Mmenuna nini?

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,845
article-0-001EABAC00000258-579_468x286.jpg

...nimeshashuhudia % kubwa ya couples walionuniana kwenye foleni za magari kuelekea makazini (asubuhi) kati ya jumatatu na ijumaa. Kulikoni jamani?

...wengine mnakuwa kwenye magari ya nguvu tu na wengine vioo wamefunga wanakula viyoyozi lakini huwezi kuwaangalia mara mbili jinsi walivyoweka ndita! Inastaajabisha na kuchekesha vile vile,

...kama hamuamini chunguzeni kwenye hizo foleni... :D
 
dah, mkuu uko sawa kabisa
kuna mapozi tofauti tofauti kwenye magari ya watu binafsi

1. wapo walio serious sana: hawa mara nyingi huwa ni mume na mke, tena ndoa yao ni ya muda mrefu, so hawana cha kujadili, kila mtu kakunja ndita, au mmoja anasoma gazeti, au kalala kabisa mwingine anaendesha gari. tena inawezekana walikorofishana jana yake so kila mtu kanuna

2. wapo walio serious kidogo: hawa inaweza ikawa ni wale wenye ndoa za umri mdogo 2-8 years, hawaongei sana mara moja moja lakini wote wanaangalia mbele

3. wanacheka na kufurahi: hawa mara nyingi ni wale aidha wachumba au binti kapewa lifti, so jamaa anachombeza kimtindo. na hata ukaaja wao ni full-mahaba!, yani wamesogeleana kabisa. pia vimada nao wanakuwepo hasa kwenye magari yenye vioo tinted, ogopa hapo unaweza kukuta mkeo au demu wako anapigiwa mdomdogo!
 
dar.jpg

...nimeshashuhudia % kubwa ya couples walionuniana kwenye foleni za magari kuelekea makazini (asubuhi) kati ya jumatatu na ijumaa. Kulikoni jamani?

...wengine mnakuwa kwenye magari ya nguvu tu na wengine vioo wamefunga wanakula viyoyozi lakini huwezi kuwaangalia mara mbili jinsi walivyoweka ndita! Inastaajabisha na kuchekesha vile vile,

...kama hamuamini chunguzeni kwenye hizo foleni... :D

Hii hapa siyo tu kwenye magari ukitaka kulijua hilo zaidi nenda kumtembelea rafiki yako aliyeoa au kuolewa hayo utayakuta.

Pili angalia wanandoa wailotoka out maongezi yao siyo kama ya wale wachumba au wapenzi waliotoka out.

Na nimekuwa nikijiuliza kwa nini inakuwa hivyo au ni kwa sababu ya kuzoeana au ni kwa sababu ya frustartaion za ndoa au inasaababishwa na nini.

Hata wanavyoamua kucheza mfano kama wametoka kwenye kumbi zinazotoa huduma ya mziki hawatacheza kama ambavyo wapenzi au wachumba watakuwa wanayarudi magoma.

Utadhani ndoa zao walilzamishwa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
...nimeshashuhudia % kubwa ya couples walionuniana kwenye foleni za magari kuelekea makazini (asubuhi) kati ya jumatatu na ijumaa. Kulikoni jamani?

...wengine mnakuwa kwenye magari ya nguvu tu na wengine vioo wamefunga wanakula viyoyozi lakini huwezi kuwaangalia mara mbili jinsi walivyoweka ndita! Inastaajabisha na kuchekesha vile vile,

...kama hamuamini chunguzeni kwenye hizo foleni... :D

Aisee mosquito, wewe ni kiboko!!! Hii ni kweli kabisa, yaani mpaka inatisha. Sababu nyingine zaweza kuwa ni:

  1. Wana matatizo ya macho kwa hiyo wanahangaika kuona vizuri, si unajua m'bongo na medical check ni nehi-nehi!???
  2. Baadhi yao wanatafakari misala ya maisha, kazini, homu, serikalini, kwenye TV nk.
  3. Lakini pia inawezekana kabisa midomo inatema mno kwahiyo ni bora kufunga bakuli tu!!
  4. Mbaya zaidi ni kwamba couples nyingi zinaspend too much time to perfectionize matters badala ya kuappreciate achievememnts zao

I wish pangekuwa na kipindi cha tiivii kuonyesha vitu kama hivi
 
Watanzania tunaonekana kama tuna uzuni muda wote. Sio kwenye magari tu. Angalia albam ya picha za harusi au sherehe nyingine iliyokusanya watu. Asilimia kubwa ya watu kwenye picha wanatoka wamenuna. Utaona meza imekaliwa na watu kama sita hivi, lakini wote wametoka wamenuna kana kwamba wamelazimishwa kuhudhuria sherehe.

Hii inaweza kuwa moja ya dalili ya nchi yetu kukosa furaha na amani. Kwenye nchi za wenzetu ambapo viongozi wanajali wananchi wake, hili suala lingefanyiwa utafiti na kujaribu kurekebishwa. Lakini kwa sababu viongozi wetu ndio hivyo tena, tumebaki kuwa wakina zumbukuku.

Hebu angali watu walivyonuna kwenye sherehe hii hapo chini. Yaani kila mtu anaonekana amezama kwenye dimbwi refu la mawazo.

babu-swahili-albums-various-picture533-watu4.jpg

babu-swahili-albums-various-picture532-watu3.jpg

babu-swahili-albums-various-picture531-watu2.jpg

babu-swahili-albums-various-picture534-watu5.jpg
 
...ha ha haaa...

Kumbe na nyie mmeyaona eeh?! hali ndio hiyo... yaani inachekesha kweli!
Ni kiburudisho tosha kwangu nikiwa naendesha kwenye foleni hizo foleni za asubuhi...

Iwapo Couples wapo wenyewe tu kwenye gari halafu wamenuniana namna hiyo, wakiwa nyumbani hali inakuwaje yarabi? Halafu ingekuwa gari moja moja sawa, kila baada ya magari mawili matatu hali ni hiyo hiyo...

Nafikiria kuanzisha kikundi cha matarumbeta barabarani 'kuwameremeta' couples wanaokwenda makazini! :)
 
...ha ha haaa...

Nafikiria kuanzisha kikundi cha matarumbeta barabarani 'kuwameremeta' couples wanaokwenda makazini! :)

Duh...... Kweli JF tamu!!! yaani nimecheka mpaka basi!!! itabidi wale vijana wa kupaza wapewe tenda kila siku asubuhi na jioni

Hii kweli kali
 
Mkuu Kununa muhimu, bei ya mafuta imepanda, mshahara haujapanda, raha itoke wapi...na mabosi wanataka the same level ya output....
 
Watanzania tunaonekana kama tuna uzuni muda wote. Sio kwenye magari tu. Angalia albam ya picha za harusi au sherehe nyingine iliyokusanya watu....

hee?!

...Babu Swahili, ha ha haaaaa... picha zako mwenyewe hizi au? tusijepigwa kabali hapa.

Duh, picha zako ni mfano mwingine tosha 'wanandoa' wakiwa sehemu moja hata kama ni harusini, 'wananuniana!'
 
Lakini mtu huyo huyo akiwa na nyumba ndogo utagundua tabasamu la mbuzi muda wote utagundua kile kifaa ni spare.
 
Mkuu Kununa muhimu, bei ya mafuta imepanda, mshahara haujapanda, raha itoke wapi...na mabosi wanataka the same level ya output....

...hayo yatawezekana wapi iwapo watu mnakwenda kazini mmenuna namna hiyo bana?

Angalau hao walionuna kwenye picha naweza kusema wanauchungu na 'michango' yao wakati vinywaji vinahesabika mezani!
 
hee?!
...Babu Swahili, ha ha haaaaa... picha zako mwenyewe hizi au? tusijepigwa kabali hapa.

Hapana si zangu. Nimezinyofoa sehemu sehemu. Wakati mimi nafunga pingu za maisha, meza na viti havikuwa vinapangwa katika mzunguko. Enzi zangu, viti (hakuna meza) vilikuwa vinapangwa kwenye "rows"....kwa hiyo usiwe na wasiwasi.

Duh, picha zako ni mfano mwingine tosha 'wanandoa' wakiwa sehemu moja hata kama ni harusini, 'wananuniana!'

Yaani we acha tu. Halafu sijui raisi wetu anatoa wapi korodani za kutabasamu tabasamu muda wote....
 
...hayo yatawezekana wapi iwapo watu mnakwenda kazini mmenuna namna hiyo bana?

Angalau hao walionuna kwenye picha naweza kusema wanauchungu na 'michango' yao wakati vinywaji vinahesabika mezani!

ahahhahahah hii imenikausha kabisa.... eti vinywaji vya kuhesabu...walitaka breweries ihamie harusini???

lakini ni kweli its yaani its such a bad view asubuhi kila mtu amenuna..yaani uchumi huwezi kujengeka na watu walionunua hivi. mmm am seconding hiyo idea ya matarumbeta!!!!! ahahahhaha. i will be in charge of the kenyan chapter!!
 
...hayo yatawezekana wapi iwapo watu mnakwenda kazini mmenuna namna hiyo bana?

Angalau hao walionuna kwenye picha naweza kusema wanauchungu na 'michango' yao wakati vinywaji vinahesabika mezani!

haha si ndo katika kufikiria all those scenarios! hakuna raha hapo!
 
ahahhahahah hii imenikausha kabisa.... eti vinywaji vya kuhesabu...walitaka breweries ihamie harusini???

hehehe nimechanga laki mbili naambulia bia 2 wapi na wapi wewe kununa muhimu hapo raha ya sherehe ni mkono uende mdomoni.
 
Jamani leo asubuhi nilikuwa maeneo ya MOrocco na ali mwinyi road; katika gari kumi na nne, ni mbili tu watu walionekana ku-smile, moja wanaongea, na nyingine dada anamfuta jamaa shati

Hebu tuanzishe movement ya kufanya watu wasmile kwenye magari!!!! tufanyeje??? au yale matarumbeta tu yanafaa
 
... vipi tukiwasiliana na Quemu tutafute Billboard moja kuuubwa pale Salender Bridge na ujumbe "mmenuniana nini asubuhi hii?", am sure ita raise few smiles kwa walionuna :)
 
... vipi tukiwasiliana na Quemu tutafute Billboard moja kuuubwa pale Salender Bridge na ujumbe "mmenuniana nini asubuhi hii?", am sure ita raise few smiles kwa walionuna :)
Super idea!!! hebu ngoja tucheki gharama na tuifadhili aisee... ntamcheki jama wa zeki hivi ina maana hawa wenye makampuni ya biashara kama voda wameshindwa kuweka haya ma-idea mwake!!!???
 
Jamani leo asubuhi nilikuwa maeneo ya MOrocco na ali mwinyi road; katika gari kumi na nne, ni mbili tu watu walionekana ku-smile, moja wanaongea, na nyingine dada anamfuta jamaa shati

Hebu tuanzishe movement ya kufanya watu wasmile kwenye magari!!!! tufanyeje??? au yale matarumbeta tu yanafaa

sio mumewe huyo, huyo ni mwizi tu.
 
... vipi tukiwasiliana na Quemu tutafute Billboard moja kuuubwa pale Salender Bridge na ujumbe "mmenuniana nini asubuhi hii?", am sure ita raise few smiles kwa walionuna :)

Very creative. Im sure hata walionuna wataanza kucheka or at least smile
 
Back
Top Bottom