Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

leadermoe

R I P
Feb 15, 2017
1,392
4,573
Mpendwa msomaji.

Kama ulisoma mkasa
(Nilivyo Okoa Maisha Ya Watalii toka Finland).

Huu ni mkasa kamili wa kisa kile. Nilielezea visa vichache kwa ufupi, lengo lilikuw kuonyesha msaada niliotoa kwa wafin.

Hapa utapata historia nzima ya maisha yangu na mwendelezo wa ule mkasa na wale watalii in details. Ni mkasa mrefu, ila nitajitahidi kumaliza kwa wakati.

Angalizo: Lengo ni kujifunza, kupitia mapito ya wenzetu, sina maana ya kutaka kuonyesha nilicho nacho, wala sina nia ya kujikweza. Imani yangu ni kupitia mkasa huu, kuna watu watapata jambo la kujifunza, kuna watakao burudika, nk.

******'
Tahadhari:

Picha zilizo tumika katika mkasa huu zimegawanyika katika makundi mawili:-

Kundi la 1:
Hazina uhusiano na mkasa huu, nimeziweka kama Mfano wa yale ninayoyaeleza yanavyofanana na picha husika.

(Mfano: Muonekano wa Rosemary , Zainabu na Zaituni n.k)

Kundi la 2:
Zina uhusiano na mkasa huu, ila sikuzipiga mimi, ziko mtandaoni. (Mfano: majina ya Airport, maduka, hotel n.k)

Majina yote ya watu yaliyotumika sio halisi, yamebuniwa kuleta radha, Wahusika wanayo majina yao halisi.

Maelezo mengine yote ni matukio na majina halisi ya maeneo husika.

Note 'disguised'
*********************

Utangulizi.

Katika maisha tunakutana na changamoto nyingi, mateso, kukatisha tamaa, umasikini, chuki, hasira, uongo, usariti, na mengine mengi.

Ndio maana kuna maandiko yanasema

"ulimwenguni kunayo dhiki nyingi"

Huu ni mkasa unaohusu familia moja ya mzee Anthony na mke wake Antonia. Baada ya changamoto, mateso na manyanyaso mengi, hatimae Anthony anafanikiwa kuandikishwa shule, jambo ambalo baba yake hakuwa ana litaka.

Anthony anapata msaada wa kulelewa na rafiki wa baba yake, malezi ambayo baba yake hakuona umuhimu wa kumpa.

Hatimae Anthony anafanikiwa kuanza maisha mapya, anapata watoto ambao anajitahita kuwapitisha njia salama na malezi bora.

Kijana mdogo anaonekana kipenzi cha wazazi, lakini anapata heka heka kipindi cha masomo yake, yaliyopelekea kuwa mbali na wazazi wake.

Mzee Anthony anawakabidhi vijana wake majukumu, je watayatimiza?

Mama anakataa kijana wake asiende kuishi ulaya, je atasikilizwa?

Fuatana nami katika mkasa huu kwani kuna mengi ya kujifunza, kuburusisha na kusikitisha.

Kiitos

***********

1939

Part One
Anthony
Anthony amezaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha 'X', wilaya ya 'X' mkoa wa 'X'. Haiba yake ni mpole.

Ni mtoto yatima , mama yake alifariki Anthony akiwa na miaka mitatu tu. Aliugua malaria kutokana na umbali kutoka hapo kijijini ''X'' mpaka hospitali ya wilaya 'X', alipoteza maisha akiwa njiani.

Anthony amelelewa na baba yake kwa msaada wa bibi yake, bibi yake alifariki Anthony alipofikisha miaka 7. Akabaki na bana pekee.

Baba yake Anthony alioa mke mwingine, mke mdogo hakumpenda Anthony, alimtumikisha na kumtuhumu mambo ya uongo.

Siku moja mzee George alitembelewa na rafiki yake mzee John, mzee John alikuwa anaishi kijiji 'X' kiko jirani na kijiji 'X' anakoishi mzee George .

Mzee John alimkuta Anthony akifanya kazi ya kutwanga kisamvu, mama yake mdogo amekaa anakula karanga, Ilikuwa ni majira ya saa 10 jioni.

Kumbe toka asubuhi mtoto wa miaka 8 hakuwa amekula, mama yake wa kambo alipika chakula mchana akala peke yake kikaisha, mtoto aliporudi toka machungani ndio akapewa kazi ya kutwanga kisanvu, kisha kipikwe ndio ale.

Baba yake aliyajua yote hayo ila alipuuza kwa madai kuwa anamfundiasha maisha. Mzee George hakuwa amempeleka shule Anthony japo ana miaka 8.

Mzee John hakupendezwa na mazingira anayoishi Anthony, alijaribu kumshauri rafiki yake, lakini haikusaidia.

Mzee John hakupendezwa na majibu ya rafiki yake, akaomba apewe yule mtoto ili akamsomee kwake, mzee George kwa kuona anapunguziwa mzigo alikubari. Mzee John aliondoka na Anthony huku akiahidi kumpeleka shule.

***
Anthony akiwa kwa mzee John alikuwa mtoto mtiifu, mzee John na mke wake walimpenda sana. Walikuwa na watoto wawili, Paul na Antonia. Paul alikuwa darasa la 1 shule ya mission. Antonia alikuwa ni binti mdogo.

Anthony aliandikishwa shule ile ile ya mission aliyokuwa anasoma Paul, alikuwa mtiifu sana nyumbani na shuleni. Walimu wake walimpenda.

****

Akiwa darasa la 3, walipokea taarifa ya kifo cha baba yake, nyumba yao ilishika moto akiwa amelala ndani, kutokana na ulevi mzee George alishindwa kujiokoa , akachomwa na ule moto mpaka mauti.

Mke wake alifanikiwa kukimbia, ila hakurudi tena pale nyumbani. (kulikuwa na tetesi ndie aliwasha ule moto , sababu haikujulikana).

Anthony akawa amepoteza wazazi wote wawili, akabaki yatima. Mzee John aliendelea kumlea kama mwanae bila kumbagua, alipomaliza darasa la nne, mzee John alihamia mkoa wa Arusha na familia yote.

Waliishi kijiji cha ngurudoto wilaya Meru. Akiwa arusha aliendelea kuwa kijana mwema. Alipofikisha umri wa kuoa, alimshirikisha mzee John kama baba, mzee alimwambia anapenda amuozeshe binti yake maana iliona atamfaa zaidi. Hakupenda amruhusu kuoa kabila la wenyeji wao.

Kipindi hicho Antonia alikuwa na miaka 16, ilikuwa mwaka 1962, mzee John aliamua kumuozesha kijana wa rafiki yake ili amtunzie baba yake jina, alimpa binti yake Antonia awe mke wake.

Baada ya kuoa kimira , Anthony aliamua kuhama pale nyumbani, alihamia kijiji ''X'' mkoa ''X''. Maisha mapya ya ndoa yalianza rasmi.
**********
Screenshot_20230313-203729_Instagram%20Lite.jpg
TAZARA-Track.jpg
 
Mpendwa msomaji.

Kama ulisoma mkasa
(Nilivyo Okoa Maisha Ya Watalii toka Finland).
Huu ni mkasa kamili wa kisa kile. Nilielezea visa vichache kwa ufupi, maana lengo lilikuwa msaada wa Kuokoa Watalii.

Hapa utapata historia nzima ya maisha yangu na mwendelezo wa ule mkasa na wale watalii in details. Ni mkasa mrefu, ila nitajitahidi kumaliza kwa wakati.

Angalizo: Lengo ni kujifunza, kupitia mapito ya wenzetu, sina maana ya kutaka kuonyesha nilicho nacho.
******'

Maisha na mapito yangu hapa duniani.

Nimeusimulia kwa urefu zaidi tofauti na ile Simulizi Ya kwanza.

Tahadhari:

Picha zilizo tumika katika mkasa huu zimegawanyika katika makundi mawili:-

Kundi la 1:
Hazina uhusiano na mkasa huu, nimeziweka kama Mfano wa yale ninayoyaeleza yanavyofanana na picha husika.
(Mfano: Muonekano wa Rose , Zainabu na Zaituni n.k)

Kundi la 2:
Zina uhusiano na mkasa huu, ila sikuzipiga mimi, ziko mtandaoni. (Mfano: majina ya Airport, maduka, hotel n.k)

Majina yote ya watu yaliyotumika sio halisi, yamebuniwa kuleta radha, Wahusika wanayo majina yao halisi.

Maelezo mengine yote ni matukio na majina halisi ya maeneo husika.

Note 'disguised'

'***********************

Utangulizi.

Katika maisha tunakutana na changamoto nyingi, mateso, kukatisha tamaa, umasikini, chuki, hasira, uongo, usariti, na mengine mengi.

Ndio maana kuna maandiko yanasema "ulimwenguni kunayo dhiki nyingi"

Huu ni mkasa unaohusu familia moja ya mzee Anthony na mke wake Antonia. Baada ya changamoto, mateso na manyanyaso mengi, hatimae Anthony anafanikiwa kuandikishwa shule, jambo ambalo baba yake hakuwa ana litaka.

Anthony anapata msaada wa kulelewa na rafiki wa baba yake, malezi ambayo baba yake hakuona umuhimu wa kumpa.

Hatimae Anthony anafanikiwa kuanza maisha mapya, anapata watoto ambao anajitahita kuwapitisha njia salama na malezi bora.

Kijana mdogo anaonekana kipenzi cha wazazi, lakini anapata heka heka kipindi cha masomo yake, yaliyopelekea kuwa mbali na wazazi wake.

Mzee Anthony anawakabidhi vijana wake majukumu, je watayatimiza?

Mama anakata kijana wake asiende kuishi ulaya, je atasikilizwa?

Fuatana nami katika mkasa huu kwani kuna mengi ya kujifunza, kuburusisha na kusikitisha.

Kiitos

***********



1939

Part One
Anthony
Anthony amezaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha 'disguised', wilaya ya 'disguised' mkoa wa 'disguised'. Haiba yake ni mpole.

Ni mtoto yatima , mama yake alifariki Anthony akiwa na miaka mitatu tu...
Asante sana kwa story cuzoo ngoja nitulie nisome vizuri!
 
Part Two
1963

Mwaka 1963 Walipata kijana wa kiume wakamuita Edward, furaha iliongezeka maana familia imepata mwanachama mpya.

Mwaka 1965 walipata mtoto wa pili wakamuita Edwin furaha ilizidi mara dufu. Familia ikawa na watu wanne.

Mwaka 1974 walipata mtoto wa tatu wakamuita Edson. Hapa sasa Anthony akaona kuna umuhimu wa kutafuta kazi ili aweze kumuda mahitaji ya familia.

Mwaka 1976 TAZARA walitangaza nafasi za kazi, Anthony alitumia nafasi hiyo kuomba kazi, bahati ikawa yake akapata kazi na kituo chake cha kazi kikawa kijiji cha kitete, wilaya mrimba, mkoa wa Iringa.
***
Hii ni simulizi ya maisha halisi ya Edson kijana wa tatu wa mzee Anthony na mama Antonia.
****
Naitwa Edson Anthony,nina haiba ya upole. Nimezaliwa mwaka 1974 katika kijiji 'X' wilaya 'X' mkoa 'X'. Mimi ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watatu wa mzee Anthony na mama Antonia.

Kaka yangu wa kwanza anaitwa Edward (RIP) na mwingine ni Edwin.

Baba yangu ni mwenyeji wa 'X' mama yangu ni mwenyeji wa ''X'' lakini amekulia Arusha. Baba yake alihamia mkoa huo kutoka mkoa wake wa ''X'' .

Baba yangu mzee Anthony alikuwa ni mwajiriwa wa TAZARA (Tanzania and Zambia Railway) Kituo chake cha kazi kilikuwa kijiji cha kitete wilaya ya mrimba mkoa wa Iringa.

Maisha yalikuwa mazuri kiasi na yenye furaha na upendo. Baba alikuwa na ng'ombe wapatao 50 na buzi 70, pale kijijini kwetu. Kutokana na mifugo ikabidi mama abaki pale kijijini kwa ajili ya uangalizi wa mji.

Tulikuwa na mashamba ambayo tulikuwa tunajipatia chakula kama mihogo, viazi, mtama, uwele, ufuta yaani tulikuwa tunafanya kilimo mseto.

Napenda kuchukua nafasi hii kusimulia histori ya maisha yangu, kuanzia malezi, elimu, mapenzi, utafutaji wa pesa na mafanikio yangu maishani.
**********

1974-1989

Maisha ya utoto

Nimezaliwa na kulelewa pale kijiji cha 'X', kabla ya kuanza shule nilikuwa nachunga mifugo yetu.

Kaka zangu walikuwa wanaishi na baba Iringa. Nilibaki mimi kwa kuwa nilikuwa mdogo.

Maisha ya machungani yalikuwa mazuri sana maana tulikuwa tunakamua maziwa ya ng'ombe tunakunywa pindi tukisikia njaa na kiu, nakumbuka moments za kubeba viazi vya kuchoma kwenye mkoba wa ngozi, maziwa kwenye kibuyu n.k

Machunganii ilikuwa ni kawaida kukutana na wachungaji wengine, hapo michezo iliendelea na kufanya nipende kwenda kuchunga.

Mama alinipa malezi naweza sema mazuri sana, mama yangu sio mkali, muda wote sura yake imechanua tabasamu. Baba yangu alikuwa mkimya sana ila aside na masihara.

Safari yangu ya kwanza kwenda Songea

Mwaka 1981 nilipelekwa shule lakini nilishindwa kushika sikio nikarudishwa. Nilianza shule ya msingi mwaka 1982 katika shule ya msingi 'X' nikiwa na miaka 8. Kipindi hicho ilikuwa lazima ushike sikio ndio uandikishwe shule.

Nilikuwa na bidii sana shuleni, pia nilikuwa najua kusoma herufi a, e i o u na kuhesabu mpaka kumi. Ikiwa ni kazi ya mama yangu tukiwa nyumbani nyumbani.

'My mom was my first teacher.'

Nilipofika darasa la pili nilichukuliwa na kaka yangu mkubwa Edward, ambae alikuwa askari mkoa wa Ruvuma wilaya ya Songea.

Nakumbuka siku moja kabla ya safari, sikupata usingizi, nilikuwa nawaza kupanda gari kwenda nje ya mkoa wetu.Nilishawahi safiri kwenda Iringa kwa baba ila nikiwa mgongoni, sasa naenda kwa miguu yangu.

Kesho yake asubuhi mapema mama alinivalisha kisha akanipatia maziwa fresh na mkate nile, baada ya kula alitusindikiza mpaka barabarani. Tulipanda bus linaitwa 'X' kutoka hapo kijijini ''X'' kwenda Mwanza, nili enjoy sana kwa mara ya kwanza. Niliona miti inarudi nyuma kadri gari linavyo kimbia.

Kutoka ''X'' mpaka Mwanza ni masaa kadhaa tu, hatimaye tuliingi standi ya ''X'. Kaka alibeba mabegi yetu tukaenda kutafuta taksi ili kwenda station ya gari moshi, kipindi hicho mabasi yalikuwa yanapita Kenya yanatokea Arusha kwenda Dar-Es-Salaam,njia ya kati ilikuwa ni gari moshi maana barabara haikuruhusu.

Tulifanikiwa kupata tiketi za gari moshi daraja la tatu, kaka alilipia siti 3 ili nipate sehemu ya kulala. Ilibidi tusubiri safari saa 10 jioni. Ilipofika sa 9 tulianza kupanda kwenye gari moshi, saa 10 kamili ilipiga honi mara tatu likaondoka.

Gari moshi liliendelea na safari huku watu wakipiga soga, lilikuwa limejaza sana mpaka abiria wengine walikosa siti wakasimama.Mimi nililala kwenye ile siti, kaka akaenda behewa la askari wenzake kupiga soga.

Siku ya tatu asubuhi kama saa 3 tuliingia Dar-es-Salaam, tulishuka na kutafuta UDA ya kuelekea magomeni kota, kwa mdogo wake na baba…

Siku ya pili tulipanda basi kwenda mpaka makambako, nakumbuka jina la basi 'kiswele coach' lilikuwa linaenda songea ila sisi tulishukia makambako ili twende kwa baba pale kitete.

Makambako tulipanda gari moshi la TAZARA kwenda kitete kwa baba. Kaka aliniacha kwa baba, baada ya wiki moja, baba alinipeleka Songea. Kutoka makambako tulipanda costa, tulifika Songea usiku sana.

……..

Nilipelekwa shule ya msingi Misufini kuendelea na darasa la pili.Kaka yangu alikuwa amepanga nyumba mfaranyaki, (jirani na ilipokuwa Buhemba hotel sijui kama bado ipo.)

Maisha mapya hayakuwa na ugumu sana katika kuzoea mzingira.Kutokana na uchezaji wa mpira nilipata marafiki wengi sana kwa haraka.

Kipindi kile kaka alikuwa na redio kaseti aina Panasonic double decks,alikuwa anapenda sana nyimbo za kongo kina Franco Makiadi, Pepe kale, wengineo.

Alikuwa anapenda sana suruali za kitambaa raini na mashati ya dog dog Kama alivyokuwa wanavaa wana muziki wa kongo.

Kaka yangu alikuwa ni mtu wa hasira za haraka sana 'short-temper', hali iliyopelekea kuchezea kichapo mara kwa mara toka kwa mjeda yule.

Alikuwa ananifunga na pingu mikono na kunipiga kwa waya, mikanda na mateke, wakati mwingine alinibana korodani. Nilipitia mateso sana kipindi hicho.

Pamoja na kuwa alinifanyia ukatili mara kwa mara, alikuwa na upendo sana usipomuuzi, tatizo nilikuwa mtoto nahitaji kujifunza, hakunipa hiyo nafasi.

Kila nguo ikitoka ilikuwa lazima niivae kwanza kabla ya watoto wengine pale mtaani, hilo simlaumu.

Kipindi hicho tunatoka mfaranyaki kwenda standi kuu kula chips mayai. Hakukuwa na vibanda vya chips mitaani, na ni lazima kutumia uma kwenye sahani ya bati ha ha haaaa.

Baada ya kuuzoea mji nilikuwa nafurahia kijichanganya na watoto wemzangu katika michezo. Nilikuwa sikosi uwanja wa maji maji kuangalia mpira wa ligi kuu, kila inapokuja timu yoyote kucheza pale. Kilikuwa ni kipindi maji jami iko moto sana, simba na yanga zilikuwa ni kawaida kufungwa pale.

Kwa kuwa wasimamizi pale getini ni asikari, walikuwa wananipitisha bila malipo. Maisha yangu yote niliyoishi Songea sikuwahi kulipa kiingilio kwa tukio linalo lindwa na polisi pale maji maji.

Nilikuwa mtundu wa kimya kimya sana, nilipenda kujifunza vitu hasa ufundi. Nakumbuka kuna siku nilijifanya fundi nikafungua redio ndogo, kaka alikuwa anapenda kusikiliza mpira RTD. Nikashindwa kuifunga baada ya vitu kubaki, ikabidi nivitupe kupoteza ushahidi (i was a kid). Aliporudi kakuta redio haiongei , kesho yake akaipeleka kwa fundi.

Fundi akanisagia 'kunguni', akamwambia kuna vitu havipo, vikipatika itaongea , nikapewa kazi ya kuvitafuta mpaka jioni akirudi avikute.

Sikufanikiwa kuviona, ikabidi nisubiri kipigo akirudi, jioni aliporudi nikamwambia sijaviona. Alikuwa na kawaida akitaka kunipiga kama ameva kombat anavua shati anabaki na suruali na buti.

Siku hiyo nilifungiwa chumbani kipigo kikaanza, nilichezea mikanda na mateke ya mbavuni mpaka askari wenzake walikuja dirishani, wakaanza kumtisha kuwa wata mshitaki kwa mkubwa wao. Ndio ikawa pona pona yangu. Hiyo nyumba kulikuwa na wapangaji askari watatu.

Kesho yake nilipandisha homa kali, kutokana na kile kipigo cha jana yake. kufika jioni nikazidiwa ikabidi nipelekwe 'mzena dispensary'. Kabla ya kwenda nilipigwa biti kuwa ole wangu niseme nimepigwa.

Kaka alishauriwa na wenzake akaombe gari ya polisi anipele hospitali ya peramiho, ni baada ya hali yangu kuzidi kuwa mbaya. Mwanzo alipata ugumu maana aliogopa chanzo cha ugonjwa wangu kujulikana.

Kesho yake nikawa na hali mbaya zaidi, ikabidi wale wenzake wakaombe gari, jioni hiyo nikapelekwa peramiho, nikatundikiwa drip 3 na nili lazwa kwa siku 5.

Baada ya kupata nafuu nikaruhusiwa kurudi nyumbani, kaka alikuwa mnyonge sana baada ya lile tukio, na vipigo vilipungua sana.

Aliambiwa nimeumia mbavu, ilibaki kidogo moja ivunjike, kwa mateke ya my brother (RIP).

Maisha yaliendelea hatimaye nilipofika darasa la 3, yaani baada ya mwaka mmoja. Tulirudi likizo nyumbani, nikiwa likizo nilimwambia mama kuhusu vipigo ninavyopata. Mama alihuzunika sana, alimsema sana kaka kwa ukatili ule alionifanyia, mama aliamua nisirudi na kaka.

Nikahamishiwa shule kutoka misufini Songea, kwenda kitete Iringa kwa baba…

*******
Table.jpg
Nimeisahau.jpg
Kiswele%20.jpg
Kiswele%20coach%20.jpg
Service%20Passenger.jpg
 
Back
Top Bottom