Mnyika: Sina mpango wa kuhama CHADEMA

Huna namba ya Mhariri wa mwananchi on line?
zamani tulikua hatuombi namba za mhariri... Mnyika alikua anapost hadi facebook

Leo mnatutuma twende kwa mhariri... kwikwikwikwi
 
Mnyika anawezatoka CHADEMA, sawa. Lakini anakwenda wapi? Ndilo swali la msingi. Kwa hatua aliyofikia akiamua kutoka CHADEMA basi awe ameamua kuachana kabisa na siasa za vyama. Huwezi kufika kiwango kikubwa hivyo halafu ufikirie kuhamia kwa wacheza bao wanaokusubiri kama kete waitumie kujinasibu na kupigia propaganda tu. Ni chama gani kingine kinachoendana na fikra na ujumbe wa Mnyika? CCM? ACT? Well...

Hadi leo nasikitika jinsi mtu wa kiwango cha Dr. Slaa, baada ya kuamua kuondoka CHADEMA, alivyobukia kwenye jukwaa la CCM/dola na kuongea hadharani maneno yasiyokuwa na busara hadi kujisahau na kutelezea kwenye kashfa ya mkulu na nyumba za dola! Kama vile haijui vizuri Tanzania.

Nashukuru kwamba hatimaye aliweza kutuliza akili mapema na kuamua sasa basi. Kuna viwango ukifikia tunaita: point of no return! Hapo tena si suala la kuangalia shetani yupi ana afadhali ujiunge naye; NO! Ni kutafuta mwelekeo tofauti kabisa wa maisha.
 
Anazichukuliaje habari za gazeti la RAIA MWEMA ambalo taarifa za kiuchunguzi zinadokeza kwamba wiki hii wameandaa uzushi mwingine kuhusiana na mnyika huyohuyo ?
 
Baada ya kuenea kwa uvumi kuwa Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika anataka kuachana na chama hicho, kiongozi huyo ameibuka na kukanusha akisema: “Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa kuhama.”

Mnyika alisema hayo jana alipopigiwa simu ili azungumzie taarifa hizo. Mbunge huyo wa Kibamba alisisitiza kwamba huo ni uzushi.

Habari za kujiuzulu kwa Mnyika zilianza kusambaa katika vyombo vya habari kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kufukuzwa uanachama.

Wakati huo, uvumi ulienea kwenye mitando kwamba amejivua nyadhifa zake zote na kwamba ameshakabidhi barua yake kwa katibu mkuu wakati huo, Dk Willibrod Slaa.

Habari hizo zilijirudia mara baada ya Dk Slaa kutangaza kujivua nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho huku akipinga hatua yake ya kumtangaza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais.

Licha ya kushindwa kujitokeza hadharani kukanusha wala kuthibitisha tetesi hizo, Mnyika alionekana kuendelea na shughuli zake za kisiasa kama kawaida.

Uvumi wa tatu uliibuka mwishoni mwa wiki iliyopita safari hii ilidaiwa kueleza msimamo wake kuhusu Lowassa kupitishwa na Chadema na kisha Ukawa kuwania urais ikidaiwa kwamba anataka kiongozi huyo ahojiwe na kuchukuliwa hatua kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya Richmond.

Habari hiyo iliyoibua hisia za wengi ilimnukuu Mnyika akisema: “Msimamo wangu haujabadilika kama ambavyo niliwahi kusema nikiwa mkurugenzi wa vijana wa Chadema tarehe 25 Februari 2008 na kipindi chote nikiwa Mbunge wa Ubungo…. Hivyo nategemea kuanzishwa kwa Mahakama ya Mafisadi Lowassa ndiye atakuwa wa kwanza. Siwezi kusaliti msimamo wangu bora nipoteze ubunge wangu.”

Katika mwendelezo wake, baadaye uvumi mwingine uliibuka kwamba baadhi ya viongozi wa chama hicho walionekana nyumbani kwa Mnyika wakimsihi asichukue uamuzi huo.

Hata hivyo, hakuna kiongozi yeyote wa Chadema aliyewahi kuzungumzia suala hilo kabla ya hivi karibuni, Ofisa Habari Mwandamizi wa Chadema, Tumaini Makene kutoa taarifa ya kukanusha akisema huo ni mradi wa kutengeneza uongo unaofadhiliwa na watu kwa ajili ya kukisumbua chama na Watanzania akisema wakati habari hizo zinaenezwa, Mnyika alikuwa akifanya shughuli za chama

Source.. MPEKUZI BLOG
 
Lazima kaombwa abakie na posho ndefu juu. Si angesema siku hiyo hiyo au kesho yake kukanusha...mmmmmm
 
Badala ya kuchukua hatua kuhusu hawa DED ambao sasa ni makada wao wanakazania tu na mkutano wa CCM
Ina maana hawajui kama hawa DED ndiyo wasimamizi wa chaguzi zinazokuja?
Hiki chama bure kabisa kwa kweli
Wachukue hatua gani mkuu! Maana hawana uwezo wa kutengua uteuzi wao.
 
Nibora yako mkuu
 
Baada ya kuenea kwa uvumi kuwa Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika anataka kuachana na chama hicho, kiongozi huyo ameibuka na kukanusha akisema: “Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa kuhama.”

Mnyika alisema hayo jana alipopigiwa simu ili azungumzie taarifa hizo. Mbunge huyo wa Kibamba alisisitiza kwamba huo ni uzushi.

Habari za kujiuzulu kwa Mnyika zilianza kusambaa katika vyombo vya habari kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kufukuzwa uanachama.

Wakati huo, uvumi ulienea kwenye mitando kwamba amejivua nyadhifa zake zote na kwamba ameshakabidhi barua yake kwa katibu mkuu wakati huo, Dk Willibrod Slaa.

Habari hizo zilijirudia mara baada ya Dk Slaa kutangaza kujivua nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho huku akipinga hatua yake ya kumtangaza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais.

Licha ya kushindwa kujitokeza hadharani kukanusha wala kuthibitisha tetesi hizo, Mnyika alionekana kuendelea na shughuli zake za kisiasa kama kawaida.

Uvumi wa tatu uliibuka mwishoni mwa wiki iliyopita safari hii ilidaiwa kueleza msimamo wake kuhusu Lowassa kupitishwa na Chadema na kisha Ukawa kuwania urais ikidaiwa kwamba anataka kiongozi huyo ahojiwe na kuchukuliwa hatua kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya Richmond.

Habari hiyo iliyoibua hisia za wengi ilimnukuu Mnyika akisema: “Msimamo wangu haujabadilika kama ambavyo niliwahi kusema nikiwa mkurugenzi wa vijana wa Chadema tarehe 25 Februari 2008 na kipindi chote nikiwa Mbunge wa Ubungo…. Hivyo nategemea kuanzishwa kwa Mahakama ya Mafisadi Lowassa ndiye atakuwa wa kwanza. Siwezi kusaliti msimamo wangu bora nipoteze ubunge wangu.”

Katika mwendelezo wake, baadaye uvumi mwingine uliibuka kwamba baadhi ya viongozi wa chama hicho walionekana nyumbani kwa Mnyika wakimsihi asichukue uamuzi huo.

Hata hivyo, hakuna kiongozi yeyote wa Chadema aliyewahi kuzungumzia suala hilo kabla ya hivi karibuni, Ofisa Habari Mwandamizi wa Chadema, Tumaini Makene kutoa taarifa ya kukanusha akisema huo ni mradi wa kutengeneza uongo unaofadhiliwa na watu kwa ajili ya kukisumbua chama na Watanzania akisema wakati habari hizo zinaenezwa, Mnyika alikuwa akifanya shughuli za chama.
 
Wachukue hatua gani mkuu! Maana hawana uwezo wa kutengua uteuzi wao.
Waende Mahakamani kama wasimamizi wa uchaguzi sasa ni makada wa CCM!Madai yao kuwa chaguzi yyt kuanzia sasa haitakuwa HURU wala ya HAKI

Mahakama inaweza ilazimisha serikali iweke uringo sawa wa haki ktk chaguzi,we call it check and balance

Lkn wenzangu wao priority yao sasa ni kuzuia mkutano wa CCM Dodoma
 
Kuna jamaa hapa jamvini ametumia nguvu nyingi kutuaaminisha ana habari za ndani za Mnyika kuhamia CCM
Bila soni wala tahayuri litakuja na hadithi nyingine ya kutunga
 
Hata Dr. Slaa na Prof. Lipumba hawakuhama vyama. Mnyika ni rafiki yangu. Ninachojua ni kwamba John Mnyika na Halima Mdee wanaenda ACT-Wazalendo ambapo anaenda kuwa GS. It's a matter of time.
Hili namie nimelisikia mkuu.
Unajua hawa ni wasomi vijana,wanahitaji sehem yenye kuwapa fursa na yenye malengo thabiti kwa faida ya wananchi na sio kuishi kwa kiki kila siku,badala ya kushughulikia masuala ya wanancho wao Chadema ni kesiii,na kusghulikia issue ndogoo ambazo CCM wanazitibu ili Chadema wa concentrate huko,yaani kama wamewashikia remote vile.

Maana wakuu juu hawataki kuachia na tayari wameishanusa mamluki ndani ya Chama.
 
Safi sana mkuu,umeeleza vizuri sana,.
Sasa hivi imekuwa viongozi wanaishi kwa maigizo tuuu
 
Mweshimiwa sana John Mnyika napenda kukumbusha badala ya kushadadia operation UKUTA tafadhali njoo huku jimboni tufanye harakati za maendeleo!

Tangu uchaguzi mpaka leo bado huku Mbezi Msumi maji ni shida, umeme imekuwa ndoto, barabara hajizachongwa tangu alipoondoka YESU.

Nakusii siasa za uanaharakati zimepitwa na wakati njoo huku tujenge UKUTA wa maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…