinguni ambamo ndani yake kulikuwa na wanyama mbalimbali, kisha sauti ikasema Ondoka Petro uchinje ule, Petro akajibu akisema Hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu wala najisi.

Na tendo hilo la kumuambia kwamba achinje ale lilifanyika mara tatu na zote Petro alikataa, ndio ile sauti ikamwambia vitu alivyovitakasa Bwana usiviite najisi. Na mwisho alipozidi kugoma kile chombo kikarudishwa juu.

Kabla sijaendelea hapa kuna mambo mawili ya kujiuliza,

1. Bila shaka wanyama walikuwepo mle ndani wote walikuwa ni Najisi ndio maana Petro aliwakataa, Na hakuwa anamkatalia Binadamu mwenzake, Bali alikuwa anaikataa sauti ya Mungu.

2. Kama sheria ile ya mambo ya walawi ilifutwa, kama watu wanavyodai kwenye Marko 7 na Mathayo 15(Hili nitaletea uzi nalo maana nalo watu wanadanganywa sana). Ni kwanini Petro alikuwa anakataa na aliwaita wale wanyama najisi na wachafu? Zingatia huyu alikuwa mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu.

Na mwisho kabisa yale yalikuwa ni maono tu na wakati anaendelea kuyafikiria kwamba yana maana gani, Roho mtakatifu akamuambia kuna watu watatu kawatuma kuja kwake hivyo aongozane nao.

Tafsiri ya Maono yale inakuja kupatikana katika Matendo ya Mitume 10:28 ambayo inasema "Akawaambia, Ninyi mnajua kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, Lakini Mungu amenionya, nisimuite mtu awaye yote mchafu wala Najisi."

Watu wanachukua vifungu kidogo ambavyo vinafavor vitu vyao ambavyo kwa macho yao vinawavutia ila hawasemu ukweli.

Jina la Bwana Libarikiwe.

Muwe na Usiku mwema.
 
Vyovyote iwavyo hakuna bado duniani ktk kizazi hiki Mkristo anayeweza kutoka hadharani hata Yesu ashuke leo aruhusu tumdanganye kwa utani kwamba tumezifuata amri zake japo kwa 5%,huyo mtu hayupo nasisitiza hayupo cha kufanya tutegemee tu huruma ya Mungu siku macho tukiyafunga.

Utakuta sinywi pombe nazini,sizini naiba,siibi nasengenya,sisengenyi nakula nguruwe (wengine wanasema ni dhambi kula nguruwe wakati dhambi nyengine zote chafu za kuwatenga na Mungu wanafanya) sili Nguruwe wake za watu siwaachi wake za watu siwaachi natamani visivyokuwa vyangu in short taja dhambi unayoijua hakuna asiyeitenda ninyi watu wenye imani kali mnafanya maisha yanakuwa magumu huku ya kwenu hamjayatengeneza.

Ondoeni kwanza udhaifu wenu ambao kimsingi hata ninyi wenyewe hamuwezi kuuondoa sababu bado mna hulka ya ubinadamu kama wale mnaotaka wabadilike walivyo na wanavyotarajia Mungu awaondolee udhaifu huo.
 
Na hapa je??

Wakolosai 2:16-17
[16]Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

[17]mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
 
Na hapa je??

1 Timotheo 4:1-5
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

[2]kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

[3]wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

[4]Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;

[5]kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
 
Nashangaa wewe unaepinga kauli ya mungu wazi wazi
Mungu alimruhusu ale kwakumaanisha neema imepokelewa na kwa mataifa.
Unapokataa nikusema neema imeishia israel na sisi tuliohesabiwa kuwa najisi hatunayo kamwe
Huwez kufanya hvy ukaendelea kujiita mkristo

Mungu alinena waziwazi je vitu nilivyovitakasa ww ni nani uviitae najisi
Unataka kusema petro wasingeweza kula izo nyama tena kutokea pale
Alikuwa huru kula atakavyo
 
Matendo ya Mitume 10:11-15
[11]akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;

[12]ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.

[13]Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.

[14]Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.

[15]Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.

Mbn ipo wazi sanaa
 
Na hapa je??

1 Timotheo 4:1-5
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

[2]kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

[3]wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

[4]Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;

[5]kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Soma hii alafu useme Tukuamini ww ama mungu?
Biblia inasema watu kama ww tujiepushe nao
Maana wana mafundisho ya shetani
 
Wagalatia 3:9
Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.

Wagalatia 3:10
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

Wagalatia 3:11
Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.
 
Yohana 5:45
Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.

Inategemeana na unaemtumaini kama unamtumaini YESU hata ukila kiti moto yeye hana muda na wewe(hauhesabiwi dhambi - hakushtaki) hivyo unabaki na uzima wa milele
Kama unamtumaini Musa unahesabiwa dhambi hivyo kupata mauti
 
2 Wakorintho 3:1
Je! Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa kuja kwenu, au kutoka kwenu?

2 Wakorintho 3:2
Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;

2 Wakorintho 3:3
mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.

2 Wakorintho 3:4
Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo.

2 Wakorintho 3:5
Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu.

2 Wakorintho 3:6
Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

Roho haijui nguruwe ni nini, haijui kuzini ni kitu gani. Ndiyo maana roho inatia uzima
Andiko(Torati) huua
 
2 Wakorintho 3:13
nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;

2 Wakorintho 3:14
ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;

2 Wakorintho 3:15
ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.

2 Wakorintho 3:16
Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

Kama unaelewa utaelewa, kama umezaliwa ili upotee nalo ni jambo jema.
 
Marko 7:18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;

Marko 7:19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote

1 Wakorintho 10:25 Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;

1 Wakorintho 10:27 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.
 
2 Wakorintho 3:13
nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;

2 Wakorintho 3:14
ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;

2 Wakorintho 3:15
ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.

2 Wakorintho 3:16
Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

Kama unaelewa utaelewa, kama umezaliwa ili upotee nalo ni jambo jema.
tembea na mungu,usijiwekee kibanda mungu hajasimama,,,, yeye anaendelea na safari alisema na uyo uyo amekuja kusema kwann alikataza ivyo vyakula visiliwe,,, alivingungia visiliwe akionyesha kuwa neema kwetu sisi hamna mpaka wayahudi walipomkataa ,masihi,,,akaviruhusu viliwe pale aliporuhusu sisi watu najisim kwa israel kupokea neema....huwezi ukawa huli izo nyama na ukawa unamuamini kristo na neema maana neema ilikuja na kuachiliwa hvyo vitu ....na kama ubatizo ulivyowakilisha kufa na kufufuka kwa yesu iii nayo inaashiria neema kukubaliwa kwa mataifa ambayo apo awali tulikuwa najisi mbele za bwana
 
2 Wakorintho 3:13
nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;

2 Wakorintho 3:14
ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;

2 Wakorintho 3:15
ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.

2 Wakorintho 3:16
Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

Kama unaelewa utaelewa, kama umezaliwa ili upotee nalo ni jambo jema.
Na hapa je??

1 Timotheo 4:1-5
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

[2]kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

[3]wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

[4]Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;

[5]kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
 
tembea na mungu,usijiwekee kibanda mungu hajasimama,,,, yeye anaendelea na safari alisema na uyo uyo amekuja kusema kwann alikataza ivyo vyakula visiliwe,,, alivingungia visiliwe akionyesha kuwa neema kwetu sisi hamna mpaka wayahudi walipomkataa ,masihi,,,akaviruhusu viliwe pale aliporuhusu sisi watu najisim kwa israel kupokea neema....huwezi ukawa huli izo nyama na ukawa unamuamini kristo na neema maana neema ilikuja na kuachiliwa hvyo vitu ....na kama ubatizo ulivyowakilisha kufa na kufufuka kwa yesu iii nayo inaashiria neema kukubaliwa kwa mataifa ambayo apo awali tulikuwa najisi mbele za bwana
Tuko pamoja
 
Back
Top Bottom