Nina uhakika kabisa wewe pamoja na wanaubungo wote mnaujua ukweli kwamba Mnyika amekuwa akifuatilia kwa karibu sana suala la maji, na mnaujua pia ukweli kwamba kuna kila mikakati inayofanywa hivi sasa kuhakikisha maji yanapelekwa ubungo. Mmekuwa na Keenja kwa Miaka mingapi na alifanya nini?
Ninyi mnalalamikia maji na barabara ilihali mnajua kabisa kwamba serikali iliyokuwa madarakani haikuwa hata na uwezo wa kulipa wafanyakazi mishahara, na inaondoka madarakani ikiwa na madeni makubwa kiasi cha kila mtanzania kudaiwa zaidi ya laki sita, hizo pesa za kujengea barabara na kuleta maji wangetoa wapi? Mnyika anafanya biashara gani inayoweza kumpa pesa za kupeleka maji na kujenga barabara Ubungo yote?
Ngoja niwashauri kitu watu wa Ubungo, kama mnataka maji na barabara viletwe kwa haraka Ubungo, chagueni Rais kutoka UKAWA. Huyo atasaidiana na Mnyika kuhakikisha ahadi hiyo inatekelezwa. Vinginevyo ni kazi bure. Hata Zitto huko kwao hajafanya lolote la maana.