Mndengereko
JF-Expert Member
- Mar 24, 2011
- 7,319
- 3,434
Unapoangalia Geography ya Ubungo na makazi ya watu, kwa kweli hata serikali iwe ya Kichina siyo rahisi kumpatia kila mtu maji labda kuwe na kituo maalum cha kutoa maji ambapo mwenye shida ataenda kuchota nakupeleka nyumbani kwake. Jamani ile milima ya Kimara, mbezi, bonyoko, malamba mawili, msakuzi na kwingineko maji yatapandishwa na nini? Ujenzi wenyewe hauna Plan ili serikali iweze kusambaza maji kirahisi. Kila mtu kajenga alipotaka na anataka maji ya bomba yamfikie. Hii katika hali halisi isiyo ya Kisiasa naona haiwezekani? Mimi naona serikali inajitahidi kupeleka penye Plani kama Ubungo NHC, Mabibo, Sinza, Mlimani City na Maeneo ya chuo. Ila huko kwingine mlimani mtafute njia mbadala serikali iwasadie wataalaam.
hujaambiwa mbezi,kimara wala malamba mwaili ni ubungo na pale ofisi za maji zipo ubungo maji iweje watu wakose maji??,kama walivyochangia wenzangu tatizo ni uoga na ukimya wetu wa tanzania ndo kinachotumaliza nauli zinapanda watu kimya ukirudi usiku mbezi ukipanda gari ubungo unaambiwa mbezi 500 na abiria tupo kimya ukisema uanzishe move ya kusema 500 sio nauli halalai iliyowekwa na sumatra abiria wenzako wanakushambulia wanakwambia eti ungetaka singepanda ungesubiria la 400,alfu kesho kutwa yake sumatra wakipandisha tunakuja kulalamika tena.,kwa style hii tutaendelea kuonewa mpk tunakufa.