Je, ulishawahi kuokota mali au kitu cha mtu ukamrudishia mwenyewe?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,143
32,884
Habari za muda huu ndugu zanguni.

Mwaka fulani mida ya asubuhi wakati nikiwa kwenye harakati za kuusaka ugali nilidondosha pochi yangu.

Pochi yangu wakati inadondoka ilikuwa na pesa kiasi kama 90,000/= na vitambulisho na kadi zangu za benki na wakati naangusha nilikuwa naelekea benki ya NBC, iliyokuwa njia ya kuelekea quality center mkono wa kushoto ukitokea tazara.

Nilipogundua kuwa pochi yangu haikuwa na mimi hapo hapo nikageuka zangu na kurudi kuelekea kituo cha polisi ili kupata loss report kwa ajili vitambulisho vyangu.

Wakati nipo polisi najiandaa kutoa maelezo nikasikia simu yangu inaita kuangalia ni namba ngeni.

Nikaipokea na sauti ya upande wa pili ukanisalimia kiungwana na kuniuliza kuwa wewe ndio fulani. Nikamjibu ndio akasema yeye ameokota pochi yangu lakini ameshaelekea kariakoo kwenye eneo lake la kazi kwa baadae nikipata nafasi niende kuchukua.

Ni taarifa iliyo nishtua na kunipa mshangao mkubwa sana pamoja na wasi wasi ukizingatia nyakati hizi za sasa.

Yule polisi aliyekuwa anachukua maelezo yangu akauona mshangao wangu na mashaka yangu lakini akanishauri niende Tu hivyo hivyo.

Kwa kufupisha maelezo nilifika pale kariakoo maeneo ya msimbazi nikamkuta na kunipatia pochi yangu ikiwa na vitu vyangu vyote.

Nilipojaribu kutaka kumpatia chochote kitu kama asante yangu kwake alikataa na kujibu kuwa nikiipokea hii pesa wewe utasahau wema wangu na hutawafanyia wengine wema.

Tangu siku hiyo nimekuwa nikirudisha vitu au vifaa vingi ninavyookota kwa kuwatafuta wenyewe.

Je, wewe ulishawahi kuokota mali au kitu cha mtu na kumrudishia mwenyewe?
 
HIYO NDIO TABIA NJEMA.


Katika sheria ya Kiislamu, hukumu ya mali iliyopotea inategemea mazingira na hali maalum. Kuna mafundisho na mwongozo katika Qur'an na Hadith ambazo zinaweza kutumika kuelezea jinsi ya kushughulikia mali iliyopotea. Hapa kuna maelezo mafupi kuhusu suala hili:​
  1. Kuifanya Juu: Muislamu anapaswa kujitahidi kuitafuta mali iliyopotea na kuipeleka kwenye mahali pa umma au kwa mamlaka husika ili mwenyewe au mmiliki wa mali aweze kuipata.​
  2. Kuifadhi Mali: Ikiwa mtu anapata mali iliyopotea, ni jukumu lake kuitunza na kuilinda hadi mmiliki arudi kuichukua. Hii inaweza kuhusisha kuihifadhi mahali salama au kuipeleka kwenye mahali pa umma.​
  3. Kuitangaza: Inashauriwa kutoa tangazo la mali iliyopotea, ikiwezekana, ili kuwawezesha watu kutambua mali hiyo na kuitambulisha mmiliki wake.​
  4. Kuipatia Haki Yake Mmiliki: Ikiwa mmiliki wa mali au mtu aliyepoteza mali anaweza kuthibitisha umiliki wake, basi inapaswa kurudishwa kwake.​

Hadith pia zinatoa mwongozo zaidi kuhusu suala hili. Kwa mfano, kuna Hadith inayosema kwamba "yeyote atakayepata mali iliyopotea na kuitafuta mmiliki wake halafu akairudisha, atapata thawabu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu." Hii inathibitisha umuhimu wa kuwa mwema na waaminifu katika kushughulikia mali iliyopotea.

Mafundisho haya yanategemea kanuni za haki na uwajibikaji katika Uislamu. Kwa kufuata kanuni hizi, Waislamu wanashauriwa kuwa waadilifu na wema wanaposhughulikia mali iliyopotea ili kuhakikisha haki inazingatiwa. Ni muhimu kuzingatia pia muktadha wa jamii na sheria za nchi husika, kwani mazingira yanaweza kutofautiana.​
 
Mimi mara nyingi sana nimewahiokota simu,pesa taslimu(nilimuona aliyedondosha)na nikarudisha kwa wenye navyo na pesa kukosewa kuja kwangu mara nyingi na naiacha mpaka mwenye nayo aichukue.
Huwa naamini kitu hicho kilikuwa msaada mkubwa kwa mwenye nacho na huenda ndicho pekee alichokuwa nacho,hivyo kuchukua kwangu hakutanipa baraka bali laana.
 
Back
Top Bottom