Sio sawa, sababu ni za kibaiolojia, google 'inbreeding' na madhara yake.
Katika jamii mambo yalikuwa categorized kuwa mabaya au mazuri kutokana na matokeo yake na experience.
Hata bila mwongozo wa dini au sayansi, jamii ziliweza kujua kipi ni kizuri na kipi ni kibaya kutokana na matokeo ya kitu hicho na experience zao.
Ndugu wakizaa, kuna uwezekano mkubwa wa watoto wao kuwa na matatizo makubwa ya kiafya na wengi wanakufa wakiwa wadogo.
Hivyo hata kabla ya dini, kwenye jamii nyingi duniani ilikuwa ni mwiko kwa ndugu wa damu kaoana, japo hawakuwa wanajua the exact science behind, lakini walikuwa na uwezo wa kuona matokeo na madhara yake.