Mmm, eti Paja na Firigisi Vya Baba. . .

Mmm, eti Paja na Firigisi Vya Baba. . .

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
35,987
Reaction score
24,232
Adabu za kizamani kwa baadhi ya maeneo ilikuwa ni pamoja na watoto kutokula vyakula fulani fulani
Vyakula hivyo ilikuwa ni kwa ajili ya baba mwenye nyumba au watu wazima

Kule nitokako ilikuwa paja na kuku au kichwa cha samaki ilikuwa kwa ajili ya baba mwenye nyumba
Kuna wengine paja na firigi ilikuwa ni kwa ajili ya baba mwenye nyumba pia

Nakumbuka kuna hg aliwhi fukuzwa kwa jirani kisa alionja firigisi bila kujua umuhimu wa firigisi kwa familia hiyo, aliyaaga mashindano pale pale.

Binafsi nina kijana mmoja asipokula paja hali kitu kingine, na wala halalamiki, ni kuwa anapenda paja japo ni mdogo. Na mie huwa sioni kwa nini asile apendacho. Ni kama mie nipendavyo miguu ya kuku na kwato zake, naskia kweli nimekula.

Sasa huwa napata wasi wasi, je kijana huyu siku akienda kwa watu si ataonekana hana adabu?
Labda anaweza jisahau akala paja afu ukakuta kumbe kala roho ya baba mwenye nyumba??

Hizi zile adabu za mtoto hali hiki kama wakubwa wapo au mwanamke hali hiki kama wanamme wapo, bado zinalipa kweli? Na zinaweza kukuondoa katika kundi la wastaarabu?

Hebu nisaidieni kabla sijaharibu watoto nyumbani kwa kuwapa uhuru wa kula watakavyo.
 
umeamkaje asali ya ODM? kwema utokako?? ngoja waje wenye miiko, mie kwangu kila mtu aweza kula chochote!
 
Last edited by a moderator:
AHAAAAA Kongosho SISI KWETU BABA ANAPEWA PAJA KIDARI NA FIRIGISI
SIKU HIZI DUNIA IMECHANGE CHAKULA KINAWEKWA MEZANI WANAITA SELF SERVICE UKICHELEWA HATA HOUSEGIRL ANAPAKUWA KIDARI ...EHEHEEEE
KUKU BWANA MIDA YA KUPAKUA UTATA SIO KIDOGO
 
Last edited by a moderator:
Paja, kidari na firigisi sasa watoto watabaki na kwato tu?


Afu hii ukii-zoom sana ndio unakuta hata wanawake wanaokwenda kukata kilaji bar wanaonekana hawana adabu.
Au ukikuta mwanamke kanunua konyagi yake, utaskia huyu naye kama janaume tu, basi anavuliwa ustaarabu woote.

Hivi hata sigara si chakula tu?

AHAAAAA KongoshoSISI KWETU BABA ANAPEWA PAJA KIDARI NA FIRIGISI
SIKU HIZI DUNIA IMECHANGE CHAKULA KINAWEKWA MEZANI WANAITA SELF SERVICE UKICHELEWA HATA HOUSEGIRL ANAPAKUWA KIDARI ...EHEHEEEE
KUKU BWANA MIDA YA KUPAKUA UTATA SIO KIDOGO
 
baba anamajukumu mengi likiwemo la kuongeza ukubwa wa familia so mwacheni ale vizuri.
 
Aisee Kongosho, hatupaswi kukaa mimi na weye aisee; maana hiyo supu ya miguu itatukosanisha. LOL

Mwangu zamani alikuwa anapenda bastola (wing/kipapatio) siku hizi ni paja tu. Kwangu msichana wa kazi ndio anakula paja (mwanangu asipokuwepo) mimi ni miguu (coz of supu) na kidali (white meat) tu.
 
Last edited by a moderator:
Kwetu nyumba nzima baba, watoto( tumefata kwa baba) na beki tatu twala Mapaja tuuu, nyama zengine hatuzitaki katuuuuu. Mama Lara tu ndo anapenda vinyama vidogo vidogo kama shingo, vipapatio na mgongo. Kuondoa purukushani ya mipaja tunanunua kuku MAPAJA TUPU pale shoprite. Basi hapo kila mtu na MPAJA wake, tambarareeeeee.
 
Paja, kidari na firigisi sasa watoto watabaki na kwato tu?


Afu hii ukii-zoom sana ndio unakuta hata wanawake wanaokwenda kukata kilaji bar wanaonekana hawana adabu.
Au ukikuta mwanamke kanunua konyagi yake, utaskia huyu naye kama janaume tu, basi anavuliwa ustaarabu woote.

Hivi hata sigara si chakula tu?
AHAAAA ndo ivo kongosho yaani inakuwa kama kuku kachinjwa kwa ajili yake tu
mimi nilikuwaga namind kweli kweli
watoto tulikuwa tunafaidi damu ,na miguu na kichwa
nimemiss damu ya kuku kweli ile supu yake balaa!
 
mhh! nilipoona heading nilijua mama Kongosho anaongelea mambo ya 18+ lol. sie kwetu hatuna hayo mambo, as long as hatumwekei shingo au vimikono kwenye hotpot all is okay. I'm suprised kusikia hii ni issue sehemu zingine since sijaona kwenye nyumba nilizokaa. kuhusu how kuwalea wanao wawe na 'adabu' just fahamu utaratibu wa sehemu unayotaka kwenda/kuwapeleka and hakutakuwa na shida.

edit: kuongezea at times dad huja na nyama yake personal for him ambayo wengine hatuili like kongoro, kichwa etc
 
Siku hizi mambo hayo hakuna kabisa na kama yamebaki basi ni kwa familia chache sana ambazo madingi wa long time bado wapo.
 
hili swala linatokeaga tu kutokana na mama kumpendelea baba ale kitu fulani,hivyo unakuta ni kama rule,mara nyingi wababa huwapa watoto wao wadogo,ili na wao wafurahi...........swala lingine ni ile siti ya mzee kwenye dining table,unakuta baba anakaa sehemu hiyohiyo,na akiwepo hamna anayekaa pale,hilo ndo nashindwa kuelewa.
 
Yeah_kwetu ni mwiko mwanamke au asiye mwenye boma kula hiyo firigisi mpaka sasa,..nimeoa asiye kabila langu kila siku ugomvi kuhusu hii kitu_maake sitaki kabisa ale mwingine zaidi yangu.....banyambala juuuuuuuuuuuu
 
Siku hizi Konnie, kuku anauzwa kulingana na unachohitaji...ukitaka kilo moja ya shingo utapata, kadhalika firigisi, paja, kongosho za kuku n.k n.k.....ila mie huwa napenda supu ya **** la kuku, pale ambapo huwa panaota manyoya ya mkia...
 
Kuna hg alifukuzwa kazi kisa kala kile KIMKIA CHA KUKU (juu ya SABURI la kuku); kumbe kile kimnofu ndiyo uilkuwa ugonjwa wa Baba Mwenye Nyumba; kila kuku akichinjwa firigisi na hicho KIMKIA anawekewa!!!!! Bahati mbaya hg naye alikuwa anakipenda KIMKIA saaana....Alipewa onyo mara mbili; mara ya tatu kilipopotea na AJIRA YAKE IKATOWEKA!!!!

Nyama ya kuku bado kuna baadhi ya familia ni KITU KIKUBWA NA KINA PROTOCAL ZAKE KATIKA KULIWA!!!!!
 
Siku hizi mambo hayo hakuna kabisa na kama yamebaki basi ni kwa familia chache sana ambazo madingi wa long time bado wapo.
Nani kakwambia yameisha? Mimi mwenyewe nina about 30yrs ila wife akipika cha kwanza kabisa kuniwekea ni firigisi na anajua nisipoikuta patachimbuka bila jembe...kuhusu vidali na makalio ya kuku hayo hayanisumbui kabisa. anakula watoto pamoja na mtoto mkubwa yaani my wife!
 
But kwanini makalio ni ya mama?
 
Mmmm!mila hizi sikukutana nazo sijui ingekusje nnavopenda mapaja lol!
 
Back
Top Bottom