Mnisaidie hawa watoto ni wafanyeje?

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,400
Kuna kijana nilimchukua akiwa bado mdogo baada ya wazazi wake kufariki yeye na mdogo wake wakike,(yatima)ni watoto wa ndugu yangu aliyefariki nikawalea toka primary mpaka sec.ambapo sasa wako form four.wote niliwapeleka private school sababu sikupenda wajisikie vibaya sababu watoto wangu tayari walikwisha kuwa watu wazima wanajitegema.

Miaka 3 nyuma kuna binti nilikutana naye akiwa anashida,nikamchukua nikaishi naye ila alikuwa akifanya kazi za ndani na nilikuwa namtunza vizuri hata kwao alikataa kurudi tena.

Jamani week ya pili hii yule binti alianza kuumwa nikampeleka Hosp.kupimwa nikaambiwa Mjamzito..nilivyo muuliza nani kakupa mimba kasema kijana wako(ambaye ni yatima yuko form 4)

Nifanye nini kwa maana nina hasira na huyu mtoto kwa sababu nimewekeza pesa nyingi kumsaidia na ukizingatia hana baba wala mama..huyu binti na yeye yale yale tena bado ni mdogo miaka 18.

Niwafukuze au niwafanyeje?sababu hata watoto wangu mwenyewe mbona hawajawahi kufanya kitu cha namna hii??

Nitawezaje kulea hii familia sababu hakijifungua itakuwaje hapa.sababu ninachokifanya nikama nawasaidia katika maisha yao.
 
Duh pole sana mkuu, cjui kwa nn watu wa namna hii huwa wanazisahau haraka sana dhiki zao,
hii inankumbusha story ya mtoto wa ndg yangu mmoja wa mbaaali ambaye alichukuliwa na auntie yake kuanzia akiwa mdogo, amesomeshwa na sasa yupo chuo kikuu ila jamaa kaingia kwenye room ya baba mwenye nyumba kachukua ATM card kajisevia million 8. inakera na inaudh mno duh
 
mmmh, pole lakini kuna raha gani kupika keki nzuri mwisho ipakwe pili pili?

Kwa mtazamo wa haraka haraka, hili lako ndugu yangu, labda uamue kutumia unyama lakini kibinadamu huu mzigo wako kabisaa.

Hawa wote kwa pamoja wanakutegemea na hawajaweza kujitegemea. Na hata kama itabidi wajitegemee inabidi uwawezeshe kwa njia yeyote, lazima mwanzo wakutegemee wewe.

Sasa fikiria, kijana akifaulu kwenda form 5? Na itakuwa na maana kama atafaulu, si inabidi uendelee kulea mkewe?
Labda cha kufikiri, angekuwa mwanao ungefanyaje?

Pole, pamoja na shida zao lakini mihemko ya ujana iko pale pale so wao kuwa hivyo haiwandolei changamoto za kukua na ujana.

Shukuru Mungu wanao hawakukuangusha, kumbuka kila kijana anareact tofauti na changamoto za kukua, siwezi kuwalaumu sana moja kwa moja, maana najua ni hatua ngumu.

Kwanza waonye kwa pamoja ila kumbuka kosa kubwa ni kurudia kosa. Kwa kuwa kijana ndio anamalizia shule angalau akimaliza kama utaweza ukamsaidia kupata pa kujishika kwa hiyo miezi michache ukisikilizia matokeo yake.

Lakini mwisho wa siku, angalau wanapata mtoto, je wangekutwa na VVU??
Kwanza watoto ni faida tupu, katakuwa kajukuu kako na utakapenda tu, na utakumbuka hasira hizi na kucheka.
 
Je, toka umewachukua kwa lengo la kuwalea, ulishawahi kuongea nao kuhusiana na suala zima la mapenzi?. Kama haujawahi kuwashauri kuhusu kuzikabili tamaa za ujanani basi kosa ni la kwako. Na hapo utakuwa umevuna haki yako. Hata biblia inasema Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. Kama kweli hukuwaongoza katika suala zima la kukabiliana na tamaa, waache.
 
Uliamua kumchukua na kumlea kama mwanao, mtreat kama mwanao. Watoto hukosa, hata wanao wangeweza kukosa (wa wengine weshakosa zaidi ya hilo).

Mungu aliyekupa uwezo (financially) na moyo wa kuwachukua na kuwalea atakupa moyo na uwezo wa kuendelea kuwasupport!

Mreprimand kijana kama ambavyo ungefanya wa kwako, mwambie once akianza kujitegemea tu, atamchukua huyo dada na kulea mwanawe!

As for binti, naye anastahili share yake ya kuonywa na kuonesha jinsi gani amekuwa irresponsible, anastahili 50% ya lawama unless alibakwa!
 
Kongosho anayesoma ni kijana ambaye ni yatima na ana undugu wa mbali na mleta maada!
Aliyepata mimba ni Mdada wa kazi ambaye yuko 18, na ametiwa mimba na huyo kijana.
 
Last edited by a moderator:
asante kwa mwongozo best.

Nilipitiwa.

Kongosho anayesoma ni kijana ambaye ni yatima na ana undugu wa mbali na mleta maada!
Aliyepata mimba ni Mdada wa kazi ambaye yuko 18, na ametiwa mimba na huyo kijana.
 
Last edited by a moderator:
Duh pole sana mkuu, cjui kwa nn watu wa namna hii huwa wanazisahau haraka sana dhiki zao,
hii inankumbusha story ya mtoto wa ndg yangu mmoja wa mbaaali ambaye alichukuliwa na auntie yake kuanzia akiwa mdogo, amesomeshwa na sasa yupo chuo kikuu ila jamaa kaingia kwenye room ya baba mwenye nyumba kachukua ATM card kajisevia million 8. inakera na inaudh mno duh

umenishtua mno
nina ndugu yang alinifanyia hivi hivi
tofauti hapo ni amount
kidogo nifikiri tunafahamiana lol
 
Fukuza wote kama mbwa,kijana wa form foo hajui kutumia dawa ya penzi!!mwe! .....fukuza.
 
Back
Top Bottom