Mnyama simba ni noma!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Vijana watatu wakiwa porini kwa ajili ya kutafuta kuni,kwa bahati mbaya mmoja wao alijikata kwa panga mguuni na kuumia vibaya sana.Wakaamua kumbeba kwa zamu kurudi naye nyumbani kwa sababu alikuwa hawezi kutembea mwenyewe.Mara ghafla wakiwa njiani,simba akatokeza.Wale jamaa wakambwaga mwenzao chini,wakatoka mbio kuokoa maisha yao.Walipofika nyumbani walishangaa kumkuta yule jamaa aliyeumia mguu kwa kujikata kwa panga akiwasubiri.Jamaa akawaambia;'mliponibwaga chini na mimi nilitoka mbio kwa kutumia njia tofauti na yenu.
 
Vijana wawili wakiwa porini,mara ghafla wakakutana na simba.Kijana mmoja akainama na kuanza kuzifunga vizuri kamba za raba zake.Mwenzie akamwambia;'unafunga kamba za raba zako ili ukimbie,unafikiri utamshinda mbio simba?.Jamaa akajibu;'hapana,nataka nikimbie kuliko wewe ili nisiliwe na simba!'.
 
Jamaa kataka kujiua wa2 wakmzuia wakashndwa jamaa akaamua kwenda porini lkn baada ya muda wanamuona anakuja mbio huku simba akiwa nyuma.
 
lol kumbe nia yake amshinde mwenzake kukimbia ili aliwe na simba.interesting
 
Hey!akimbie ili awe mbele ya rafiki yake ili simba ajipatie mlo
 
Jamaa kataka kujiua wa2 wakmzuia wakashndwa jamaa akaamua kwenda porini lkn baada ya muda wanamuona anakuja mbio huku simba akiwa nyuma.

Duh! hii kali mkuu sasa jamaa kashaamua kufa si atulie tu simba amtafune? Labda jamaa Intension yake ilikuwa kujiua kwa kifo anachokipenda yeye sio kuliwa na simba
 
Wawindaji walimkuta jamaa yuko juu ya mti uliojaa miiba.Wakamwuliza wewe,unafanya nini huko juu.Jamaa akawajibu juzi nilikuwa nafukuzwa na Simba ndio nikapanda kwenye huu mti sasa nimeshindwa kushuka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom