Write your reply...Amini usiamini Ukiondoa viongozi wa juu wa serikali zote Tanzania bara na visiwani pamoja na familia zao ...tuliobakia sisi sote ni watumea wao ...haya mengine ni kujifariji tu
You are absolutely correct brother/sister!
Unajua nisichokifahamu mimi ni pale mtu ambae anaijua historia ya Unguja kinyume-kimbele na baadae anasema kuwa Mapinduzi yamekuja sio kwasababu ya udhalimu uliokuwa ukitendeka. Mwana-historia huyo huyo anafika hata kuuliza nani alikuwa akidhulumiwa enzi za Sultani? Nikisikia hivi huwa machozi yananitoka. Ukiwaoneshea kidole kwenye elimu watakupa hayo majina 2-3 ya akina Jumbe, Mwinyi, and so on.
Hivyo wana-historia hawa hawajui kuwa elimu Unguja ikiendeshwa kibaguzi na kikabila chini ya huyo Sultani wao? Hawajui kuwa waafrika waliokuwa wakiruhusiwa kuendelea kwenye secondary schools ilikuwa ni not more than 3% - yaani hii 3% ndio quarter ya waafrika kuingia kwenye secondary schools kwa Zanzibar nzima.
Hawajui kuwa ilikuwa unapomuandikisha mtoto wako shule anaulizwa kabila la mama na la baba? Kwanini wakiuliza makabila ya wazee ? – ili wamuweke mtoto kwenye quarter yake, kama ni ya 3%, 2%, 1%, etc. Hivyo hii haikuwa dhulma tosha yakufanya mapinduzi?
Hivyo leo Bara waambiwe Wachaga watakaoingia secondary schools kila mwaka itakuwa ni 2%, wahaya 3%, wazaramo na wandengereko 2%, etc - hivyo huu hautokuwa ni ubaguzi? Hivyo hii haitokuwa dhulma kwa watoto wakichaga, wakihaya, wakindengereko, etc wenye uwezo wa kusoma zaidi? Hii haitotosha kwa wachaga, wahaya na wandengereko kuwa ni sababu ya kufanya mapinduzi ili wapate haki sawa kwa wote?
Yanatokea mapinduzi tarehe 12 January, 1964, tayari yalikuwa yashatangazwa matokeo ya kuingia secondary school, lakini masomo bado kuanza. Karume akatoa amri kuwa examination results zipitiwe upya na nafasi za kuingia secondary school zitolewe according to the results. Idadi ya waafrika walioingia secondary school ilipanda ghafla na kuwa zaidi ya 3% allocated by the Sultan and his henchmen.
Cha ajaabu ni kuwa, wale waliokuwa wamefeli chini ya Sultani na wakapata nafasi baada ya mapinduzi wengi wao walipata 1st grade katika mitihani yao ya form 4 ya Cambridge na mmoja alikuwa jamaa mmoja maarufu akiitwa Balozi ambae aliimba ile nyimbo ya
ELINA NAKUPENDA (by Hijja Saleh).
Huyu Balozi alifeli chini ya Sultani na chini ya Karume ka-graduate kidedea with a first class grade from Cambridge Examination Board. Sio yeye tu na wengine tele. Sasa hapa ndio utaweza kuona vipi waafrika wakibinywa enzi za Sultani na bado historians wetu hawazioni dhulma hizi.
Sikatai pia kuwa sababu nyengine ya mapinduzi ilikuwa ni kuu-contain uislamu katika visiwa vya Zanzibar na East Africa. Hili hata bwana Lukuvi analikubali openly. Lakini hii imekuja kutokana na ukandamizaji wa waafika katika nyanza zote Visiwani. Kama ingelikuwa ni haki sawa kwa wote, basi hao wabaya wetu wasingeliweza kujipenyeza in order to fulfill their ulterior motivations na mapinduzi yasingelitokea.
Kwa upande mwengine hebu imagine kama Sultani angelikuwepo Visiwani mpaka leo, hali ingelikuwa vipi for the majority of the Africans? Sisemi kama sasa hivi chini ya SMZ kila kitu Visiwani ni sawa na kuwa we are all very happy, lakini at least kwenye elimu
hakuna anaeweza kusema kuwa kabila fulani wanabaguliwa na SMZ au wameekewa quarter fulani. And education my brothers and sisters is everything. Mnyime adui yako elimu, jua ushamshinda na ushamuuwa kabisa.
Ukeshapewa ufunguo wa elimu basi hata mambo mengine yawe magumu vipi, there will be a way out in your future. Ndio maana kabla nikasema I don’t care kama hivi sasa tunatawaliwa na Tanganyika au vipi. As long as hakuna pingamizi katika mambo ya elimu, as long as Wazanzibari wanajielimisha kwenye vyuo vikuu nchini na nje, then, there will be a way ya kuuangusha huu ukoloni mpya wa Tanganyika - ni ukoloni and we Zanzibaris are not happy about it at all. It just needs time. Mambo hayawezi kuendelea kuwa kama hivi yanavyokuenda sasa for good.
One day there will be again an independent People's Republic of Zanzibar, lakini kama tukiendelea kushikilia kuwa Sultani alikuwa bora basi hatutofika pahala, kwasababu maadui zetu wataendelea kututisha kuwa mnasikia mambo hayo – tokeni kwenye Muungano na visiwa vitarejea kwenye ukoloni.
Muungano utavunjika because our brothers on the Mainland don’t care about Zanzibar. Muungano utavunjika kutokana na matendo ya Bara. Wanafanya mipango yao bila ya kufikiria kuwa Zanzibar nayo ipo. Wao wanaona kuwa Tanzania ni Tanganyika tu na kuwa huu wetu sio Muungano wa nchi mbili zilizokuwa huru. Hawajali kabisa mustakbali wa Zanzibar. Ikiwa Muungano wa Soviet Republics ulikufa, sijui huu wetu wenye nyufa kila ukuta utadumu vipi milele?
Chakuchekesha ni kuwa huu Muungano wetu wa nchi mbili unatushinda na halafu tunataka Shirikisho za nchi zote za Africa Mashariki. Itawezekana vipi? Let’s manage our Union first in a better way and then talk of something else. Mwezi wapili huu marais wa EAC wanashindwa kukutana!
Wanafikiri Muungano au kuunda Shirikisho ni jambo rahisi kabisa? Zanzibar has sacrificed a lot mpaka tukafika hapa tulipofika leo. Zanzibar has surrendered her sovereignty to Mainland, who else is ready to do that? Mainlanders should bow down to us. We are a great people. Limelight yote ya nchi wanaichukuwa wao na sisi tupo gizani na hatusemi kitu.
Zanzibar outside the Sultan and outside the Union leo ingelikuwa ni pepo. Of course, wanatutisha kuwa tungelikuwa tunauwana kama Rwanda. Lakini ni bora kuuwana na baadae tukapata akili kama walivyopata akili hao wenzetu wa Rwanda.
Anyway, wacha niwachie hapo!
Kila la kheri kwa kila brother and sister katika sherehe hizi za Christmas za mwaka huu na Mola atuvushe na kila balaa katika mwaka ujao! AMEEN!