Mo endelea kuiga iga bidhaa za watu

Mo endelea kuiga iga bidhaa za watu

Kuna haja Mo kutafuta watu wa kumshauri kuhusu marketing ni sehemu ambayo kwa kiasi kikubwa anafeli sana,
Bidhaa zake nyingi anaiga yaan hana ubunifu kabisa, Bakhresa ana watu wazuri sana na ni wabunifu mno tofauti na Mo, Yeye kila siku anadurusu tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani wanamwonea tu...
Hakuna ambaye aja copy bhana..

Hizo sabuni za unga hio kampuni ni ya kwanza kugundua...?Watu wana copy mpaka majina wanabadilisha herufi moja tu.Ndo nashangaa kitu kidoogo nongwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna majukwaa mengi ya kuchangia, mfano chit-chat, mapenzi, ila kwenye mambo ya kisheria tuyazungumze kisheria!! Unajua ni gharama kiasi gani mtu anatumia kujenga jina la bidhaa yake? Yaani hata ujanja hajui mtu anabidhaa yake inaitwa kleesoft, wewe unatoa yako unaiita cleansoft!!! Na vifungashio vinataka kufanana??!!! Watu wa marketing wanajua vizuri!! Tena ingekuwa ulaya unaweza firisika kabisa!!
 
Huyu Mo mshenzi sana,niliagiza dogo sabuni ya kleesoft akapewa Mo cleansoft ilibidi nirudishe
Afu anazingua kweli, bidhaa zake zipo hoi sokoni kwanzia
Nyembe
Sabuni
Sembe,kila kitu anaiga afu cha kusikitisha zaidi haboreshi analipua tu

Kidogo kawadaka kwenye soda zake hapo ndio anapolia ugali wake tena sababu ya ujazo lakini ubora ni "0"
Kampuni tanzu ya METL Group inayotengeneza sabuni ya unga ya Mo Cleansoft imeshindwa katika shauri lililofunguliwa na Keds Tanzania Co. Ltd kwa kutengeneza na sabuni zinazoshabihiana na bidhaa yake ya Kleesoft. Tume ya ushindani (FCC) imesema METL imeiga jina na kuleta mfanano.

Source: Swahili times

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio unayechanganya mambo! Kuna kuiga huduma kama kwenye sekta ya bima, mawasiliano, na ma bank! Hiyo haina shida kwenye biashara kwani huibi haki ya mtu, kwani mpesa, ni tofauti na tigo pesa, huwezi lalamika, sasa huyu mo yeye anaenda mbalii zaidi hadi kwenye majina, na kuweka utofauti mdogo sana, na kufananisha hata vifungashio!! Mfano hiyo sabuni ya kleesoft yeye akaleta yake cleansoft!! Huo si uhuni? Ndio maana ameamliwa hiyo bidhaa iharibiwe!! Kwenye matangazo mfano ya radio mteja ataweza kutofautisha kati ya kleesoft na cleansoft? Huko kwingine mfano azam energy, naye mo energy, haina shida kwani ni majina mawili tofauti, na ndio maana hata bakhresa aliwashinda coca cola kipindi kile anaanzisha kinywaji chake cha azam cola kwani walitaka azuiwe kutumia neno COLA!!!
Kleesoft vs cleansoft. Kumbe yana fanana eee.

Ila umeona tofauti ya coca cola na azam cola.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasheria wake wamezembea kutetea trademark yake! Lengo la trademark ni kuonesha origin(source) not necessarily itofautishe bidhaa. Jina "Mo" Cleansoft liko wazi linaonesha source ya bidhaa. Kuna maamuzi ya mahakama yako wazi juu ya hilo.

Wale wengine watakuwa wame-rely on aspects of dilution and infringement based on resemblance ambazo zingepanguliwa na hoja ya uwezo wa hii trademark yao kuonesha source ya bidhaa yao. Sehemu ya jina hilo ambayo ni "Mo" ni maarufu sana kwa mteja kuchanganya source ya bidhaa. Haiwezekani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LAKINI MO ALIVYO MSHENZI ATAKUBALI KUZIONDOA HIZO BIDHAA,ILA ATAKACHOWAFANYA NI KAMA KWENYE SUKARI HATA KAMA EXPIRE DATE YAKE IMEFIKA ATATIA KWENYE KIFUNGASHIO KINGINE...ndio maana tunasema ni ngumu matajiri kuiona pepo wanachotufanya ni kutulisha sumu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohammed Dewji hata jina la "MO" ka-copy kwa MO Ibrahim,kwani kabla MO Ibrahim hakujikita sana kujiita MO Dewji ! Sema Wabongo wengi ni Bongolala hawana kumbukumbu kihivyo!

Baada ya kuona neno MO lina- sound vizuri kama "more" basi kila kitu kinacho- trend au ku-peak basi tegemea Mohammed Dewji ataki-copy kwa kuanza na MO!

Mo Chalk, Mo Chupi, Mo Fire ,Mo breath n.k
 
Mohammed Dewji hata jina la "MO" ka-copy kwa MO Ibrahim,kwani kabla MO Ibrahim hakujikita sana kujiita MO Dewji ! Sema Wabongo wengi ni Bongolala hawana kumbukumbu kihivyo!

Baada ya kuona neno MO lina- sound vizuri kama "more" basi kila kitu kinacho- trend au ku-peak basi tegemea Mohammed Dewji ataki-copy kwa kuanza na MO!

Mo Chalk, Mo Chupi, Mo Fire ,Mo breath n.k
MO Salah wa Liverpool kakopi kwa Mo fire
 
Back
Top Bottom