Mo Dewji ulikosea sana 'Kumsifu' vile hadharani Kocha Mgunda

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,176
Mwekezaji wa Simba SC Mo Dewji usichokijua pamoja na utajiri wako ni kuwa 90% ya Wajumbe wa Bodi ya Simba SC ni wapigaji watupu na wengi wao ni wasaliti kutokana na kutumika kwao kutoka upande wa pili.

Mo Dewji baada ya wewe kumsifia mno vile Kocha Mgunda na kuahidi kuwa ungekutana naye Ili mzungumze na ikiwezekana umpe yimu (Simba SC) moja kwa moja, hapa ndipo uliharibu.

Mo Dewji watu wanaokuzunguka ndani ya Simba SC hawataki Mgunda apewe timu moja kwa moja kama unavyotaka kwani wanajua Mgunda akiwa Kocha Mkuu wao hawatapata ile 10% yao na isitoshe Kocha Mgunda ni mzawa na mjanja (mtoto wa mjini) hivyo wanajua kuwa atawakatalia tu.

Hivyo basi Mo Dewji tambua ya kuwa hata matokeo ya jana (Simba SC kufungwa na Azam FC) ni sehemu ya mkakati wa kimafia na kihujuma kutoka kwa hao wana Simba SC (Wazee wa 10%) ili Kumharibia Kocha Mgunda na uondoe imani naye.

Na mchakato wa kumpata na kumleta Kocha Mkuu wa kigeni ufanyike na kama kawaida yao akija wao wapate (wale hiyo 10% yao), ambayo ndiyo inawaweka mjini pamoja na zile 10% wanazozipata kutoka kwa wachezaji mizigo wa kigeni na hata wa kizawa.

Mo Dewji kama kawaida yangu GENTAMYCINE bingwa wa kupata taarifa ngumu na za ndani kabisa ambazo kwa 99.9% huwa ni sahihi (kweli) ni kwamba, hata katika mechi ya Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar FC kama hakutokuwa na umakini mkubwa na kukabiliana na hawa mafia na wasaliti kuna uwezekano mkubwa Simba SC ikafungwa tena au kutoka sare/Suluhu Ili tu kuendelea kumharibia Kocha mzawa Mgunda kisha aje Kocha wa kigeni (hasa Mzungu) na ule utamaduni wao wa kula 10% uendelee na maisha yao yaendelee.

Kazi kwako tu sasa kuyafanyia kazi!
 
Gentamycin, kama tu hamuwezi kukubali kwamba kufungwa ni sehemu ya mchezo, mtaendelea kutafuna uchawi.

Kuna shida sana upande wa mashabiki upande wa hizi timu mbili. fahamu Azam pia anataka matokeo. Azam sio timu ya kubeza, ,ametoka kupoteza shirikisho, amepoteza kwenye ligi, so ameingia akiwa na ari zaidi ya kupata matokeo
 
Mwekezaji wa Simba SC Mo Dewji usichokijua pamoja na Utajiri wako ni kuwa 90% ya Wajumbe wa Bodi ya Simba SC ni Wapigaji watupu na wengi Wao ni Wasaliti kutokana na Kutumika Kwao kutoka upande wa Pili.


Kazi Kwako tu sasa kuyafanyia Kazi!!!

Umafia? He he he
 
Inawezekana Kuna huo 'umafia' unaosema lakini je, hao 'mamafia' ndio wanapanga kikosi?
Mechi ya Jana Mgunda amefeli kwenye uchaguzi wa kikosi na kupelekea kufeli kimbinu.
Kikosi Cha Simba ata kiwe kamili hakina uwezo wa kupata matokeo chanya Kwa Azam au Yanga alicho ongeza Mgunda ni hamasa tu. Kikosi ni chakawaida, ata kama waseme baada ya wiki tatu warudiane Simba anastahili afungwe.

Ivi we Una James Akaminko, Ndala, Sospeter Bajana, Migunamiguna kulia Kipre, kushoto Lyanga nje una Nado juu una Dube, Kola na Mbombo Unafungwa vipi na Simba!!
Mpira wa Tanzania unachupri nyingi.
 
Kazi imeanza
Screenshot_20221028-075534.jpg
 
Mwekezaji wa Simba SC Mo Dewji usichokijua pamoja na Utajiri wako ni kuwa 90% ya Wajumbe wa Bodi ya Simba SC ni Wapigaji watupu na wengi Wao ni Wasaliti kutokana na Kutumika Kwao kutoka upande wa Pili.

Mo Dewji baada ya Wewe Kumsifia mno vile Kocha Mgunda na Kuahidi kuwa ungekutana nae Ili mzungumze na ikiwezekana umpe Timu (Simba SC) moja kwa moja hapa ndipo Uliharibu.

Mo Dewji Watu wanaokuzunguka ndani ya Simba SC hawataki Mgunda apewe Timu moja kwa moja kama unavyotaka kwani wanajua Mgunda akiwa Kocha Mkuu Wao hawatapata ile 10% yao na isitoshe Kocha Mgunda ni Mzawa na Mjanja (Mtoto wa Mjini) hivyo wanajua kuwa atawakatalia tu.

Hivyo basi Mo Dewji tambua ya kuwa hata Matokeo ya Jana (Simba SC Kufungwa na Azam FC) ni sehemu ya Mkakati wa Kimafia na Kihujuma kutoka kwa hao wana Simba SC (Wazee wa 10%) Ili Kumharibia Kocha Mgunda na uondoe Imani nae na Mchakato wa kumpata na kumleta Kocha Mkuu wa Kigeni ufanyike na kama Kawaida yao akija Wao wapate (wale hiyo 10% yao) ambayo ndiyo inawaweka Mjini pamoja na zile 10% wanazozipata kutoka kwa Wachezaji Mizigo wa Kigeni na hata wa Kizawa.

Mo Dewji kama Kawaida yangu GENTAMYCINE Bingwa wa kupata Taarifa Ngumu na za Ndani kabisa ambazo kwa 99.9% huwa ni sahihi ( kweli ) ni kwamba hata katika Mechi ya Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar FC kama hakutokuwa na Umakini mkubwa na Kukabiliana na hawa Mafia na Wasaliti kuna Uwezekano mkubwa Simba SC ikafungwa tena au kutoka Sare / Suluhu Ili tu kuendelea Kumharibia Kocha Mzawa Mgunda kisha aje Kocha wa Kigeni (hasa Mzungu) na ule Utamaduni Wao wa Kula 10% uendelee na Maisha yao yaendelee.

Kazi Kwako tu sasa kuyafanyia Kazi!!!
Mpira ni mchezo wa hadharani, Simba imezidiwa quality wote tumeona.

Pili kocha mzungu akiletwa pesa yake analipwa kwenye account hiyo biashara ya 10% hapo.

Mtendaji mkuu CEO wa Simba ni mtu wa Mo Dewji, Try again ni mtu wa Mo Dewji Sasa hapo swala la 10% linatoka wapi? Kwahiyo Barbara anapiga 10%?

Tatu huyo muwekezaji aache ujanjaujanja ziko wapi billion 20?
 
Mgunda ni kocha mzuri ila ushikaji ndio utamdondosha, Boko, Nyoni na Mkude wanapewa nafasi zaidi kishikaji, jana upande wa Nyoni ulikuwa kama shimo mipira inapitishwa, una beki 2 wawili , Israh Mwenda na Kapombe pia kapona tayari, kwa nini umtumie Nyoni ili kumtafutia game time tu.

Unamuingiza Boko, wakati nje una Sakho, unaowezo wa kumtumia Phiri 9, na Sakho 10, ushikaji kwenye kazi utaishi kuleta matatizo tu.
 
Nini kifanyike mtoa mada. Je, Matola mnamhitaji tena?
Matala ananifanya niwaze mara mbili mbili pale simba nini kinamuacha kila kocha akiondo bila shaka kikosi cha jana alipanga yeye 100% yaani toka siku ile alipotofautiana na pablo kuhusu substitution ya Pascal wawa nikajua jamaa ni kweli huwa ana wategeshea mitego makocha waharibu ili abaki yeye bila kuondoka matola simba itafufukuza sana makocha yule jamaa ni kirusi kwenye benchi la ufundi
 
Gentamycin, kama tu hamuwezi kukubali kwamba kufungwa ni sehemu ya mchezo, mtaendelea kutafuna uchawi.

Kuna shida sana upande wa mashabiki upande wa hizi timu mbili. fahamu Azam pia anataka matokeo. Azam sio timu ya kubeza, ,ametoka kupoteza shirikisho, amepoteza kwenye ligi, so ameingia akiwa na ari zaidi ya kupata matokeo
Ndio maana kauli mbiu ya mpira wetu inasema soka letu kivyetu vyetu hyo tu inatosha kututofautisha na mashabiki wa team zengine.
 
Back
Top Bottom