Bakari Maligwa
Member
- Aug 18, 2010
- 65
- 22
...Kwa kuwa ni kawaida ya binadamu kusahau; japokuwa si watu wote wanaosahau historia. Kumbukizi zinaonesha kwamba, Muafaka wa Zanzibar uliyopelekea kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (Zanzibar) kulitokana na sintofahamu na songombingo za kisiasa baina ya CUF (Maalim Seif Sharif Hamad) na CCM (ya Komandoo Salmin Amour Jumaa) tangu mwaka 1995. Mwaka 2000, Pemba tulishuhudia mauwaji ya watu takriba 33 na wengine kukimbilia Shimoni-Mombasa, Kenya. Pamoja na hayo, tulishuhudia wawakilishi wa CUF wakisusia vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa mara kadhaa kutokana na kadhia hiyo.
...Leo, kwa nini watu washangae Dk. Slaa kutomtambua Jakaya Kikwete? Kama ushindi aliyoupata JK haukuwa na "dosari" kubwa na ndogo kusingekuwa na haja ya Dk. Slaa kumkataa JK. Mbona hamshangai asilimia 73% ya wapigakura waliyojiandikisha kupiga kura kumkataa JK kwa (1) kutokumchagua na (2) kwa kutokupiga kura. Hata kura alizopata mwaka 2005, kama milioni 9.1, zimepungua hadi kufikia milioni 5.3 (hivi); na hili hamlioni? Au kama wasemavyo Waswahili, "NYANI HAONI NONGOLE?"
...Ipo haja ya kuona jinsi gani mtu mmoja na au chama (kikundi) cha watu wanaweza kumkataa mtu - hususan kwenye demokrasi ya watu - mtu kama hamkubali mtu, huo ni uhuru wake...na haijalishi anayekataliwa ni nani na au ana wadhifa gani! Kwa Dk. Slaa kumkataa JK ni haki; na ni haki yake - na ndiyo demokrasi. Bravo Doctor Slaa, revolution starts with cognitive ideas! ALUTA CONTINUA....