Mnashangaa Dk. Slaa kumkataa JK..?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnashangaa Dk. Slaa kumkataa JK..?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bakari Maligwa, Nov 16, 2010.

 1. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Kwa kuwa ni kawaida ya binadamu kusahau; japokuwa si watu wote wanaosahau historia. Kumbukizi zinaonesha kwamba, Muafaka wa Zanzibar uliyopelekea kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (Zanzibar) kulitokana na sintofahamu na songombingo za kisiasa baina ya CUF (Maalim Seif Sharif Hamad) na CCM (ya Komandoo Salmin Amour Jumaa) tangu mwaka 1995. Mwaka 2000, Pemba tulishuhudia mauwaji ya watu takriba 33 na wengine kukimbilia Shimoni-Mombasa, Kenya. Pamoja na hayo, tulishuhudia wawakilishi wa CUF wakisusia vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa mara kadhaa kutokana na kadhia hiyo.
  ...Leo, kwa nini watu washangae Dk. Slaa kutomtambua Jakaya Kikwete? Kama ushindi aliyoupata JK haukuwa na "dosari" kubwa na ndogo kusingekuwa na haja ya Dk. Slaa kumkataa JK. Mbona hamshangai asilimia 73% ya wapigakura waliyojiandikisha kupiga kura kumkataa JK kwa (1) kutokumchagua na (2) kwa kutokupiga kura. Hata kura alizopata mwaka 2005, kama milioni 9.1, zimepungua hadi kufikia milioni 5.3 (hivi); na hili hamlioni? Au kama wasemavyo Waswahili, "NYANI HAONI NONGOLE?"
  ...Ipo haja ya kuona jinsi gani mtu mmoja na au chama (kikundi) cha watu wanaweza kumkataa mtu - hususan kwenye demokrasi ya watu - mtu kama hamkubali mtu, huo ni uhuru wake...na haijalishi anayekataliwa ni nani na au ana wadhifa gani! Kwa Dk. Slaa kumkataa JK ni haki; na ni haki yake - na ndiyo demokrasi. Bravo Doctor Slaa, revolution starts with cognitive ideas! ALUTA CONTINUA....
   
 2. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amkatae, amkubali, alie, acheke, ajinyonge - bado JK ni rais aliyeapishwa. Sasa kumkataa JK unadhani kunamsaidia nini kama si kujitia majonzi tu. Mwanaume wa kweli anatulia na kujipanga upya kwa kuandaa mikakati kwa ajili ya 2015. Tujikumbushe huko Zanzibar, Maalim Seif alikataa kuitambua serikali na rais wake, kwani mambo yalisimama ?? Rais si aliendelea hadi uchaguzi uliofuata.

  Thiery Henry alifunga goli kwa mpira wa mkono, refa akalikubali goli japo vyombo vya elektroniki baadaye vilionyesha kuwa lilikuwa goli la mkono, je lilifutwa ?? Nasema, na narudia kusema kuwa mwanaume halisi hutulia na kujipanga upya si hili la kutoa tamko la kutoutambua ushindi. Haimsaidii kitu.
   
 3. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama tunaelewa demokrasia basi alichosema Slaa ni sahihi kwani ndicho anachokijua na kukiamini na wapo wengi pia wanakubaliana naye.Swala lakupanga mikakati alishalisema hata kabla ya uchaguzi na amelirudia mara nyingi sana,kwamba atajikita katika kuimarisha chama na kuuelewesha umma mipango yao dhidi ya nchi hii kama mkakati wa kuchukua nchi 2005
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ilikuwa vizuri ndugu yangu kabla hujacoment ungejifunza au kutaka kujua ni nini sababu ya Dr.Slaa kutomkubali Jk.
  Kwa nini Dr.Slaa mwaka 2005 hakukataa ushindi wa Kikwete akatae mwaka huu?
  Sio vizuri kuzungumzia jambo kiushabiki zaidi.
  Yaani unadiriki kufananisha ushindi wa jk na goli la mkono ktk football halafu bado unashangaa kwa nini Dr. Slaa amemkataa JK.
  Go back to school brother.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sahihisho: ni 2015
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Fisadi anapo-comment.
   
 7. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Vipi na wabunge wanamkubali au Dr. Slaa peke yake? Bora na wabunge wangesusia bunge kukazia msimamo wa chama kuliko nusu kukubali na nusu kutokubali.
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  wazo jepesi.
   
 9. P

  Pax JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Thinking yako ipo shallow sana na kabla hujaandika humu muulize mtu unachoandika kabla. Wabunge wamechaguliwa na wananchi ili wakapiganie na kutetea haki zao bungeni kwa hoja zenye mantiki. Watu wamelala vituoni kulinda kura zao halafu leo kirahisi tu wasihudhurie vikao?
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapan ni wazo zito na ndio kilichofanyika kule Zanzibar wawakilishi hakuhudhuria ufunguzi wa blw na vikao ili kuonyesha msisitizo wa kile walichokuwa wakikiamini! tofauti na chadema wamekimbilia kuwa kambi ya upinzani hii inaonyesha kuwa wapo kimaslahi zaidi kwa maana hakuna Bunge bila ya Rais na ndie mwenye mamlaka ya kulivunja na kusaini miswada.!
   
 11. sizy

  sizy Member

  #11
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  sina uhakika na ubongo wako, kwa sababu ukiandikacho sio sawa na unachokiamini
   
 12. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kichefuchefu.. unaongea mambo tofauti na thread iliyopo hapa
  na haujui maana halisi ya demokrasia na haiwezekani raisi aliyechaguliwa na NEC aongoze wanannchi
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Umasikini wa mawazo!!!!
   
 14. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Amkatae, amkubali, alie, acheke, ajinyonge - bado JK ni Rais wa JMT na Wabunge wa Chadema watafanya kazi chini ya JK kupitia serekali yao kivuli au watafanya na Slaa? Kuweni open minded wajameni msibishane na vitu ambavyo havihitaji degree kuving'amua.
   
 15. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  unapoongea mwanme halisi unamaanisha nini? kuna wanamme wengine sio halisi?:smile-big::smile-big:
   
 16. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  JK hajakataliwa na Dr Slaa kama individual bali ni wananchi walioibiwa kura ndiyo wanaomkataa JK.
   
 17. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Between the two evils choose the lesser one. Dr Slaa angekubali matokeo ama kumkubali Raisi angewakatisha sana tamaa washabiki wake. Hapa anataka kugain people sympathy kuonesha kwamba Ikifika mwaka 2015 atakuwa anadai "mwaka 2010 tulionewa kwani tulishinda, mwaka huu hatukubali". Hiyo itawafanya wananchi wamwonee huruma. Dr Slaa anajua siasa, Ila tu CCM pia tayari wapo makini na kaktika vikao vyao wameshapanga 2015 itakuwa ni kulinda kura na sio kuchakachua. Mchezo utakuwa mtamu!
   
 18. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  .....watafanya na Slaa eventually.
  Alichofanya jana Dr Slaa ni mwanzo tu wa kufikia huko....mwanzo wa ngoma ni lele!
  So Dr Slaa is on the right track!
   
 19. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Kama wako serious basi wasusie Bunge na posho za vikao wasamehe na hata mishahara ile minono wasichukue. Hiyo ni sacrifice ya kutosha kuwapatia nchi fika 2015
   
 20. b

  bob giza JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wee lazima ni nyumba ndogo ya jeikei uwe mdume au mdemu..i mean utakuwa mwehu tuu
   
Loading...