Mnajua, kuna mtu anaweza asikupe pesa kwa sababu hana kwa wakati huo lakini akakupa ushauri wa maana wenye thamani mara 3 zaidi ya pesa uliomuomba?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
6,519
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania;

Hivi mnajua, kuna mtu anaweza asikupe pesa kwa sababu hana kwa wakati huo, lakini akakupa ushauri wa maana wenye thamani mara 3 zaidi ya pesa uliomuomba?

This is my true story
=========
Siku moja nikiwa chuo kikuu mwaka wa 2 nilipigiwa simu mida kama ya saa 3 usiku na kutaarifiwa juu ya ugonjwa wa mtoto wa dada yangu aliyekuwa anakaa mkoani iringa. Mtoto yule wa miaka 11 aligongwa na gari ndogo akiwa anatoka shuleni akirejea nyumbani.

Dereva alifanya tukio kisha akakimbia na gari yake. Kutokana na mapenzi niliyokuwa naye kwake nikakusanya nguo zangu haraka haraka nikasema kesho lazima nianze safari ya kutoka mkoa huu niliopo niende Iringa kwa ajili ya kumfariji dada yangu.

Nikiangalia katika wallet yangu nina 20,000/= na hiyo ndio nauli ya kwenda pamoja na kurudi Iringa. Nikajisemea kimoyomoyo, isiwe kesi, ngoja niende kwa uncle wangu akaniongezee mkwanja kisha asubuhi niondoke na gari ya saa 12:00 asubuhi.

Huyu jamaa nilikuwa ninamuita uncle kwa sababu yeye ni kabila moja tu kama mimi yaaani ni MJALUO wa Wilayani RORYA mkoa wa MARA na anafamiana sana na baba yangu kwa maana walicheza na kusoma wote ila tukaja kukutana mkoa huo nilioenda kusoma chuo.

Basi mimi huyoooo nikatoka zangu Hostel mpaka kwa uncle ambaye alikuwa anakaa mbali kidogo na nilipokuwa ninaishi mimi ila ni sehemu ya kutembea kwa miguu tu (walkable distance) kama mwendo wa 45 minutes hivi. Sawa bwana, nikaanza safari ya kwenda kwa uncle, nikafika salama nikamueleza yalinomsibu dada yetu yule pamoja na mtoto wake.

Uncle alipigwa na butwaa sana kwa maana anamjua sana yule mtoto kwa sababu wakati mama yake anajifungua miaka 11 iliyopita na yeye pia alikuwa Iringa kikazi. Baada ya kula chakula na kupiga stories mbili tatu basi uncle akaingia mfukoni akatoa elfu kumi kumi nne (40,000/=) kisha akanipa hivyo jumla nikawa na 60,000/=.

Daaah licha ya kupata support ya uncle bado pesa ikawa haitoshi kwa nauli ya kwenda, kurudi pamoja na pesa ya kumpa dada kama support katika kumuuguza mtoto. Kumbuka hapo mtoto amelazwa hospitali ya mkoa wa Iringa. Nikasema sawa ngoja niende tu hivyo hivyo huku nikiamini kwamba Mungu atafungua milango ya neema.

Sawa, nikasimama nikaanza kumuaga uncle kisha niondoke. Sasa wakati nimesimama nataka kuondoka uncle akaniangalia sana usoni kisha akaniambia uncle embu usiondoke kwanza, kaa hapo tuongee jambo moja dogo. Kumbe uncle alikwishaniona nilivyokuwa nina mawazo chungu nzima kichwani mwangu juu ya safari ya kesho.

Mazungumzo yakaanza awamu ya pili huku ucle akiniambia hivi, "mjomba, ninaomba uniwie radhi sana kwa kiasi hicho nilichokupa kwa maana biashara zangu na mimi zimeyumba sana sasa hivi.

Sasa uncle, badala ya wewe kufunga safari kwenda Iringa kesho asubuhi, kwanini usichukue hizo pesa zako kisha ukamtumia dada yako, zikamsaidia katika gharama za matibabu ya mtoto alafu wewe uje kwenda kumuona mtoto baada ya kufunga chuo? Kwa maana na mimi biashara zangu zitakuwa zimenyanyuka kidogo nitakupa nauli utaenda ukae huko likizo nzima.

Hapo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja" Nilimwambia uncle sawa, basi ngoja nikafikirie ushauri wako kisha nitaufanyia kazi. Basi yeye pia akakubali na sote tukaagana, mimi huuuyooo nikaondoka.

Baada ya kufika hostel nilitafakari sana ushauri ule wa uncle kabla ya kwenda kulala. Ilivyofika asubuhi kesho yake mimi huuuyooo mpaka Bank (kipindi hicho mobile money hakuna mdogo wangu acha kutoa macho na kujiuliza eti kwanini haukutuma kwa m-pesa au Tigo Pesa).

Nilimtumia dada zile pesa katika account yake, na hakika zilimsaidia sana na mpaka yeye akashukuru kweli (sipendi kumsaidia mtu kisha nikamtangaza kwa watu. Nimeamua kutangaza msaada niliompa dada yangu kwa maana ni sehemu ya mkasa. When helping the poor, please leave camera at home).

Mtoto alipona kisha nikaenda kumuona kwa msaada wa fedha ya nauli kutoka kwa uncle, ingawa mtoto alikuwa na makovu kadhaa mwilini, ila yaliendelea kupona taratibu taratibu.

Hakika uncle hakuwa na fedha ya kutosha kwa wakati ule lakini ushauri wake ulikuwa na thamani mara 3 kuzidi pesa niliyomuomba.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,281
2,000
Umesema kweli kabisa. Ila wabiongo wengi ukiwa haujiwezi kimaisha, lakini ukawasaidia ushauri ambao uliwasaidia, watakwambia ahsante ila kuanzia hapo popote watakapoenda watauchukua huo msaada na kumsingizia mtu fulani mwenye statasi kwamba ndiye aliwasaidia.

They won't refer to you again
 

tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
5,919
2,000
Nilichojifunza kwenye maisha yangu kuna baadhi ya wana familia bora usiwasaidie manake usoni na alivyo moyoni ni vitu viwili tofauti. Wanajifanya wanakupenda kumbe Simba wenye njaa.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 

sawima

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
2,720
2,000
Sasa hapo inategemea uelewa wa mtu watu wengine wana uelewa mdogo ukimpa ushauri badala ya fedha wataona hufai tu.
 

SOKIDODO

Senior Member
Apr 18, 2020
115
250
mkasa wako unafanana kabisa na wa dada yangu, tofauti ni wahusika tu na ni jinsi gani mtu unamsaidia, tunatofautiana uelewa baada ya kumsaidia mtu. kuna kipindi shem anakaa mbali na familia yake yalikua yanamkuta kama hayo,mtoto anaumwa na gharama ya hosptl inalingana na kiwango ulichonacho na ndo kiasi cha nauli ya kwenda na kurudi, anaamua utume fedha ili kusaidia matibabu, ila baade analaumiwa kwa kutokwenda kumuona mtoto akiwa anaumwa huku akisahau pesa aliyokua nayo alituma yote kusaidia matibabu. sasa unajiuliza kufika akiwa hana hela ni bora kuliko kutuma mtot atibiwe kwanz?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom