Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Mnamlalamikia Mnyika maji kwani yeye slikuwa mbunge tangu uhuru? huyo Keenja na wenzake waliwafanyia nn miaka 50 iweje yeye miaka 5 kwanza si huku kimara kila wiki yanatoka na leo pia yanatoka.
 
Toka lini maji yakawa kipaumbele?

Vipaumbele ni ushoga na vimini vya mademu.
 
habari za uhakika CCM kata ya Ubungo Kibangu ilipeleka wajumbe kwenye kikao kujadili habari za Maji Ubungo na kukubaliana kutumia maji kama agenda ya uchaguzi mwaka kesho kumdhibiti Mbunge John Mnyika.

Makao makuu ya Idara ya maji kwa eneo na Ubungo ni Tabata Maji. Afisa Mtendaji mkuu wa pale Tabata ni Mama mmoja ambaye anelezwa kuwa mfuasi wa CCM. Ana maelekezo kukata maji Ubungo Kibangu kujenga taswira ya John Mnyika kushindwa kazi ya kutetea wananchi.

Mkatati mwingine wa CCM ni kudai kwamba wanao uwezo kuchangishana fedha hata kama pangekuwa na ulazima wa kujenga tanki kubwa eneo hili, lakini Mnyika haonekani. Yuko bize na mambo yake tu wakati wananchi wanateseka. Maeneo mengi ya Dar es Salaam maji yanatoka, lakini eneo la Ubungo Kibangu halina Maji kwa wiki takribani tatu sasa.

Jumuisho ni kwamba Ukame wa maji Ubungo Kibangu ni agenda ya CCM kikishirikiana na Meneji mmoja mwanamama wa idara ya Maji Tabata.

HAYA. CHADEMA MPO? WENZUNU KETE INAYOTUMIWA NDO HIYO...MENEJA WA DAWASCO TABATA NA LAWAMA YA MNYIKA KUTOKUFANYA MIKUTANO AU KUONGEA NA WANA-UBUNGO.

TAARIFA YA AWALI:

ni nchi gani duniani shirika la maji la kiserikali litakausha mabomba ya maji kwa wiki mbili na watu wakaweza kushi bila maji kwa wiki mbili? na bado mtaani pakawa kimyaaaaaa....kama hakuna tatizo.

hivi huu si ujinga kweli?
 
kutokana na mh mnyika kutingwa na majukumu ya kibunge bunge la katiba,ina maana hilo eneo halina diwani???? au lina diwani lakini boya???
 
Moderators tunaomba mtuondolee huu uchafu.
 
Back
Top Bottom