MMU nimefiwa

MMU nimefiwa

Mama wa rafiki yangu wa kufa na kuzikana amefariki wapendwa. Ni my childhood best friend ambae siwezi kuelezea urafiki wetu kwa maandishi. Yani huyu mkaka ambae mama ake amefariki tulipendana sana kama ndugu wa damu, hatukuwahi hata kuwa wapenzi japo wengi walihisi sisi ni wapenzi. Naugulia tu hapa, niko mbali kwenda kuzika sitaweza nimebaki na majonzi hata kazi hazifanyiki tena. Uwiii hapa sina hata wa kunibembeleza mwenzenu, huku niliko sina hata ndugu.
Nimeona hata niandike hapa nipunguze msongo huenda nitapata ahueni.

Pole sana mdada!!
 
TULIZA MOYO tenda mema aliyokusihi TIME WAITS FOR NO ONE
 
nimechelewaaaa.. but BE STRONG Mrembo nature. Imeshatokea na hauwezi kuubadili ukweli. RIP mama.
 
Last edited by a moderator:
Yes ni my brother. Kwa kweli inaumiza moyo sana hasa pale unapofikiria kuhusu mahangaiko ya maisha na suala la familia. Joseph ameenda. Mkewe na watoto wako hospital.. Tunatarajia kumpumzisha katika nyumba yake ya milele baadaye leo mchana.{Jumatano tarehe 10/04}.

Pole sana Nicas Mtei ....
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu, sisi sote ni wa njia moja. Mbele yetu nyuma yake.
 
Pole mrembo, rip mama
Jamani asanteni
woote angalau najiona wepesi kidogo, huyu ni kama mama yangu mzazi,
imeniuma sana siwezi elezea kushindwa kuwepo na kumfariji rafiki yangu
mpendwa na kipindi hiki kigumu cha msiba wa mama.
 
Pole sana kwa msiba huo mkubwa. Mungu awepo moyo mkuu na uvumilivu kipindi hiki kigumu

Faraja: Kwa kuwa wa kukuzika bado yeye yuko hai, usiumie sana. Jipe moyo, urafiki wenu bado utaendelea kudumu
 
Pole Nicas na wafiwa wote. Mungu alitoa na ametwaa Jina lake libarikiwe

Pole sana. Nami nipo katika wakati mgumu sana kwa wiki hii. Nimeondokewa na wapendwa wawili kuanzia jumapil had leo.
Wa kwanza ni kaka yangu Anaitwa Joseph Rweyemamu {Mtoto wa mama mkubwa}. Amefariki kwa ajali ya gari Kahama.. Mwingine ni rafiki yangu Kipenzi. Anaitwa Elizabeth {Wakyo} Mkongwe.. Kwa kweli imekuwa week ya huzuni sana kwangu.. Vifo vya vijana hao waliokuwa wanaanza kupata maendeleo ktk maisha yao vimefanya niyafikirie maisha katika namna ya tofauti na isiyoelezeka..

R.I.P Luteni Joseph Rweyemamu.
R.I.P Elizabeth 'Wakyo'Mkongwe.

I will always love and miss u wapendwa wangu..
 
Nataka nikutumie rambi rambi itafikaje?
 
Kwa Mara nyingine tena nawashukuru kwa faraja mnayoendelea kunipatia, binafsi najua ni namna gani mmekuwa na mguso moyoni mwangu!mbarikiwe sana wote....nimeshindwa kutaja mmoja mmoja na kujibu! mazishi yalifanyika Same mashariki Jana! Tuzidi kuiombea hii familia na Baba ambae sasa ni mgane.
 
Back
Top Bottom