MOI Wajiunga Tena na MGOMO

Watanzania tunabahati ya kupata starting point ya kuikataa serikali iliyopo madarakani tunashindwa kuitumia
 
Madaktari tafadhari sana mie ninawaamini sana kuweni na msimamo mmoja na wakudumu sio leo alfa kesho beta
 
Afya ya binadamu yoyote ni muhimu na katika binadamu hakuna aliye wa zaidi kuliko mwenzake na ndiyo maana wote hufa na baada yahapo kwenda kwa Mungu ama motoni kwa tunavyo amini na ndivyo ilivyo,ila Zaidi Ulimboka ni Kiongozi wa MAT na ni dokta mwenzao hawakufurahishwa na kilicho mkumba na mazingina yalivyokuwa.

hapo kwenye red, acha uongo Dr. Ulimboka siyo kiongozi wa MAT. Ni Kiongozi wa Jumuiya wa Madaktari. Jumuiya iliundwa baada ya kuona akina DR. Namala Mkopi wameshindwa kukaza mgomo.
 
tafadhari usishabikie propaganda ndugu yangu naomba fika moi saa hizi ndo uupate ukweli, kuonyesha video kwani inasaidia?ukihitaji huduma ndo utajua kumbe mgomo upo tena wa moto
 
Sheria ni siku 5 hujaonekana kazini unajifukuzisha kazi walishaifanyia marekebisho na imeshaanza kutumika muda mrefu, kuwa usipoonekana kazini siku 5 mfululuzo umejifukuzisha kazi. So walichofanya MOI n kuonekana kazini then wanarudi tena kwenye A kama wameanza mgomo leo unaesabu siku 5 za kazi wanarudi tena mchezo huo wataucheza weee hadi watakapo pata majibu ya matakwa yao


Thank you for the update
 
Tunachangia tu hapa ,coz tuna afya ila shubiri wanaijua wagonjwa walokutana na mgomo
 
Kwa vile wao wanatibiwa India hata waganga wa kienyeji wanapelekwa hawana time na nyie mlio wapa ridhaa ya kuongoza nchi.
 
wengi mnaonekana kuunga mgomo utazan nyie wote madokta! nakubal hizi ni harakat na naamin kati yenu hakuna hata mmoja mwenye mgonjwa aliye hoi taabani MOI n.k
 
Am very disappointed kuna watu kama wewe TZ? U are conservative and rigid, blind and deaf. Pole sana. U r on the wrong side of river. Hamna daktari anaetafuta umaarufu. Hujui unachoongea. Wewe na wale jamaa wa Magamba lenu moja. Ungekuwa unajua nusu tu ya yanayoendelea ungekaa kimya kabisa.
 
Serikali yangu baada ya kupigwa kwa dr.Ulimboka na upelelezi haujatupa tumaini la kupatikana watu waliofanya unyama ule, hapa naungana na madaktari ktk kitendo chao cha kugoma kufanya kazi kutokana na hatari ya maisha yao wenyewe. Mazingira bora huanza na maisha yao kutokuwa hatarini na sasa hivi serikali mmewapa sababu madaktari...
 
wengi mnaonekana kuunga mgomo utazan nyie wote madokta! nakubal hizi ni harakat na naamin kati yenu hakuna hata mmoja mwenye mgonjwa aliye hoi taabani MOI n.k

Its so sad watu wanafurahia sana wakisikia mgomo umeanza au unaendelee! Why?
 
Its so sad watu wanafurahia sana wakisikia mgomo umeanza au unaendelee! Why?
Mkuu wangu binafsi yangu sikubaliani kabisa na mgomo ulotokea mwanzo na sababu zangu nimeziweka wazi kabisa. Lakini pamoja na mgomo ule kutoafiiana nao kwa uhalisia wake, hakuna sababu wala uhalali wa serikali yetu kufikia kufanya jaribio la mauaji wakati tunavyo vyombo vya sheria. Imekuwa mazoea kwa serikali yetu kila inapopingwa basi lazima mtu au watu wafe kwanza kutia adabu. Huu ni unyama mkubwa sawa kabisa na ule wa madaktari wasiojali amani na utulivu hujengwa ktk misingi gani.

Hii ndio maana tumesisitiza dialogue badala ya maguvu iwe upande wa madaktari au serikali japokuwa tunafahamu uwezo na nguvu ya serikali. Lakini busara na hekima inatakiwa kutumika badala ya Udikteta pamoja na kwamba waziri mkuu walisema LIWALO na LIWE!. Wafukuzeni kazi kama wamekataa kujiuzuru kuliko kujaribu kufanya mauaji. hamuwezi basi tudini ktk kiti myazungumze upya na iwe wazi kwa wananchi na bunge..

Kama Ulimboka alikuwa akituhumiwa na jambo ama kiongozi wa mgomo angefikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Kutofanya hivyo kuwaweka madaktari ktk hali ya wasiwasi wanapokuwa kazini, wengi wao inabidi wajifiche maana wameshiriki ktk mgomo ule... Hata mimi ningekuwa ktk nafasi yao nisingefiuka kazini maana sasa sii swala la madai bali usalama wangu..You never know what may happen..
 
Its so sad watu wanafurahia sana wakisikia mgomo umeanza au unaendelee! Why?

rais,mawaziri na wabunge hawawezi kugoma kwa kuwa ndio waliotufikisha hapa. kuwatukuza wanasiasa na kuwapuuza madaktari ni kuupuuza utu wetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom