Mnaoishi Mabwepande au Chanika na kufanya kazi Posta mnaamka saa ngapi ili kuwahi ofisini?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,283
2,043
Hakika kuishi DAR kuna RAHA na SHIDA Zake. Shida kubwa ya Kuishi Dar ni Umbali wa kutoka unapoishi na unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kama Mtumishi wa Umma anayeishi Mabwepande au Chanika na anafanyia shughuli zako Posta na unatakiwa kuripoti Ofisini saa 1.30 iwe una usafiri binafsi au wa Umma.

Je unapaswa kuamka saa ngapi?
 
Kwa gari binafsi, Chanika to Posta kukiwa na foleni kidogo au hamna kabisa ni saa 1 na nusu hivi.

Screenshot_20240212-142617.png


Ila foleni ikiwaka (rush hours) unaweza kutumia masaa 2 hadi mawili na nusu.

Hapo kwa private car.

Kwa usafiri wa umma hiyo topic nyingine.
 
Huo ujinga niligombana sana na marehemu mama yangu

Mama alikuwa ana nyumba Ukonga Banana na kazi alikuwa anafanya NMB Magomeni.

Mimi nilivyomaliza chuo nikapata ajira Muhimbili

Nilivyopata ajira nikataka kuhama mama akawa anakomaa tukae wote maana yeye ni mgonjwa na mimi ndio mwanae wa pekee..

Nikamshauri tupangishe nyumba yetu ya Ukonga kisha sisi twende tukapange appartment Magomeni ama Kariakoo maana gari aliyokuwa anatumia mafuta kila siku kutoka Ukonga kwenda Magomeni anaweka ya 15,000. Kwa mwezi mafuta tu yanamlia kama laki nne hivi na inamlazimu aamke alfajiri sana awai kazini. Sasa si bora hiyo laki 4 akalipe kodi Magomeni.

Akanionaa mimi mpuuzi sana kwamba kwa nini akapange wakati nyumba yake ameshajenga. Akaona kama namrudisha nyuma..

Angesikiliza huu ushauri wangu angeishi maisha mepesi sana. Kazini angekuwa anaenda kwa miguu tu, na anachelewa kuamka.
 
huo ujinga niligombana sana na marehemu mama yangu

mama alikuwa ana nyumba ukonga banana na kazi alikuwa anafanya NMB magomeni.

mimi nilivyomaliza chuo nikapata ajira Muhimbili

nilivyopata ajira nikataka kuhama mama akawa anakomaa tukae wote maana yeye ni mgonjwa na mimi ndio mwanae wa pekee..

nikamshauri tupangishe nyumba yetu ya ukonga kisha sisi twende tukapange appartment magomeni ama kariakoo. maana gari aliyokuwa anatumia mafuta kila siku kutoka ukonga kwenda magomeni anaweka ya 15000 kwa mwezi mafuta tu yanamlia kama laki nne hivi na inamlazimu aamke alfajiri sana awai kazini. sasa si bora hiyo laki 4 akalipe kodi magomeni

akanionaa mimi mpuuzi sana kwamba kwa nini akapange wakati nyumba yake ameshajenga . akaona kama namrudisha nyuma..

angesikiliza huu ushauri wangu angeishi maisha mepesi sana. kazini angekuwa anaenda kwa miguu tu, na anachelewa kuamka
Mbona umeandika ujinga?
 
Hakika kuishi DAR kuna RAHA na SHIDA Zake. Shida kubwa ya Kuishi Dar ni Umbali wa kutoka unapoishi na unapofanyia shughuli zako za kila siku. Km Mtumishi wa Umma anayeishi Mabwepande au Chanika na anafanyia shughuli zako Posta na unatakiwa kuripoti Ofisini saa 1.30 iwe una usafiri binafsi au wa Umma je unapaswa kuamka saa ngapi?
Kuna Watu tunaishi Mkuranga na tunapiga mzigo Posta halafu fresh tu tunawahi
 
Hakika kuishi DAR kuna RAHA na SHIDA Zake. Shida kubwa ya Kuishi Dar ni Umbali wa kutoka unapoishi na unapofanyia shughuli zako za kila siku. Km Mtumishi wa Umma anayeishi Mabwepande au Chanika na anafanyia shughuli zako Posta na unatakiwa kuripoti Ofisini saa 1.30 iwe una usafiri binafsi au wa Umma je unapaswa kuamka saa ngapi?
Chanika posta ni kilomita 35 unatakiwa auamke saa 10 alfajiri.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom