Mmiliki wa mabasi ya J4 apiga wawili kwa risasi

Je kama ni kujihami ? Tulieni mpaka habari kamili yeye siyo mjinga auwe tu! ! Maana ya kua na silaha nikujilinda ,sito vinginevyo

Anaweza kuwa kundi la wajinga pia wauaji, kujilinda sio lazima kuua, kutoa tu silaha tayari umejilinda, kupandisha risasi tayari anayekutishia usalama akili inakaa sawa, risasi hewani bado ni kujilinda, kuelekeza mtutu bado unajilinda, eneo unalopiga sasa hapo tafsiri inaanza kugeuka kutoka kujihami mpaka kuua kwa kukusudia. . . . . .
 
Mmmmh! Hii ni tatizo la serikali tawala


Na si ajabu kesho ukamkuta mtaani huyo Juma Mahende akitamba tu
 
Siku zote mwenye hela ndiyo mwenye haki!

By the way! R.I.P wapendwa wetu!
 
Huyu bwana pia ndiye mmilikiwa wa lile basi lililopata ajali mwaka jana mwezi wa 9 na kuuwa watu zaidi ya 39. Duh ana majanga...

Pole wafiwa...
 
Tunaona vibaka wakiuliwa kila siku na mpaka kuchomwa moto.

Tunataka tujuwe upande wa pili wa shillingi, kwanini amewapiga risasi?

Hata Kama Upande wa Pili Wangekuwa Alshabaab wa Somaliland, Kitendo Hichi ni Unyama , Ukatiri , Uasi na Uadui wa waziwazi Kwa Mwanadamu na Mungu.
 
Watu kama hawa wanastahili kifungo cha maisha kuwa mfano kwa matajiri wengine wanaoona serikali haiwezi kuwafanya kitu kwa rushwa wanazotoa na kuchukua maamuzi kichwani wakiona ni sahihi maana kuna wapumbavu wanasema alikuwa anajihami wakati kutoa silaha ni kujilinda tosha na pia alitakiwa apige juu ili kujiami sio kupiga binadamu wenzake wawili tena kifuani alidhamiria kuua kisa yeye ni Tajiri na anajulikana na serikali
 
Mhhhh! Hata Kikwete hawezi na haitatokea kujiamuria na kupiga mtu risasi, sembuse raia wa kawaida?? Hakuna haja ya upande wa pili wa shilingi, maana huo upande haupo tena duniani.

Hamjamuelewa FaizaFoxy ,nadhani anachotaka kujua upande wa pili wa story ni nini? Jee hao walio pigwa risasi ilikuwaje? Maana yaweza kuwa walimvamia kutaka kumdhuru akaamua kujitetea na kusababisha vifo. Self defence.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom