MMU nimefiwa

MMU nimefiwa

Pole kwa msiba ndugu!
Kwa Mara nyingine tena nawashukuru kwa faraja mnayoendelea kunipatia, binafsi najua ni namna gani mmekuwa na mguso moyoni mwangu!mbarikiwe sana wote....nimeshindwa kutaja mmoja mmoja na kujibu! mazishi yalifanyika Same mashariki Jana! Tuzidi kuiombea hii familia na Baba ambae sasa ni mgane.
 
Mama wa rafiki yangu wa kufa na kuzikana amefariki wapendwa. Ni my childhood best friend ambae siwezi kuelezea urafiki wetu kwa maandishi. Yani huyu mkaka ambae mama ake amefariki tulipendana sana kama ndugu wa damu, hatukuwahi hata kuwa wapenzi japo wengi walihisi sisi ni wapenzi. Naugulia tu hapa, niko mbali kwenda kuzika sitaweza nimebaki na majonzi hata kazi hazifanyiki tena. Uwiii hapa sina hata wa kunibembeleza mwenzenu, huku niliko sina hata ndugu.
Nimeona hata niandike hapa nipunguze msongo huenda nitapata ahueni.

pole sana. mpe pole na yeye.
 
pole sana msiba unakuhusu sana huo daaa
 
Back
Top Bottom