Mna Nini Ndani ya Kitabu cha Sheikh Ponda?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,848
30,189
MNA NINI NDANI YA KITABU CHA SHEIKH PONDA?

Ili kitabu kiwe kitabu lazima kiwe na elimu mpya yaani ile ambayo jamii haijui.

Hii elimu mpya ndiyo roho, moyo na maisha ya kitabu kwani kitabu kina maisha na kifo kama binadamu.

Kitabu kikikosa vitu hivyo kinaweza kufa mapema au kikafa katika kuzaliwa yaani kitabu kinaingia katika mzunguko tayari kisha kufa.

Katika miaka ya hivi karibuni kuanzia mwaka wa 2010 Tanzania imeshuhudia kuchapwa vitabu muhimu sana vya historia.

Kitabu cha kwanza kilikuwa, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' cha Dr. Harith Ghassany (2010), ''Mimi Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar,'' cha Hashil Seif (2017), ''Maisha Yangu Miaka Minane Ndani ya Baraza la Mapinduzi Khaini au Mhanga wa Mapinduzi?'' Khamis Abdullah Ameir (2022).

Hivi ni vitabu kuhusu historia ya Zanzibar.
Nashukuru kuwa nimehusika katika vitabu hivyo vyote hapo juu kwa njia moja au nyingine.

Tanzania Bara waandishi wa vitabu vilivyochapwa kuhusu historia ya Tanganyika ni ''My Life My Purpose,'' cha Benjamin William Mkapa (2019) na ''Julius Nyerere A Biography,'' kitabu kilichaondikwa na Issa G. Shivji, Saida Yahya Othman na Ngwa'nza Kamata (2021) kuhusu maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; na kitabu cha maisha ya Ali Hassan Mwinyi, ''Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu,'' (2021).

Vitabu hivi sikuhusika moja kwa moja ukikitoa kitabu cha Julius Nyerere.

Lakini mengi katika vitabu hivyo nikayajua kiasi cha kuweza kufahamu wapi kalamu haikuandika sawasawa kwa sababu hii au ile.

Vitabu vyote hivi vinahusu historia ya Tanzania na serikali yake. ambayo marais hawa waliongoza.

Kwa bahati mbaya sana waandishi wa vitabu hivi wamejifanyia uhariri mkubwa katika tatizo la Waislam kama kundi la raia ambayo serikali imekuwa kama vile inawatazama kwa jicho lililojaa hofu.

Ukisoma vitabu hivi vyote unatoka na picha ya kuwa Tanzania ni nchi yenye utulivu mkubwa kama wanavyosema watawala walio madarakani na ndiyo walioshika serikali, Tanzania ni kisiwa cha amani.

Hivi ndiyo alivyosema Benjamin William Mkapa na Ali Hassan Mwinyi kadhalika.

Mwalimu Nyerere yeye hakuandika kitabu cha maisha yake.

Matatizo haya ya ubaguzi wa dini kwa hakika yalianza wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza Mwalimu akiwa kwanza Waziri Mkuu wa Tanganyika, kisha Rais wa Tanganyika na mwishowe Rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya kuaga aliyotoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 anasema yeye aliondoa upogo baina ya Waislam na Wakristo.

Kwa hiyo marais wote waliofuata baada yake ndiyo kusema wamerithi nchi iliyokuwa haina ubaguzi kwa misingi ya dini.

Kwa ajili hii basi Marais hawa waliokuja baada yake hawakuwa na cha kurekebisha.

Hapa ndipo kinapoingia kitabu cha Sheikh Ponda, ''Juhudi na Changamoto.''

Sheikh Ponda anaingia vipi katika orodha hii ya vitabu vinavyowahusu marais watatu waliotawala Tanzania?

Kitabu cha Sheikh Ponda kinapingana na vitabu vyote vitatu vya marais hawa kwa kutoa picha halisi ya ukweli ulivyo toka uhuru upatikane.

Mbali ya maisha yake mwenyewe katika kupigania haki za Waislam, Sheikh Ponda ndani ya kitabu hiki chake anaeleza namna gani taasisi za serikali zinavyofanyakazi pale wanapokabiliana na Waislam na pale wanaposhughulika na raia wengine.

Ukizisoma kurasa hizi Sheikh Ponda anavyoeleza yaliyomfika kwa kupigania haki za Waislam yatakutoka machozi.

Mwanzo wa kitabu Sheikh Ponda anaeleza juhudi za Waislam katika kupata elimu na anahitimisha kwa kuweka wazi kwa ushahidi namna Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) lilivyokuwa linahujumu juhudi hizi.

Sheikh Ponda anaeleza katika kitabu chake juhudi zilizotumika kupata ushahidi wa dhulma hii na kufikisha ushahidi kwa vyombo vinavyohusika ili haki itendeke.

Baada ya kuona juhudi za Waislam zinapuuzwa Sheikh Ponda aliitisha maandamano ambayo serikali iliyapiga marufuku.

Sheikh Ponda hakukubali.

Katika Msikiti wa Kichangani baada ya Sala ya Ijumaa Sheikh Ponda alisimama kuzungumza na Waislam kuhusu umuhimu kwa kutoa hofu katika nyoyo zao na kuwataka waanandamane katika maandamano ambayo yeye atakuwa mbele kuyaongoza.

Nilikuwapo hapo msikitini siku ile nimekaa chini ya miguu ya Sheikh Ponda napiga picha na kurekodi yote aliyokuwa anasema yeye akiwa kasimama mbele yangu.

Alipomaliza kuzungumza na Waislam Sheikh Ponda aligeuka akaangalia kibla kisha akanyanyua mikono yake juu kuomba dua.

Kama siku ile mwaka wa 1998 Sheikh Ponda alipotusalisha Msikiti wa Mwembechai Sala ya Maghrib akawaliza Waislam ndani ya sala hali ilirijudia Msikiti wa Kichangani mwaka wa 2012.

Waislam wake kwa waume walitokwa na machozi.

Waislam waliandamana kama vile askari waliokuwa nje ya msikiti na silaha za kutisha na mavazi ya mapambano hawapo.

Askari wale hawakuwashambulia Waislam na maandamano yakafanyika na kama aivyowaahidi Waislam Sheikh Ponda alikuwa mbele akiyaongoza maandamano.

Huyu ndiye Sheikh Ponda aliyenyanyua kalamu kueleza hali ya nchi yetu ilivyo.

Kitabu hiki ni kitabu muhimu kwa kila Mtanzania anaeitakia nchi yetu amani ya kweli kukisoma.

1661798793462.png
1661798851026.png
 
Uamsho mpaka waamshwe ndio waamke wajue wanafanya nini sasa unatakaje kitu kipya kwa waliolala ndugu yangu.
 
Kwa maoni yangu mimi sidhani kama Tanzania kuna Ubaguzi dhidi ya Uislamu/Waislamu kwanza ni kinyume chake, nasema hivyo kwa maana Uchumi karibia wote wa Tanzania umeshikwa na Waislamu, Matajiri wote wakubwa Tanzania ni Waislamu, leo hii kama mtu anatafuta kazi Ofisi binafsi uwezekano wa kuomba kazi kwa Muislamu ni mkubwa sana karibia 90% sasa ni ubaguzi gani huo wa Uislamu/Waislamu unaoungelea? Au ndio ile wanaita reverse psychology inatumika?

Labda kama Muislamu mweusi anabaguliwa na Waarabu au Wahindi kwa maana ndiyo wenye Uchumi wa nchi, sasa sielewi Muislamu atabaguliwa vipi Tanzania?
 
MNA NINI NDANI YA KITABU CHA SHEIKH PONDA?

Ili kitabu kiwe kitabu lazima kiwe na elimu mpya yaani ile ambayo jamii haijui.

Hii elimu mpya ndiyo roho, moyo na maisha ya kitabu kwani kitabu kina maisha na kifo kama binadamu.

Kitabu kikikosa vitu hivyo kinaweza kufa mapema au kikafa katika kuzaliwa yaani kitabu kinaingia katika mzunguko tayari kisha kufa.

Katika miaka ya hivi karibuni kuanzia mwaka wa 2010 Tanzania imeshuhudia kuchapwa vitabu muhimu sana vya historia.

Kitabu cha kwanza kilikuwa, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' cha Dr. Harith Ghassany (2010), ''Mimi Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar,'' cha Hashil Seif (2017), ''Maisha Yangu Miaka Minane Ndani ya Baraza la Mapinduzi Khaini au Mhanga wa Mapinduzi?'' Khamis Abdullah Ameir (2022).

Hivi ni vitabu kuhusu historia ya Zanzibar.
Nashukuru kuwa nimehusika katika vitabu hivyo vyote hapo juu kwa njia moja au nyingine.

Tanzania Bara waandishi wa vitabu vilivyochapwa kuhusu historia ya Tanganyika ni ''My Life My Purpose,'' cha Benjamin William Mkapa (2019) na ''Julius Nyerere A Biography,'' kitabu kilichaondikwa na Issa G. Shivji, Saida Yahya Othman na Ngwa'nza Kamata (2021) kuhusu maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; na kitabu cha maisha ya Ali Hassan Mwinyi, ''Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu,'' (2021).

Vitabu hivi sikuhusika moja kwa moja ukikitoa kitabu cha Julius Nyerere.

Lakini mengi katika vitabu hivyo nikayajua kiasi cha kuweza kufahamu wapi kalamu haikuandika sawasawa kwa sababu hii au ile.

Vitabu vyote hivi vinahusu historia ya Tanzania na serikali yake. ambayo marais hawa waliongoza.

Kwa bahati mbaya sana waandishi wa vitabu hivi wamejifanyia uhariri mkubwa katika tatizo la Waislam kama kundi la raia ambayo serikali imekuwa kama vile inawatazama kwa jicho lililojaa hofu.

Ukisoma vitabu hivi vyote unatoka na picha ya kuwa Tanzania ni nchi yenye utulivu mkubwa kama wanavyosema watawala walio madarakani na ndiyo walioshika serikali, Tanzania ni kisiwa cha amani.

Hivi ndiyo alivyosema Benjamin William Mkapa na Ali Hassan Mwinyi kadhalika.

Mwalimu Nyerere yeye hakuandika kitabu cha maisha yake.

Matatizo haya ya ubaguzi wa dini kwa hakika yalianza wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza Mwalimu akiwa kwanza Waziri Mkuu wa Tanganyika, kisha Rais wa Tanganyika na mwishowe Rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya kuaga aliyotoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1984 anasema yeye aliondoa upogo baina ya Waislam na Wakristo.

Kwa hiyo marais wote waliofuata baada yake ndiyo kusema wamerithi nchi iliyokuwa haina ubaguzi kwa misingi ya dini.

Kwa ajili hii basi Marais hawa waliokuja baada yake hawakuwa na cha kurekebisha.

Hapa ndipo kinapoingia kitabu cha Sheikh Ponda, ''Juhudi na Changamoto.''

Sheikh Ponda anaingia vipi katika orodha hii ya vitabu vinavyowahusu marais watatu waliotawala Tanzania?

Kitabu cha Sheikh Ponda kinapingana na vitabu vyote vitatu vya marais hawa kwa kutoa picha halisi ya ukweli ulivyo toka uhuru upatikane.

Mbali ya maisha yake mwenyewe katika kupigania haki za Waislam, Sheikh Ponda ndani ya kitabu hiki chake anaeleza namna gani taasisi za serikali zinavyofanyakazi pale wanapokabiliana na Waislam na pale wanaposhughulika na raia wengine.

Ukizisoma kurasa hizi Sheikh Ponda anavyoeleza yaliyomfika kwa kupigania haki za Waislam yatakutoka machozi.

Mwanzo wa kitabu Sheikh Ponda anaeleza juhudi za Waislam katika kupata elimu na anahitimisha kwa kuweka wazi kwa ushahidi namna Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) lilivyokuwa linahujumu juhudi hizi.

Sheikh Ponda anaeleza katika kitabu chake juhudi zilizotumika kupata ushahidi wa dhulma hii na kufikisha ushahidi kwa vyombo vinavyohusika ili haki itendeke.

Baada ya kuona juhudi za Waislam zinapuuzwa Sheikh Ponda aliitisha maandamano ambayo serikali iliyapiga marufuku.

Sheikh Ponda hakukubali.

Katika Msikiti wa Kichangani baada ya Sala ya Ijumaa Sheikh Ponda alisimama kuzungumza na Waislam kuhusu umuhimu kwa kutoa hofu katika nyoyo zao na kuwataka waanandamane katika maandamano ambayo yeye atakuwa mbele kuyaongoza.

Nilikuwapo hapo msikitini siku ile nimekaa chini ya miguu ya Sheikh Ponda napiga picha na kurekodi yote aliyokuwa anasema yeye akiwa kasimama mbele yangu.

Alipomaliza kuzungumza na Waislam Sheikh Ponda aligeuka akaangalia kibla kisha akanyanyua mikono yake juu kuomba dua.

Kama siku ile mwaka wa 1998 Sheikh Ponda alipotusalisha Msikiti wa Mwembechai Sala ya Maghrib akawaliza Waislam ndani ya sala hali ilirijudia Msikiti wa Kichangani mwaka wa 2012.

Waislam wake kwa waume walitokwa na machozi.

Waislam waliandamana kama vile askari waliokuwa nje ya msikiti na silaha za kutisha na mavazi ya mapambano hawapo.

Askari wale hawakuwashambulia Waislam na maandamano yakafanyika na kama aivyowaahidi Waislam Sheikh Ponda alikuwa mbele akiyaongoza maandamano.

Huyu ndiye Sheikh Ponda aliyenyanyua kalamu kueleza hali ya nchi yetu ilivyo.

Kitabu hiki ni kitabu muhimu kwa kila Mtanzania anaeitakia nchi yetu amani ya kweli kukisoma.

Huyu shkh isa Ponda namkumbali sana, ni miongoni mwa viongozi wa waislamu wa chache wanao jitambua, na wako tayari kusema ukweli na kufia dini yao bila uoga sio mnafiki huyu shkh.

Waislamu wame tengwa sana katika mfumo yetu ya elimu na utawala kanisa imepewa kipao mbele kutuchagulia watawala kwa kupitia elimu ya shule zao kiujanjaujanja, na ni waislamu wachache wenye uwezo wa kugundua hili, wenzetu wengi weme fudishwa kuchukia waislamu hata bila sabb.
 
Upotoshaji.

Toa mfano ni kwa namna gani kanisa linachagua watawala.

Toa mfano waislamu wametengwa .
 
Waislam acheni kulialia bila sababu za msingi

Hii nchi inatambua uwepo wa dini, lakini haiongozwi na misingi ya kidini
 
Mkorea...
Zipo mada za utani ukatumia lugha za utani za maneno "lialia."

Hii si mada ya maskhara.
 
Upotoshaji.

Toa mfano ni kwa namna gani kanisa linachagua watawala.

Toa mfano waislamu wametengwa .
Randy,
Rais Mkapa aliomba ushahidi wa tatizo hili.
Prof. Hamza Njozi akaandika kitabu ''Mwembechai Killings...'' (2002).

Serikali ikakipiga marufuku.
 
Dini zisitumike vibaya. Tufanye harakati za kisiasa na si za kidini. Imani ni kitu sensitive, kusifanyike allegations zozote ambazo haziwezi kuthibitishwa, tuache kuigawa jamii.
 
Mix...
Ushahidi upo na ulipotolewa Rais Mkapa aliyeutaka ushahidi alipata mshtuko mkubwa.

Uamuzi ukawa ushahidi usiachwe ukasomwa.

Kitabu kilichokuwa na ushahidi huo, ''Mwembechai Killings...'' kilichoandikwa na Prof. Hamza Njozi kikapigwa marufuku.
 
Rest mzeebaba nobody takes you seriously hata waislam wenzako hawaelewi hii chuki na propaganda unayo ihubiri Kila siku. Miwani ya udini gives you blurred vision huoni kitu with an open mind. Give it a rest, nobody cares.
 
Huyu mzee ni wa kupuuzwa. Hata waislamu wenzie wameshampuuza siku nyingi sana. Hizi harakati zake zimekosa mashiko sana. Tumuheshimu kama binadamu lkn tumpuuze kwa kuwa ana ombwe kubwa la ubaguzi na chuki za wazi za kidini. Huyu ban ya milele inamuhusu.
 
I'm glad hizi propaganda zake fall on deaf ears.
 
Rest mzeebaba nobody takes you seriously hata waislam wenzako hawaelewi hii chuki na propaganda unayo ihubiri Kila siku. Miwani ya udini gives you blurred vision huoni kitu with an open mind. Give it a rest, nobody cares.
Bufa...
Una haki na fikra zako.
Sina chuki wala sifanyi propaganda.

Sikiliza Khutba ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Mtoro Post #13 itakufikirisha.
 
Huyu mzee ni wa kupuuzwa. Hata waislamu wenzie wameshampuuza siku nyingi sana. Hizi harakati zake zimekosa mashiko sana. Tumuheshimu kama binadamu lkn tumpuuze kwa kuwa ana ombwe kubwa la ubaguzi na chuki za wazi za kidini. Huyu ban ya milele inamuhusu.
Tai...
Tembelea Post # 13.

Wiki mbili zilizopita nimechaguliwa Mwanachama Bora JamiiForums wewe unazungumza nipigwe ban.
 
Mzee Mohamed Said jaribu kubadirisha fikra zako achana na fikra za mwaka 47.
Hii nchi haina udini hii nchi ni ya wote wenye dini na wasio na dini.
Huo upendeleo unaoutaka utaupata only Arabuni.
Muislam mwenzako Jakaya Kikwete aliwahi sema "Waislam ni km watoto wa kambo muda wote ni kulialia kuonewa"
Zeeka kwa amani mzee wangu,
Wakati wewe ukilalamika huku mitaani tunakula pamoja na kuoana bila shida.
Kwaheri!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom