Mmenuna nini?

kila siku nikiwaona wamenuniana kwenye magari yao ya nguvu naikumbukia hii thread na kuji-smilia tu.... nashindwa ya nini kama maisha yenyewe ndio hayo. heri mie niko kwenye matatu!!!!! halafu naskia kuwapiga picha nije nipost hapa jf!
 
Vipi maisha yanasemaje Nairobi huko?:rolleyes:
 
...duuuh! GP ajabu gani mke kumpangusa shati mumwewe? ...inaonekana mamsapu wako akikugusa tu (hadharani) si msonyo huo utaoutoa :D

si ajabu, lakini kuna kitu kitafuata hapo akimaliza usishangae akasema "honey ule mpango tulioongea juzi vipi kuhusu kunipeleka shopping?".
hapo kidume lazima ujichekeshe-chekeshe!.
wizi mtupu.
 
Vipi maisha yanasemaje Nairobi huko?:rolleyes:

Nairobi bomba kabisa... baridi tu ndio nyingi, lakini twashkuru. waja lini??? nikulaki airport na limo ya nguvu...hatutanuniana...duh kwenye limo????? :)
 
Hii hapa siyo tu kwenye magari ukitaka kulijua hilo zaidi nenda kumtembelea rafiki yako aliyeoa au kuolewa hayo utayakuta.

Pili angalia wanandoa wailotoka out maongezi yao siyo kama ya wale wachumba au wapenzi waliotoka out.

Na nimekuwa nikijiuliza kwa nini inakuwa hivyo au ni kwa sababu ya kuzoeana au ni kwa sababu ya frustartaion za ndoa au inasaababishwa na nini.

Hata wanavyoamua kucheza mfano kama wametoka kwenye kumbi zinazotoa huduma ya mziki hawatacheza kama ambavyo wapenzi au wachumba watakuwa wanayarudi magoma.

Utadhani ndoa zao walilzamishwa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
haya tuambie ya kwako ikoje,maana unasema utafikiri ya kwako inanoga kama zamani,kwenye kuchangia hoja mnajifanya za kwenu nzuri kumbe mzimeshaoza ,hamzungumzi vizuri na wenzi wenu,wakali kuliko pilipili,mko busy kwa sana na mnawasingizia wenza wenu wamewachosha.hebu mseme ukweli naamini wengi wetu huwa tunanuna,haya kila mtu ajikague kwanza!
 
Nairobi bomba kabisa... baridi tu ndio nyingi, lakini twashkuru. waja lini??? nikulaki airport na limo ya nguvu...hatutanuniana...duh kwenye limo????? :)

Nina mwaliko in two months to come,, nitakwambia kabla....i cant miss...si nasikia kwen limo kuna kila kitu so kununiana kutatoka wapi!
 
mhh jamani utafikiri mnanisema mimi,maana nature ya MR ni kununa ,sasa asubuhi kwenye gar huwa najichekesha weeee,mi ananiuzi lakini!ye wapi kanuna tu..ila akiwa na idea yake tu ndio atazungumza nikimuuliza anasema anapiga mahesabu ,uzuri nature yangu ni ucheshi ,kununa ni adui yangu hata kama nimekasirika vp hutajua ,
 
...hivi hata wewe ukiwa unaendesha yeye hununa tu? mnh, ana hila!
 
Watanzania tunaonekana kama tuna uzuni muda wote. Sio kwenye magari tu. Angalia albam ya picha za harusi au sherehe nyingine iliyokusanya watu. Asilimia kubwa ya watu kwenye picha wanatoka wamenuna. Utaona meza imekaliwa na watu kama sita hivi, lakini wote wametoka wamenuna kana kwamba wamelazimishwa kuhudhuria sherehe.

Hii inaweza kuwa moja ya dalili ya nchi yetu kukosa furaha na amani. Kwenye nchi za wenzetu ambapo viongozi wanajali wananchi wake, hili suala lingefanyiwa utafiti na kujaribu kurekebishwa. Lakini kwa sababu viongozi wetu ndio hivyo tena, tumebaki kuwa wakina zumbukuku.

Hebu angali watu walivyonuna kwenye sherehe hii hapo chini. Yaani kila mtu anaonekana amezama kwenye dimbwi refu la mawazo.

babu-swahili-albums-various-picture533-watu4.jpg

babu-swahili-albums-various-picture532-watu3.jpg

babu-swahili-albums-various-picture531-watu2.jpg

babu-swahili-albums-various-picture534-watu5.jpg
Mh, Babu Swahili hilo nalo neno, hasa hapo uliposema hata kwenye masherehe mtu ukiangalia album au video unakuta kweli watu wamenuna utadhani wapo msibani.
Lakini hii si kwa wote, mimi na mwenza wangu tuliamua siku nyingi kwamba raha tutajipa wenyewe, hata kwenye daladala tunapiga story na kuchekeshana.
 
Back
Top Bottom