Sadly, haya mashindano ya ajali yanaonekana kupamba moto kati ya Hood, Abood na Sumry. Niliwahi kushauri huko nyuma kuwa kama mmliki (kwa maana ya kampuni) inapata ajali mara kwa mara basi ifungiwe mpaka pale serikali itapojiridhisha kuwa kampuni hiyo inafuata kanuni zote za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na ubora wa mabasi yenyewe, uwezo na nidhamu ya madereva wao.
Lakini kwa kuongeza (and very practicle) wamiliki wa mabasi haya matatu: Hood, Abood na Sumry, WAAPIZWE kwa vitabu vya dini zao kwamba iwapo wanatumia/watatumia 'science ya kimazingira' kuendesha na kuleta ufanisi kwenye biashara zao basi mungu awapumzishe. Waapizwe!
RIP na poleni wafiwa na wale wote mliopata ajali pamoja na ndugu,jamaa na marafiki wa wahanga wote.