Mnishauri jamani, hizi hospitali zinatuchanganya

Mnishauri jamani, hizi hospitali zinatuchanganya

Xin shan low

Member
Joined
Jun 26, 2025
Posts
94
Reaction score
52
Nimepima hospitali moja wakasema nina malaria 4,wamenipa dawa, kabla sijameza dawa nikaenda hospitali nyingine kuhakikisha wakasema sina malaria,

Nipo njia panda, nimeze dawa au nisimeze?
Ushauri wenu tafadhali
 
Walitumia kipimo gani? Je sehemu ya kwanza na ya pili kipimo kilikuwa tofauti au ni kile kile?
 
Ukiona hospital yoyote inakwambia una Malaria zinazohesabika sijui 1,2,3,4,5,6 ondoka haraka hapo hamna hospital ni ubabaishaji
 
Huko si ndio watasema imepanda kichwani?
Let me tell you this, waafrica na WA Tanzania tunadharau sana hizo public hospitals ila ukweli unabakia pale pale .... Pamoja na unaoita uzembe sijui kutoka kujali wateja lakini still public hospitals ziko vizuri...

Aende Hospital akapate huduma ila asiingie uchochoroni humo kwenye vipimo hawachelewi kukupa majibu wanayoyataka wao
 
Huyo wa malaria nne ni tapeli, hasa hizi hosp private wamekaa kinjaa njaa sana na kudanganya wagonjwa, hosp nyingi za serikali zinasema kweli kama huna huna kweli, nenda kapime na magonjwa mengine sio kila dalili mbaya ya mwili ni malaria peke yake.
 
Fanya kuchemsha mwarobaini kisha kunywa ×3 kwa siku,hauna madhara mti huo.
Kisha angalia hali yako itavyokuwa.

Kama una hangaika kujua kama unaumwa au huumwi basi ongeza hospital ya tatu ukapime.
Kisha analyse matokeo.
Kama hospital 2 zinatoa jibu sawa nawe ukahisi wako sawa basi kunywa dawa.Else kunywa mwarobaini.
 
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom