Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni: Katika Mgomo wa wafanyabiashara, kosa la Mwigulu Nchemba ni lipi?

Wa chini wanatekeleza wajibu wao Kwa mujibu wa sheria na kanuni,kama kuna Changamoto zingine pelekeni Kwa utatuzi au karipoti.kwa vyombo.

Huo uchumi ungeshakuwa umekufa kitambo ndio kwanza unapata Sasa sijui mnaongea nini hasa..

Rais kamuondoa Makala Kwa sababu za kushindwa kusimamia Changamoto kwenye Mkoa wake ,hiyo sio kazi ya Mwigulu.
Huyo mwigulu mbona mara nyingi hukutana na wafanyabiashara na kuongea akitoka hapo habadiliki kitu ni kama zile tozo zake za simu zilizoleta hasara na watu kuacha kutumia sana hzo njia especially in digital error
 
KERO ni nyingi sana, Tena huyu anamchafulia mama CV ya uongozi wake kabisa, imagine wafanyabiashara wakigoma nchi nzima siitaonekana mama ndio kafeli kabisa na uchumi kufa.
Hafu wafanyabiashara wametoa hoja zenye mashiko zikifanyiwa kazi zitaondoa urasimu na kuweka mazingira mazuri kiuchumi
Mama hafanyii kazi majungu,angekuwa anafanyia kazi majungu au chuki zenu binafsi wafuatao wangekuwa hawapo ofisi Ili awafurahishe nyie..

Mwigulu
January
Nape
Kijaji,
Mbarawa,
Bashe
 
La prove kuwa failure Kwa lipi hasa?
Hayo masuala ya upuuzi wa TRA Wala hayamhusu Waziri unless hamuelewi kazi za Waziri.

Hiki anachoongea Chalamila ndio kazi hasa ya Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa TRA ,Takukutu na Polisi sio issue ya Mwigulu..

Angekuwa ame prove failure.kama.uchumi ungekuwa unaanguka nk ila sio blaa blaa zenu Kwa sababu za chuki za Kisiasa..

Kazi za waziri ni zipi na wizara yake?
 
Huyo mwigulu mbona mara nyingi hukutana na wafanyabiashara na kuongea akitoka hapo habadiliki kitu ni kama zile tozo zake za simu zilizoleta hasara na watu kuacha kutumia sana hzo njia especially in digital error
Kwanza hawezi badili sheria ya Bunge,hili amewahi lizungumza mara nyingi tuu,kama jambo Hilo au sheria ilipitishwa na Ngazi zote haliwi la Mwigulu Bali la Serikali yote Ili libadiloke ni lazima Rais aingilie kati..

Ujue watu wengi hamjielewinna sijui nyie mnafanya kazi zipi, Mwigulu hatungia sheria Wala kupendekeza sheria ,hayo yote hufanywa na Wataalamu wa Fedha, uchumi na Kodi baada ya kujiridhisha..

Waziri anaenda ku act kama.msemaji na mjenga hoja ya hicho kilichopendekwzwa na anaanzia kwenye Baraza la Mawaziri ndio linaenda Bungeni,wote hao wakipitisha na Rais kusaini haliwi suala la Mwigulu,sheria inaipa Wizara mamlaka ya kutunguia kanuni na miongozo kwenye sheria mama.

Kwa hiyo Mwigulu hawezi kulaumiwa kwenye sheria za Bunge,mara ooh utitiri wa Kodi Sasa hizo ni Kodi za Mwigulu au za Serikali? 🤣🤣🤣
 
Kazi za waziri ni zipi na wizara yake?
Kazi kubwa ya Wizara ni kutunga na kusimamia sera na miongozo ila utekelezaji hufanyika kwingine na watu wengine,Sasa hao watu wakiboronga Waziri hatakiwi kulaumiwa Bali walaumiwe wao na kama hiyo sheria ndio mbaya Bado sio swala la Waziri Bali ni la Serikali,kumbuka Waziri unaweza kuwa umesomea Kiswahili na ukawa Waziri wa sheria Sasa msidhani kwamba ni kazi ya Waziri Kupitia vifungu vya sheria ,hapana..

Shida ambayo Mwigulu Huwa anapata ni kwamba yeye amesoma uchumi Yuko kwenye field Sasa unakuta mtu hata hajasomea hiyo fani anapayuka tuu Sasa mtu anapata jazba anamjibu vibaya..

Yaani ukute Mimi Mhandisi nime design kitu vizuri kabisa harafu layman wa Kiswahili ananikosoa as if anajua hapo unakasirika unamuona mpuuzi mmja hivi ndio maana mnaitwa waganga harafu mnachukia 😂😂
 
Mtu ana PhD ya business administration huku hajawahi kuwa na biashara yoyote hajui hata changamoto za watu then una mpa wizara aongoze matokeo yake ni Kuja na theory zinazofeli.
Kuna muongeaji mmoja alisema wastaafu wa TRA hufungua frame kariakoo mwisho hushindwa biashara kabisa na kula corner, Sasa wakute wanakomoa wafanyabiashara
😂😂😂😂😂
 
Unamjua mfanya biashara kwa jina la Ramadhan Nhtuzwe...🤔
Huyu jamaa alikua mfanya biashara hapo kariakoo, na kwakifupi alikamatiwa mizigo yake na TRA.
Jamaa amefilisika na juzi nikimuona wilayani Urambo mkoa wa Tabora, amefungua duka la kawaida na anauza bidhaa za nyumbani kwa rejareja kama duka la mangi.
Nimemsikia Majaliwa akimtaja kuwa wanalifanyia kazi.
Magufuli alishindwa kumsaidia Majaliwa ataweza?
Kwanini huyo Muha ameteswa kiasi hicho?
 
Wakuu Salam,

Naomba nitangaze maslah, mimi ni mfanyabiashara, nipo Kariakoo, nje ya kariakoo na mkoa wa Pwani.

Malalamiko yetu wafanyabiashara mengi ni justifiable.. lakini hili la kumlaumu Mwigulu Nchemba bila supporting evidence is ungrounded.

Kuna watu wanatumia udhaifu wa migogoro ya sheria zilizopo kumgandamiza bila sababu.

Mfano.

1. Hoja ya fine ya kutokutoa EFD recept sio ya leo, na hii ilipingwa sana na aliekuwa mbunge wa Muleba Anna Tibaijuka, nilishangaa saana yale mapendekezo, kama kawaida ya bunge letu.. papatu papatu hoja ikapita ikawa sheria, Kipindi hicho Mwigulu ni Wazir wa mambo ya ndani.

2. Hoja ya ushuru wa malori, Ndugu Chuki anaweza kuwa ana issues personal na Mwigulu na siwez kuwaingilia , ila kodi ya 2.7M sio kubwa kama anavyodai, kumbuka kubeba tonneau 10 had mwanza ni zaid ya 1.5M na hiyo ni non negotiable.... kutaka hiyo gharama iingizwe kwenye diesel ni ku shift tax burden to non beneficiaries, ambayo ni unfair taxing.

3. Hoja za registration of warehouse sio kitu kipya na wengi tumesajili nikiwemo, hoja za umiliki ni jambo jingine, labda tuseme issue ya With holding Tax ndio haijakaa Sawa, lakini kulalamika kwamba tusisajili sio Sawa kabisa.
Kwenye ethical business ni lazima usajili store na ulipie usimamiz wake, ikiwa na vigezo vyote.... hii ni excuse ambayo kumlaumu nayo Mwigulu ni ku choose easy victim.

4. Hoja za task force zilikuwepo toka kipind cha mwendazake... kwamba tunasumbuliwa hili ni kweli na ni sualq la kuweka utaratibu tu wa namna ya ku control, ambayo sikuona sabab ya kumzodoa mwamba vile.

5.Utitiri wa kodi kwenye biashara na mamlaka nyingi zinazosimamia jambo moja ni suala la kurith na Mwigulu sidhan kama ni wa kulaumiwa 100% , issue hapo ni CCM kuweka na kuunda hizi taasisi kutafutia washkaj wao ulaji.
Kuna kila sabab ya kuunganisha taasisi nyingi sana ili kuondoa usumbufu.

Ni hayo tu... tumuhukumu Mwigulu kwa mengine lakini sio moja kwa moja kwa baadhi ya sheria ambazo amezikuta.
Nonsense
 
Mwigulu, mchengerwa, na huyu Kijaji ndio mawaziri wanaongozwa kuchukiwa ndani ya Bunge mpaka nje ya Bunge

Kwanza Wana majibu ya shombo Sana

Pili hata ukifanya nao mkutano wa mambo serious hakuna kinachotokea
Mchengerwa una mwonea.
Jamaa ni msikivu sana anasikiliza hata watu wa chini kabisa.
Mchengerwa ni mbunifu na mtendaji mzuri, kote alikopita alianza kuzisuka wizara vizuri sana.
Bado sijamsikia wizara ya utalii labda bado anajipanga
 
Mchengerwa una mwonea.
Jamaa ni msikivu sana anasikiliza hata watu wa chini kabisa.
Mchengerwa ni mbunifu na mtendaji mzuri, kote alikopita alianza kuzisuka wizara vizuri sana.
Bado sijamsikia wizara ya utalii labda bado anajipanga


Ujajua show zake kwa wabunge wenzake

Ni balaa

Hao watatu ndio mawaziri ambao hata Mbunge akiwa na shida asumbuki kupiga simu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom