Mnyika is the brightest MP in Tanzania

Mnyika is the brightest MP in Tanzania

Wewe Sasa unatafuta SOKOMOKO NA WENYE DINI YAO! Yaani hotuba ya Mnyika unaifananisha ni QURAN TUKUFU! Kwa maana nyingine Mhe. Mnyika ni sawa Mtume Mohammed SAW?!

Hapo ndo utagundua kifuata upepo
 
Jk aliahidi watu wa kigoma kuwa ataigeuza kigoma kuwa dubai ya tanzania leo kiko wapi?jk aliwaahidi watu wa kagera kuwajengea international airport pale kajunguti leo ipo wapi?jk aliwaahidi wakaazi wa kanda ya ziwa kuwanunulia meli mpya ktk ziwa victoria leo ipo wapi?wacha kuweweseka.

Anazungumziwa myika
 
Endelea kumuomba mungu atupe uhai utajua nin maana ya WAZALENDO

Endelea kuota ndoto za mchana,eti wazalendo wakati mnabeba viroba toka crdb kwa ajili ya kuugandamiza upinzani wa kweli?
 
Endelea kumuomba mungu atupe uhai utajua nin maana ya WAZALENDO

Kama uzalendo ni kuwadanganya unao waongoza kwa kuwanunulia baiskeli na wewe kiongozi unatembelea hammer,na kumiliki vitalu vya gesi basi uzalendo huo ni sumu na inabidi kuuogopa kama ukoma.
 
Tunasubr hela za escrow na nyingne zinazofann n hizo kama safari hii wataambiwa warejeshe ndipo tuweke maji ubungo na kwngneko,coz si ubungo tu kuna shida maji!
 
Miaka 54 ya uhuru mmeshondwa kuyapata hayo maji toka kwa serikali ya chama tawala,leo hii una taka hayo toka kwa mbunge?mbona unashindwa kufikiria kwa kutumia akili ya kawaida?
wewe umayetumia akili ya kawaida unataka kuniambia kwamba Mnyika alipoahidi kuwa atahakikisha watu wa jimbo la Ubungo tunapata barabara na maji alikuwa hatumii akili ya kawaida? Kama alijua kuwa tumeshindwa kupata maji miaka yote hiyo kwa nini atuahidi, alituongopea?
 
Mnyika ni bora kwa Chadema kawazidi kina Lema, Sugu, Wenje,.

mkuu,Mnyika si bora kwa CDM tu,ni hazina ya Taifa yule.CDM ina wabunge ambao hawazidi watano lakini Taifa lina wabunge wawili ndani ya CDM (walikuwa watatu kabla ya ZZK kujivua uanachama),nao ni Mnyika na Lissu.
 
Izo ahadi ndo wanaztumia kujenga vitega uchumi vyao,halafu badae watumbie watoto wao wana akili sn.........,si unaona miji yote magorofa yao!!
 
Mbona mnapenda kuwalinganisha wabunge wa chadema na zito kwani hakuna ccm wakulinganishwa nao au ccm wote ni vilaza sana! Au zito ndo jembe lenu ccm
Mzee unajikanganya mara Tunalinganisha Chadema na Zitto sio ccm,mara tena Zitto ndo jembe lenu ccm,mbona mbele nyuma?
 
Hoja ipi unataka ndugu, hapa hoja ya msingi ni Maji, na Maji yako chini ya wizara ya Maji! Sasa Mnyika ahukumiwe vipi? Je! Hakuisimamia serikali kuleta maji ya kutosha ubungo? Je? Unajua ni nani alitaka kukwamisha budget ya Maji isipite bungeni? Kamuulize Prof.Magembe atakwambia Mnyika alitaka kuninyang'anya uwaziri. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Average
 
ha ha haaaa watu wanatafuta sifa et kujifanya wanajibizana na ZZK? Mnyika anajibizana na sisi mafans wa ZZK; kwan aloweka picha n ZZK au sisi. ZZK iz another level
Zitto kwa asili yake ni msaliti, na usaliti huo hajaufanya CHADEMA tu bali pia ndani ya ACT baada ya kumhadaa Limbu na kubadilisha jina la chama kutoka ACT - Tanzania kwenda ACT - Wazalendo na kukiita chama chake. Zitto hajatimiza miezi sita ya uanachama ndani ya ACT imekuwaje ateuliwe kuwa kiongozi mkuu wa Chama? Hiyo ni kwa mujibu wa katiba ipi ya chama?
 
Jamani kwa waliofuatilia hotuba ya kambi rasmi ya upinzani mtakubaliana na mimi kuwa John Mnyika is the best Mp.
Hotuba ya kurasa 119,zilizosheheni hoja kali ni record.

Mnyika ni moja ya ya MP wajinga na mbumbu kuwahi kutokea Tanzania. Mbunge huyu amekuwa akitupotezee muda mwingi sisi wana Ubungo kwa kuandaa mandamano yasiyokuwa na tija, Hotuba unayoiongelea imejaa malalamiko, lugha za kejeli, uchonganishi na uchochezi mtupu, Hotuba zenye tija hujikita kwenye "wayforward", kutafuta ufumbuzi badala ya kulalamika tu. Hotuba za Watu makini ni za Akina Zitto, Nchemba, Job Lusinde, Wasira, Cheyo, Mtikira, Makonda, Chenge, Muhongo, Ngereja, Kunana, Nape bila kujali kuwa ni wabunge au siyo Wabunge, hotuba zao ni za kijamii zaidi, hazilengi kushambulia kundi fulani na kulibeza, zinalenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili Watanzania, siyo huo UHARO wa Mnyika.
 
The wayfoward nikuondoa ccm madaraka ili dola ishikwe na watu wenye nia njema na nchi hii. Wabunge kaziyao kubwa nikueleza serikali matatizo ya maeneo yao. Serikali itoe pesa labda ya maji. Ss serikali ya ccm imeshindwa kufanya hivyo. Kila siku ni ufisadi tu. Hakuna hela ya maendeleo. Mh mnyika kila siku anasema bunge ufisadi , serikali acheni kuingia mikataba ya kifisadi, kodi ikusanywe ipasavyo. Hii wayfoward ndugu yangu ni ipi. Wapeni nchi CHADEMA (UKAWA)
 
Mnyika ni moja ya ya MP wajinga na mbumbu kuwahi kutokea Tanzania. Mbunge huyu amekuwa akitupotezee muda mwingi sisi wana Ubungo kwa kuandaa mandamano yasiyokuwa na tija, Hotuba unayoiongelea imejaa malalamiko, lugha za kejeli, uchonganishi na uchochezi mtupu, Hotuba zenye tija hujikita kwenye "wayforward", kutafuta ufumbuzi badala ya kulalamika tu. Hotuba za Watu makini ni za Akina Zitto, Nchemba, Job Lusinde, Wasira, Cheyo, Mtikira, Makonda, Chenge, Muhongo, Ngereja, Kunana, Nape bila kujali kuwa ni wabunge au siyo Wabunge, hotuba zao ni za kijamii zaidi, hazilengi kushambulia kundi fulani na kulibeza, zinalenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili Watanzania, siyo huo UHARO wa Mnyika.

Poor you!!
 
Back
Top Bottom