Uhusiano wa fedha na Hatima ya uzao wako

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi
Mwanadamu katika lugha ya kiroho ana mwili, ana nafsi na ana roho, ndio maana mwz 1:26, Mungu anamuumba Mwandamu Roho, Mwz 2:7 anaumba mwili na nafsi Vyote vinafanya kazi Kwa ushirikiano ndani ya Mwanadamu.

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Mungu hajawai kubadili utaratibu wake Hadi kesho Mungu akitaka kuleta MTU mwanadamu anaanza na Roho Kwanza na mwili anakuja kuchukua Kwa mwanamke

Wakati Yesu anazaliwa , Yesu alikuwepo kabla hata ulimwengu kuwepo lakini hakuwa na mwili WA nyama kama wanadamu na ndio maana alipokuwa anakuja duniani ulitafutwa mwili ili aweze kuja Kwa Sura ya mwandamu na ndipo bikira Mariam alipewa nafsi hiyo ya kupitisha mwili WA Yesu kwa njia ya kibinadamu

Waebrania 10:5
[5]Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,
Dhabihu na toleo hukutaka,
Lakini mwili uliniwekea tayari;

Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Kuna mahusiano makubwa Kati ya fedha yako na uzao wako

A. Fedha inakaa kwenye Moyo
Mathayo 6:21kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Moyo Kibiblia sio Moyo WA Damu na nyama tunazungumzia MTU wa ndani ndio huyo ambaye ana beba vitu Vyote kuanzia Roho WA Mungu, fedha yako, mawazo yako , nafsi yako na etc kwa hiyo fedha yako siku zote unabeba Roho iliyoko ndani yako

B. Roho iliyoko nyuma yake
Fedha unabeba Roho ndani yake hivyo popote unapojipatia kipato kuna hamua ni Roho yupo atakaye tawala kesho yako yaani uzao wako

Luka 22:3-6 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.
Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. Wakafurahi, wakapatana
Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.

Najifikiri kitendo cha Yuda kupokea wazo la kumsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha shetani akamwingia hapo hapo , ina maana siku zote chunga Sana unapopokea fedha inatoka kwa Roho hipi

C. Imebeba nini?
Wakati mwingine fedha inabeba magonjwa na mengine ni ya kuambukizwa na mengine sio ya kuambukiza , unaweza kupelekea kizazi chako magonjwa pasipo kujua

2 Wafalme 5:1,10,15-16,20,27
[1]Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda;

[10]Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.
.
[15]Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.

[16]Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
.
[20]Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama BWANA aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake.

[27]Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.


Najiuliza maswali wale watoto WA Gehazi wanapomuuliza Baba Yao kwanini wao wanazaliwa na ukoma sizani kama angepata usajiri kwamba alikwenda kupokea posho ya namaani ambayo Mungu aliwakataza kupokea

5. Udanganyifu
Fedha inabeba na Roho ya udanganyifu , na uzao unakuwa na kizazi cha watu wahongo

Matendo ya Mitume 5:1-3
[1]Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,
,
[2]akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja .

[3]Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
 
Petro alishangaa Sana wakina anania na safina wamekuja mbele zake lakini na shetani pamoja naye , kumbe fedha ilipofika mikononi mwa Petro alimwona shetani akashangaa wamekutana na shetani wapi kumbe kwenye uongo

Yohana 8:44
[44]Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

6. Uasherati na Uzinzi

Waebrania 7:9-10 Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi;
.
[10]kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.

Wakati Ibrahimu anatoka vitani ameshinda vita akaja na fedha yake kumshukuru Mungu wakati anafika njia panda anapokelewa na wafalme wawili mmoja WA sodoma na mwingine Mfalme wa Salem , Mungu akamwongoza kumpa Mfalme wa Salem mfalme Melkizedeki

Biblia inasema hata lawi alitoa ilo fungu la kumi alilotoa Ibrahimu wakati lawi ni kizazi cha 4 baada ya Ibrahimu ebu tufikiria angempatia hiyo fedha Mfalme wa sodoma ina maana lawi angekuwa kwenye agano na Miungu ya sodoma ambayo kulikuwa na Uzinzi na uasherati ambao ulimkasiliaha Mungu ata akaamua kuwaangamiza
 
Uhusiano wa MTU wa ndani na Roho.
Waefeso 3:17 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;

Roho wowote anakaa ndani ya Moyo wa Mwandamu kupitia Moyo au MTU wa ndani roho anapata utawala wa Maisha yako kuanzia kwenye uzao Hadi kesho yako ndio maana roho zote zinakaa kwenye Moyo.

Njia 2 za roho kuingia kwa mwanadamu

A.Kwa fedha
Kwa njia ya fedha roho anaingia kwenye Moyo WA Mwanadamu, maana hazina yako ilipo ndipo na Moyo wako ulipo

B. Maneno ya Moyo

Unaweza kufunga agano na Roho Kwa njia ya mapatano kutoka moyoni mwako , na Ayo mapatano yanaitwa kihapo au makubaliano

Kwenye bustani ya Edeni adamu na Eva walikubaliana kumfuata shetani kupitia Kula tunda Kwa hiyo kupitia maneno unakuwa umekaribisha uhusiano wako na Roho WA Mungu au Miungu

Nb

Siku zote mtoto anatoka Rohoni Kwanza ndio maana utaskia MTU alikuwa tasa akapata mtoto au MTU

Uhusiano wa mtoto na Baba

Kuna uhusiano Mkubwa sana WA mtoto na Baba kwa sababu mtoto siku zote anabeba Damu ya Baba

Ndani ya Damu kuna nini

A. Roho ( uhai)
Mambo ya Walawi 17:11Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.

Siku zote ndani ya Damu ya Baba kuna kuwa na Roho ambaye Baba anamtumikia kama unamtukia roho WA dhambi ujue na mtoto pia atapokea roho Yule Yule WA dhambi na kama unamtukia roho WA nuru hivyo hivyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom