Mmiliki wa mabasi ya J4 apiga wawili kwa risasi

Hii tabia imeanza kushamiri yaani unamdai mtu hela nyingi unapoanza kudai hupewi ukitumia lugha kali mdaiwa anakuuwa.
Kwa hiyo mtu asidai haki yake? Imekuwa kama seamans waliokuwa wanafanya kazi meli za ugiriki jamani?
 
Waliouawa ni Ali Mohamedi na Claudia Sikarwanda.Star TV imeripoti kuwa mmiliki wa mabasi ya J4 Bwn.Juma Mahende amewapiga wafanyabiashara wenzake wawili kwa risasi mbele ya ofisi yake na kufariki papohapo.Hatari hii imetokea Mwanza.Jeshi la polisi limemkamata na kumtia ndani muuaji.Kamanda wa polisi wa Bwn.Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hili.Ndugu wa marehemu wanasema jamaa waliouawa na muuaji walikuwa wanadaiana 25Milion.Inashangaza na kuhudhunisha kama haya yanaweza kutokea Tanzania.Roho za wapenzi wetu(hata kama wana makosa) zinapotea kwa namna ya kikatili.Cha ajabu usishangae kukutana mitaani na muuaji akiwa huru.

Ni vigumu Kwa tajiri kuingia mbinguni, kama ngamia katika tundu la sindano. Na utajiri wote huo anaua Kwa milioni 25 na kupoteza mabilioni ya biashara zake! Kweli neno linasema kutajirika Kwa mtu mwovu ni Kwa uharibifu wake mwenyewe. Sasa ngoja polisi wamle mpaka wajenge nyumba, na mabasi yake yamefikia ukomo, amefarakana na utajiri
 
Huyu J4 ni mhuni sana, kawapa watu wengi sana simu yangu akiwaambia ndio namba yake ili akipigiwa nijibu mimi.

Kama huko Butimba hakuna nafasi mleteni Keko ale nyasi na mawaziri wastaafu.

BURE KABISA
 
Utajiri haumfai mtu asiyestaarabika , ni mangapi kafanya mungu alimrehemu ,Leo huu utajiri mdogo ndo afanye hivi, yaani Kwa jina la yesu atalipa mpaka gari lake la mwisho
 
Huu umafia ni business ya kawaida kwa vitajiri vya kanda ya Ziwa ambavyo vinalindwa na mfumo ccm. Mfano ni yule mabina m/kiti wa ccm alouwawa kipindi kile, wale wale akina Gitana, Zakaria, mabula J4,...watu hatari sana ambao ulinzi wao pekee ni ccm, ndo chaka lao.

Mabula gani mkuu?
 
Tunaona vibaka wakiuliwa kila siku na mpaka kuchomwa moto.

Tunataka tujuwe upande wa pili wa shillingi, kwanini amewapiga risasi?

Hapa si kuangalia upande wa shillingi, NO.. this is an open and close case: 1ST DEGREE MURDER.

Unapopewa lisensi ya kumiliki silaha unasisitizwa kutoua. Unaelekezwa namna ya kujihami na mtu ambaye anakutishia kukutoa roho..Ua tu kama naye karusha risasi.

Nimepata hasira ya ghafla kwa sababu tabia ya Mahende inajulikana. Nimekumbuka tena ile kesi ya pale Lugalo njia panda ya Kawe. Inatia hasira sana.
 
Kama mke na mume wanatumia silaha za moto haya, endelea tu moaka jioni utakuwa umeelimika

Kwani kuwa na silaha si ruksa kulingana na sheria zake na umiliki wake' na matumizi yake pia! ss suala la mtu kuitumia either kwa kujihami au lah inahusu vipi ccm!!? hayo ni matatizo ya mtu binafsi na mnashangaza nyie mnao husisha hata ugomvi wa kuku ku'uhusisha na na siasa mara ccm, kwahiyo mnataka nchi iongozwe na nani ili hata hao kuku wakigombana yawe matatizo yao binafsi na sio siasa!? ' kwanza hii nadharia mmeitoa wapi!?! Tuachane na ligi za kipuuzi
 
Kama pesa.za.quality group dodoma.waliokamata.wameambiwa.ni wezi.na.jeshi.la.police..na huyu.si.anatoka.dk mbili...yangu.macho.nchi inaitaji.fashist.ili tuende.mbeleee
 
Back
Top Bottom