Mnyika is the brightest MP in Tanzania

Mnyika is the brightest MP in Tanzania

Mwanajavi Lukolo, Nyongise! Ushauri mwanana kabisa huo kama umande mzuri juu ya majani wakati wa alfajiiri. Ni ukweli Mh. J.J. Mnyika ni mmoja kati ya Wabunge hodari kabisa hapa Tanzania kwa sasa. Nakuunga mkono kabisa kwa ushauri huo. Mh. Mnyika tafadhari zingatia hayo, kuna watanzania wengi tu wanaoridhishwa na utendaji wako.



Mdogo wangu Mnyika, nakuonya mimi Lukolo kama kaka yako, kwamba wewe ndiye mbunge bora wa Tanzania. Wewe ndiye uliyetoa hoja nyingi zaidi kuliko wabunge wote nchini, wewe ndiye uliyeuliza maswali mengi sana sambamba na Tundu Lissu. Zitto Kabwe, hakuwemo hata katika orodha ya wabunge kumi bora wa nchi hii katika bunge la 2010 - 2015. Kwa viwango ulivyovifikia Mhe. Mnyika, hupaswi hata kidogo kujishushia heshima kwa kufanya malumbano na watu wa kawaida kabisa kwenye mitandao, wenye nia ya kutaka kukutoa kwenye mstari.

Mnyika hebu komaa kidogo kisiasa mdogo wangu, majibu yako kwa Zitto yanakushushia hadhi na kumpa umaarufu usio wa lazima Zitto. Hebu fanya kazi ya kujenga chama chako cha CHADEMA, na achana kabisa na hizi story za Zitto. Wanasiasa waliokomaa hupinga maandishi ya kwenye gazeti kwa kumshitaki mhariri na si kumjibu mchangiaji wa habari kwenye gazeti. Wanasiasa waliokomaa hawapotezi muda kujibu tuhuma za kitoto za kwenye mitandao.

Mnyika komaa kisiasa! Hivi sasa wewe ni naibu katika mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini, si mtu mdogo hata kidogo. Hupaswi kuweweseka kama mtoto kila unapoguswa. Kuna mengine ambayo unaweza kuyajibu kwa kuitisha press conference iwapo yataonekana yanataka kuleta madhara kwako na kwa chama, na kuna mengine ambayo unapaswa ku-ignore. Lakini kuna yale ya kawaida ya kila siku yanayojitokeza, muache msemaji wa chama ajibu. Ni kujidharirisha sana, kukesha kwenye mitandao kujibu kila hoja ya kipuuzi inayorushwa humo. Usipoteze muda wako mhimu kushughulika na watu wasio kuwa na madhara kwako.

Nimekuonya na kukushauri kama kaka yako, ukishupaza shingo, usinililie itakapovunjika.
 

Mpo sasa juu ya mlichokiandika.

Niseme tu kwa ufupi kuwa, Barcelona fc siku zote inamwombea Christiano Ronaldo awe unfitness, sio kwasababu wanamchukia Ronaldo la hasha! Bali ni kwasababu Christian Ronaldo anamathara kwenye ushindi wao.

Hakuna mtu asiyependa Mnyika awepo ni mbunge wake tena kwa chama anachokipenda yeye, ata wanachadema japo tunawabunge na tunawapenda katika majimbo yetu lakini bado tunawaonea wivu watu wa Ubungo na Singida kwa Tindu Lissu.

John Mnyika na Tindu Lissu ni lever ingine katika medani za kibunge na uwezi walinganisha na wengine japo wabunge ni wengi.

Yani ni hivi, kama tunazungumzia soka, basi hawa ni Ronaldo na Messi
sasa kama hao ni Ronaldo na Messi na ZZK nae?
 
wabunge.jpg
 
Hivi kuongoza kuomba muongozo spika ndiyo unakuwa mbunge bora.

Nimecheka sana.
 
Ahadi ya maji na barabara jimbo la ubungo bado hajatekeleza. Alituahidi tukakesha Loyola kulinda kura lakini hatujaona matunda.
tuendelee kukesha na mwaka huu tuakikishe madiwani na wabunge wengi wa ukawa wanaongezeke ili waweze kuongeza udhibiti wa halmashauri
 
Nina uhakika kabisa wewe pamoja na wanaubungo wote mnaujua ukweli kwamba Mnyika amekuwa akifuatilia kwa karibu sana suala la maji, na mnaujua pia ukweli kwamba kuna kila mikakati inayofanywa hivi sasa kuhakikisha maji yanapelekwa ubungo. Mmekuwa na Keenja kwa Miaka mingapi na alifanya nini?

Ninyi mnalalamikia maji na barabara ilihali mnajua kabisa kwamba serikali iliyokuwa madarakani haikuwa hata na uwezo wa kulipa wafanyakazi mishahara, na inaondoka madarakani ikiwa na madeni makubwa kiasi cha kila mtanzania kudaiwa zaidi ya laki sita, hizo pesa za kujengea barabara na kuleta maji wangetoa wapi? Mnyika anafanya biashara gani inayoweza kumpa pesa za kupeleka maji na kujenga barabara Ubungo yote?

Ngoja niwashauri kitu watu wa Ubungo, kama mnataka maji na barabara viletwe kwa haraka Ubungo, chagueni Rais kutoka UKAWA. Huyo atasaidiana na Mnyika kuhakikisha ahadi hiyo inatekelezwa. Vinginevyo ni kazi bure. Hata Zitto huko kwao hajafanya lolote la maana.
Kamanda JF siyo sehemu ya porojo kwa faida ya JF tutajie hizo idara za serikali ambazo wafanyakazi wake hawajalipwa mishahara, yaani Mnyika kashindwa kutimiza ahadi zake mnazua uongo.
 
Mnyika alete maji Ubungo kwanza,tunamsubiri ana maswali magumu sana ya kujibu

Huna uwezo wa kupambana na Mnyika wewe , Mnyika tunamuona anavyoibana serikali katika swala la maji na mambo mengine, usitufanye wajinga hapa, aliwahi kuibana serikali kuhusu Maji ubungo prof Magembe akapwaya bungeni. Mlaumu kwanza Kikwete aliyeshindwa kuwapa maji ya uhakika watanzania kwani ndiye anakusanya kodi za watanzania na tumuhoji pesa zetu kazifanyia nini?

Ubora wa Mnyika hauna shaka hata kidogo, ni miongoni wa wabunge makini ambao wakisimama bungeni serikali inahaha kote kote kuokoa jahazi ili isizame. Hongera sana Mnyika fanyia kazi ushauri uliopewa achana na wasaliti wenye akili tunajua.
 
Mnyika ni bora kwa Chadema kawazidi kina Lema, Sugu, Wenje,.
 
Duuh .. nilijua nintaasisi fulani ndio imetoa tamko hilo kumbe ni swala la mtu mmoja .

Ambaye anaweza kua ni Ndugu,mfanyakazi , au mwana siasa mwenza wa Mbunge huyo .

haya by the way hongera kwa kiasi chako unefanikiwa kumpigia kampeni .
Sema huku kumuuita Mbunge Bora ,Usilifanye kimajuimuisho kifanye la kwako ww mwenyewe

Ubora unakuja pale wanapowakilisha na watanzania wengine pia ambao siyo wa Ubungo! Muchrespect to him!
 
Wananchi wa Ubungo, Bonyokwa, Temboni, Kimara, Manzese wanataka maji na barabara siyo muongozo spika.

Raisi mwenye mamlaka - ccm
Waziri mwenye dhamana - ccm
Naibu waziri - ccm
Mkurugezi wa Almashauri - ccm
Meya - ccm

......................?
 
Raisi mwenye mamlaka - ccm
Waziri mwenye dhamana - ccm
Naibu waziri - ccm
Mkurugezi wa Almashauri - ccm
Meya - ccm

......................?
Sasa kama alikuwa anayajua haya yote kwa nini alitoa hizo ahadi au ndiyo ulaghai wa kisiasa kuona wanaubungo wajinga.
 
Huna uwezo wa kupambana na Mnyika wewe , Mnyika tunamuona anavyoibana serikali katika swala la maji na mambo mengine, usitufanye wajinga hapa, aliwahi kuibana serikali kuhusu Maji ubungo prof Magembe akapwaya bungeni. Mlaumu kwanza Kikwete aliyeshindwa kuwapa maji ya uhakika watanzania kwani ndiye anakusanya kodi za watanzania na tumuhoji pesa zetu kazifanyia nini?

Ubora wa Mnyika hauna shaka hata kidogo, ni miongoni wa wabunge makini ambao wakisimama bungeni serikali inahaha kote kote kuokoa jahazi ili isizame. Hongera sana Mnyika fanyia kazi ushauri uliopewa achana na wasaliti wenye akili tunajua.
Huo ni mtazamo wako na uko sahihi,Lakini swala hili litaamuliwa na wana Ubungo wanaoguswa na tatizo moja kwa moja.Tunamsubiri.
 
Back
Top Bottom