Mnyoo wapatikana kwenye ubongo wa Binadamu huko Australia

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,539
Mwanamke mmoja nchini Australia amekutwa na mnyoo akiwa hai, mwenye urefu wa sentimeta 8, kwenye ubongo wake wa mbele.

Mnyoo huyo aina ya Ophidascaris robertsi mwenye umbo la kamba, kwa kawaida hupatikana kwenye nyoka wasio na sumu, wanaopatikana zaidi Australia, huku ikidhaniwa kuwa huenda mwanamke huyo alipata mnyoo huo, wakati akikusanya nyasi, karibu na mahali alipokuwa akiishi.

Kufuatia sintofahamu hiyo, watafiti wamesema kuwa kisa hicho kinaashiria kuwa, kuna hatari ya ongezeko la magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
FB_IMG_1693468650331.jpg
 
Sio nguruwe tu hata nyama ya kondoo Ecchinococcus granulosus (echinococcosis). Chamsingi ni kuhakikisha nyama inapikwa vzr inaiva ndio iliwe.

Umesahau kuna Taenia saginata napatikana kwenye nyama ya ngombe ambayo ni infected.
Ila sijui kwanini nguruwe nimetokea kutokumpenda kabisa esp nilipojua anaingia hedhi kama binadamu. Mpaka harufu ya nyama yake siipendi. Labda niwe na njaa sana ndo nitamla.
 
Ila sijui kwanini nguruwe nimetokea kutokumpenda kabisa esp nilipojua anaingia hedhi kama binadamu. Mpaka harufu ya nyama yake siipendi. Labda niwe na njaa sana ndo nitamla.

Acha kudanganyika nguruwe haingii hedhi hizo ni stori za wafia dini wapumbafu wanao penda kupotosha kwa manufaa yao,katika wanyama wote duniani kiumbe mwenye menstrual cycle ya kuvuja damu ni binadamu pekee,wanyama wote waliobaki wana kitu kinaitwa eostrous cycle ,baada yai kutokurutibishwa huwa linakuwa dissolved mwilini wala hakuna damu ya period kama mwanadamu.

Jielimishe,kataa wahuni.
 
Ok sasa huyu mnyoo huko ubongoni anakula nini?

Minyoo huwa na site wanazo pendelea kuishi ndani ya host,wengine kwenye misuli(skeretal m.),wengine kwenye utumbo,wengine kwenye ini(liverflukes),wengine kwenye mapafu na wengine kwenye ubongo.

Parasites wote wanatumia nutrients za host huku wakimletea madhara host husika.
 
ni vipimo tu havipo, ila huku africa nafikiri kuna vyuma vina minyoo hadi mita 30.

uhakika tena kwa mazingira yetu haya ya kunyakunya hovyo,kuogelea hovyo kwenye madimbwi,kula kula hovyo vyakula ambavyo si safi na salama.

Ndio mana inashauriwa kunywa dawa za minyoo(deworming) angalau mara mbili kwa mwaka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom