Wakuu, nimeona mjadala wa baraza la Congress la Marekani likiijadili Tanzania Jana na hapo hapo Leo ubaloz wa Tanzania umetoa statement ya kuonya wale woote watakaokuwa chanzo cha vurugu na kuharibu Uchaguzi.
Wakuu wale ni MABEBERU tujitahid Sana kukwepa uvunjivu wa haki wale wenzetu ukisikiliza Kwa makini utagundua kuwa wanafuatilia kila kinachopangwa na kinachofanyika na wanadata zooote kuunganisha na hii statement ya ubalozi tunatakiwa tujiangalie kuna mipango inapangwa Juu Ya wale watakao kuwa chanzo cha kuvuruga Uchaguzi Kwa kunyima haki za watu, angalia ile statements Ya Leo imesema Kwa kushirikiana na nchi za kidemocrasia watafikiria hatua stahiki, hilo neno ni kubwa na linaonesha kuwa kuna mipango mikubwa inapangwa na nchi nyingi za ulaya kutaka kumwadibu yoyote atakaekuwa chanzo cha kunyima haki Au kupora haki najua wapo watakaosema ah wapi ah wapi Lakini kumbuka kuwa, hata hizo Data za Uchaguzi mlizoziweka kwenye hiyo laptop yenu wanaziona na wao ndio wanaokurusu usiangalie na kuziedit
Mkiambiwa kuwa lisu ni mpango wa MUNGU muwe mnaelewa, kila mbabe na mbabe wake
Hivi mnajua hilo neno walilosema kuwa kwakushirikiana na nchi zenye democracy mnajua maaana yake? Wameishajipanga kumwadibu yoyote atakaepora haki, hivi nyie mnaijua ile kampuni Ya kisheria inayomsimamia lisu? Ile inamtandao kwenye nchi zote za ulaya na inaweza kushawishi chochote kwenye nchi yoyote na nyie hamjui kudhungu, wakiongea na watu wenye ushawishi Kwenye hizo nchi mtashangaaa mambo yanakuwa mambo haya endeleeni kusema kuwa msiponichagua.
Endeleeeni kusema kuwa ole wenu msiponichagua, wakuu msicheze na Yule Robert wa ile kampuni Ya kisheria Ya kimataifa, Yule ana Wateja wake ambao ni watoa maaamuz huko ulaya, ana Wateja wake ambao ni wajumbe kwenye vyombo vya maaamuzi huko ulaya na Marekani atawashawishi watapendekeza Halafu serikali zao zitabaki na issue ya utekelezaji huku mtaanza kukumbiana mmoja baada Ya mwingne mwisho mnajikuta mnaanza nilikuwa natekeleza sheria, Mara niliamlishwa na wakubwa Wangu, na mkumbuke kuwa wale wanaweza kuamua wakasema sisi tunamtambua fulani ndio rais wa Tanzania haya mtaenda wapi? Wakisema hivyo mtaenda wapi? Maanaa watakachofanya ni kukuondoa wewe Au kuelekeza misaada yoote Kwa huyo wanaemtambua.