MODs please delete hii thread, imekaa kizushi sana, no proof, no mashiko, nothing, ngoja ni-Report abuse
Sasa mbona umekuja juu? tulia watu waandike uone jinsi kijana wenu alivyo nae fisadi, niliisha wahi kusema humu ndani hakuna mtu msafi CDM hata mmoja, yataanza kujionyesha kwa mmoja baada ya mwingine, haya ya mnyika hayo sasa
Huu ni mchezo wa kitoto. Mpumbavu pekee ndiye anaweza kuamini kauli hizi. Na hii ndiyo style ya mapacha 3/mafisadi 3 kuchafua watu wengiiiiiiiii ili wapate nafuu. Ujinga wao ni kwamba nafuu wanayotaka si kuonekana wasafi, bali kwamba sio wachafu peke yao. Wanadhani hiyo ni falsafa ya kuwasaidia, kumbe ni fallacy ya kuwaangamiza. Kupata mil. 90 huo ni mkopo ambao wabunge wote wamepewa na watalazimika kuulipa. Pia hakuna ushahidi kuwa kila mbunge (hasa Mnyika) aliuchukua kwa kuwa ni hiyari ya mbunge. Hizo fedha nyingine pia hazina ushahidi, benki haitajwi (itaje ili watu wafuatilie), na sababu inayoeoelezwa haikubaliani na conclusion, kwa kuwa si kazi ya mbunge kutoa hiyo kazi mnayodai. Ungesema, ni mkurugenzi (wa serikali ya CCM au meya (wa CCM) tungekuelewa.
Sasa unataka tuanze kuamini JF ni ya Chadema. Hii thread haina matatizo yoyote na kama MODs wataifuta tutajiuliza maswali mengi. Mbona tumejadili habari nyingi sana zenye mwelekeo huu kwa viongozi wengine hasa wa CCM?
Kumbukeni JF ni jukwaa la watu wenye maoni na milengo tofauti. Mnyika mwenyewe hajakanusha iweje wengine mumsemehe?
Sasa naanza kuelewa kwanini watawala huwa wanaangamiza vyombo vya habari vinavyowapinga, hata wewe ungekuwa mtawala si ajabu ungefanya hivyo hivyo!
Mleta hoja hakuandika kama ni tetesi, na tetesi si tuhuma za kuchafua watu. Tunachotaka humu ni ushahidi au facts zinazoweza kutusaidia kupata ukweli. Kipindi cha daladala huwezo kukifuatilia kupata ukweli. labda kama wale wanaozungumza wanafahamika, wanahojiwa kwa undani ili kuthibitisha madai yao, pia akili ya mwandishi mwenyewe kutambua uwezekano wa tuhuma yenyewe. Hata awe Makamba, januari, ngeleja, tutadai hayo ili kila mtu apate haki yake
</p>Jamani wana JF!</p>
<p>Ndio maana JF inaonekana ni CDM kwa kupinga kila kinachoibuliwa against CDM na kuunga mkono kila kinachohusu ccm, mngeambiwa J. Makamba kapewa hela na makampuni ya madini kusafirisha udongo wenye dhahabu nje ya nchi naamini mngeendelea kudodosa na kusaka ukweli na sio kumjibia kuwa hiyo ina mhusu waziri wa madini kama mnavyomjibia Mnyika sasahivi. Ingawa habari hiyo ni tetesi lakini source imetajwa kipindi cha daldala ingawa ushahidi zaidi katika hilo unahitajika na pia sio lazima kila tuhuma ijibiwe lakini ukimya pia unaleta hisia za kuwepo kwa viji chembechembe vya ukweli lakini pia watu huchokoza ili wapate kitu flani ndani yake. Tuvumiliane jamani tunapotofautiana.
Juzi nikiwa natizama kipindi cha daladala kinachorushwa na itv kila siku saa moja jioni.kuna tetesi mh. J.mnyika umechukua ela kutoka kwa magari ya maji taka ili yaendelee kumwaga maji taka hayo katika mabwawa ya kiwanda cha urafiki yaliyopo mabibo.je tuhuma hizi zina ukweli?tujulishe wapiga kura wako wa mabibo.
Kijana ameingia kwa kasi sana kukamata mshiko, nasikia siku alipopewa ile cheki ya Tshs 90m alichanganyikiwa akaanza kutetemeka , kwani hakuamini kabisa kama angeweza kupata hela kama hizo
Hizi ni habari za ndani kabisa na za uhakika, na tena huyu dogo kwenye akaunti yake ameingiziwa Tshs 280m kwenye benki fulani, muulizeni amepewa na nani ? asije kuwa anatumiwa na mapacha 3
Sasa mbona umekuja juu? tulia watu waandike uone jinsi kijana wenu alivyo nae fisadi, niliisha wahi kusema humu ndani hakuna mtu msafi CDM hata mmoja, yataanza kujionyesha kwa mmoja baada ya mwingine, haya ya mnyika hayo sasa
Najua utatumia nguvu nyingi sana kum defend ila ukweli ndio huo, kijana nae ni fisadi
Juzi nikiwa natizama kipindi cha daladala kinachorushwa na itv kila siku saa moja jioni.kuna tetesi mh. J.mnyika umechukua ela kutoka kwa magari ya maji taka ili yaendelee kumwaga maji taka hayo katika mabwawa ya kiwanda cha urafiki yaliyopo mabibo.je tuhuma hizi zina ukweli?tujulishe wapiga kura wako wa mabibo.
Hizi ni habari za ndani kabisa na za uhakika, na tena huyu dogo kwenye akaunti yake ameingiziwa Tshs 280m kwenye benki fulani, muulizeni amepewa na nani ? asije kuwa anatumiwa na mapacha 3
Kwanini tumuulize yeye wakati unayesema hayo ni wewe?
Porojo za namna hii ni hatari kwa ustawi wa JF.Tatizo ni kwamba mods wetu wako bize na pilau la Pasaka.Kuachia upuuzi wa aina hii kunaweza kuigharimu JF pindi mhusika akidai amekashifiwa.Kama mnaotoa tuhuma mna hakika na mnachosema,kwanini basi msiweke wazi uthibitisho mlionao?
Hakuna ukweli wowote kuu ya hili hata kwa kuliangalia kwa haraka Mbunge ana mamlaka gani ndani ya jiji Kama sio Manispaa wakiongozwa na Mkirugenzi wa Manispaa husika?.Tuwekee jina la bank aliyowekewa,acount number na ilitoka kwa nani pia na kwa sbb gani hapo tutakuelewa tofauti na hayo utakuwa umetumwa na chama cha MAFISADI a.k.a magamba kuja kuchagua cv za watu.Myika Kama unapita humu embu fafanua juu ya tuhuma hizi pls
Cant comment on siasa za majitaka kuhusu majiataka yahee:spy: