Mme wangu kanizalisha mitoto myeusi

Mme wangu kanizalisha mitoto myeusi

una uhakika hayumo humu jukwaani? Kama akiisoma hii post unadhani atajisikiaje? Wewe ni mmbea mkuu , kama alikumind ww ungemfichia siri tu hata kama ulimtolea nje. Huo ndio utu uzima, othewise utoto haujakutoka.
 
Huyo dada kama kasoma hakuelimika hata kidogo. Biology ya kawaida ya kidato cha nne, angeelewa kuwa mtoto ni tunda kati yake na mumewe. Kama watoto ni weusi basi hata yeye kachangia. Asije akadhani mkorogo unarithishwa! Ni sawa na mwanaume kumlaumu mwanamke kuzaa watoto wote wa kike wakati kisayansi mwenye kuamua jinsi ya watoto ni mwanaume! Mwanamke ana mbegu za aina moja YY. Mwanaume ni XY. Wakati viini vinaungana, mwanaume akitoa Y basi anakuwa mtoto wa kike na akitoa X anakuwa wa kiume.

La pili na kubwa zaidi ni hiyo kasumba ya mtu mweusi kuchukia weusi. Inaonyesha jinsi dada huyo alivyo na fikra potufu na hajithamini hata kidogo. Kuoa wa aina hiyo ni majanga!

Samahani mkuu naona kama umechanganya mambo hapa kuhusu hizi sex chromosome?kwa baiolojia yangu finyu naona ni the other way around kuwa mwanamke ndio mwenye chromosome XX na mwanamme ana XY, na kama yai likipevushwa kwa X basi jinsia ya huyo mtoto itakuwa ya kike na kama ikiwa Y atakuwa wa kiume.
 
Huyo mama kicheche,kwani wakati anaolewa na huyo mwanaume alitegemea atazaa watoto wazungu wakati mumewe mweusi kama giza,stupid her
 
Habari zenu wana JF?

Hiyo ni kauli ambayo nimewahi kuambiwa na dada/mama wa makamo 40's years. Dada huyu tulitokea juana wakati anasoma Postgraduate Diploma chuo kimoja hapa mjini.

Pia shirika letu ni mojawapo ya wateja wakubwa wa bank yao (dada huyu anafanya kazi bank mojawapo kubwa town hapa) nami binafsi ni mteja wa bank hiyo. Basi nilikuwa nikienda ananihudumia kama corporate customer, siku moja akanitolea uvivu nikiwa nimekaa ofisini kwake akanambia tafadhali JICHO TAI nakuomba mtoto mmoja tu niangalie nilivyo mzuri jamani mme wangu amenizalisha mitoto myeusii!

Angalia watoto wako walivyo wazuri jamani, mme wake ni mtu wa kanda za juu kusini na sasa kastaafu. Huyu dada ni mrembo sana kwani kachukua sura ya kichaga miguu ya wasukuma lol, mimi nikamshauri kuwa kwanza haiwezekani na pia watoto ni baraka na zawadi toka kwa Mungu wawe weusi, weupe, wafupi au vyovyote.

Sasa kila akiniona anasisitiza ule mpango vipi. Mimi sitaki kuomba ushauri nifanyeje hapa kwani nilishajua cha kufanya, ila nawaza ni kwa nini mama awaseme watoto wake hivI? akina mama wa JF ulishawahi kuwaza hivi au kusikia mama akiwasema watoto wake kwa namna hii?

jiulize wewe ni wa ngapi kuambiwa hayo?

unazaaje na mke wa tu, tena mumewe kastaafu??

unafikiaje kuongea na mke wa mtu mambo hayo??

and then unakuja public kabisa?
 
Mleta mada umevurungwa na mambo ya katiba...Hakuna mama yoyote duniani anaweza kusema vibaya watoto wake!weka ushahidi hapa.

Wapo aisee...wanawake wengine wapuuzi sana....kuna dada pia alishawai kumwambia rafikiyangu anataka ampatie "third born"...soo depressing
 
Kuchanganya mbegu ya watoto ipo toka kale mbona.
Kama mume au mke mmoja wao ni kilaza, unawezakuta wameambulia watoto wote vilaza.
Hapo ndipo unapohitaji kuchanganya mbegu ya nje. Mama anataka kuchanganya mbegu apate watoto wazuri.MSAIDIE MKUU.
 
Hivi ninavyompenda mwanangu do I see beyond his cute little face?

Do I find any single fault with him?

Afu leo hii bonge la nyau linadiriki kuwaita watoto wake mwenyewe 'mitoto myeusi'!!
 
Nasikiaga hata yule dada mwenye blog ya michambo huwa anamficha mtoto wake eti anasema mbaya
watu wanahangaika hawapati watoto, wao wanaona watoto wabaya, hongera zao.

Mujini kuna mambo! Duuh! Mtutafutage tuwape mbegu bora basi!!! Ila mtoto ni mtoto hata kama hakui..au ana sura mbaya kama Remmy ni mtoto tu!
 
Huyo mama kicheche,kwani wakati anaolewa na huyo mwanaume alitegemea atazaa watoto wazungu wakati mumewe mweusi kama giza,stupid her

Mimi nadhani mleta mada hakuiweka hii mada katika context husika. Hujamtendea haki huyo mdada. Eleza vizuri alichokuambia na ni wakati gani. Wakati mwingine mtu anaweza sema kiutani zaidi.
Haya maneno watu tunayasikia kila mara maofisini.
At 45+ ni nani anayeweza kuchukulia hayo maneno seriously?! Inawezekana alizungumza na wewe kwa tafsida. Ladies ni mahiri kwenye hili. Lakini JT sifa mojawapo ya mwanaume ni kuwa na kifua.
I can imagine ungekuwa ni Hotel Manager ungekuja kusema mangapi. Grow up boy.
 
Huyo mama si mzima yani watoto wake mwenyewe anawesema vibaya?alikuwa wapi kipindi anaamua kuolewa na huyo mume mweusi?
 
Ni ujinga tu na kukosa ufahamu,watu wanalia wana miaka kumi na kitu kwenye ndoa hawana watoto,wanatamani apate

hata mlemavu tu wafute aibu,kwa wenye kukejeli watoto wao malipo ni hapahapa duniani na ndo maana unamkuta mtoto

anakuwa mtu wa kukataliwa kwa kila anakoenda au akikua mkubwa hajali mzazi wake kumbe chanzo ni mzazi mwenyewe

alikuwa na tabia ya kumkataa na kumtusi mtoto.
 
Watu Wanajua Kukufuru Nyie,"eti Mitoto Myeusi".Mi Nahisi Hao Watoto Si Wake.Kama Ni Wake Asinge thubutu Kusema Hivo..Duh!
 
ukizaa nae {ikatokea} akatoka mtoto ana matege ya ubanio {siombei hivyo} atasema "MME WANGU KANIZALISHA MITOTO INA MITEGEEE"..
Maamuzi ni yako mkuu.
 
Back
Top Bottom