Plaintiff
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 308
- 209
Watu wanalitumia fungu hili kuhalalisha kula wanyama ambao wamekatazwa katika kitabu cha Mambo ya walawi. Na kwa kuweka mambo sawa fungu hili halizungumzii vyakula, na kudhihirisha hili ukisoma hiyo matendo ya mitume 10 yote utaelewa.
Fungu lenyewe linasema "Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, vituvilivyotakaswa na Mungu usiviite wewe najisi." Mwisho wa kunukuu.
Kwa kifupi labda nisimulie hiki kisa kilivyokuwa,
Ukisoma Matendo ya Mitume 10 kuanzia fungu la 9 Petro alikuwa na njaa sana wakati msosi unaandaliwa alizimia na alioneshwa maono na katika maono hayo Kilishushwa Chombo chenye pembe nne kutoka mbinguni ambamo ndani yake kulikuwa na wanyama mbalimbali, kisha sauti ikasema Ondoka Petro uchinje ule, Petro akajibu akisema Hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu wala najisi.
Na tendo hilo la kumuambia kwamba achinje ale lilifanyika mara tatu na zote Petro alikataa, ndio ile sauti ikamwambia vitu alivyovitakasa Bwana usiviite najisi. Na mwisho alipozidi kugoma kile chombo kikarudishwa juu.
Kabla sijaendelea hapa kuna mambo mawili ya kujiuliza,
1. Bila shaka wanyama walikuwepo mle ndani wote walikuwa ni Najisi ndio maana Petro aliwakataa, Na hakuwa anamkatalia Binadamu mwenzake, Bali alikuwa anaikataa sauti ya Mungu.
2. Kama sheria ile ya mambo ya walawi ilifutwa, kama watu wanavyodai kwenye Marko 7 na Mathayo 15(Hili nitaletea uzi nalo maana nalo watu wanadanganywa sana). Ni kwanini Petro alikuwa anakataa na aliwaita wale wanyama najisi na wachafu? Zingatia huyu alikuwa mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu.
Na mwisho kabisa yale yalikuwa ni maono tu na wakati anaendelea kuyafikiria kwamba yana maana gani, Roho mtakatifu akamuambia kuna watu watatu kawatuma kuja kwake hivyo aongozane nao.
Tafsiri ya Maono yale inakuja kupatikana katika Matendo ya Mitume 10:28 ambayo inasema "Akawaambia, Ninyi mnajua kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, Lakini Mungu amenionya, nisimuite mtu awaye yote mchafu wala Najisi."
Watu wanachukua vifungu kidogo ambavyo vinafavor vitu vyao ambavyo kwa macho yao vinawavutia ila hawasemu ukweli.
Jina la Bwana Libarikiwe.
Muwe na Usiku mwema.