Wanajamvi!
Nimepewa taarifa kuwa maeneo ya kimara korogwe kuna ajali mbaya sana imetokea leo na kupoteza maisha ya watu. Ajali yenyewe imesababishwa na lori aina ya fuso ilio feli brakes na kugonga toyota landcruiser yalikuwa yakitokea mbezi kuja mjini, na baada ya kuigonga landcruiser VX ikarushwa upande wa pili wa barabara ikakutana na lori jingine ikaligonga na lile lilofeli brakes likaruka upande wa pili nalo likagonga ile lori liligonga VX na kugonga daladala iliotokea mjini kwenda mbezi na kuangukia kwenye kituo cha basi ambacho kilikuwa na watu wakisubiria usafiri, inavyosemekana watu waliokuwamo ndani ya VX wamepoteza maisha hapo hapo na wendine kwenye daladala, waliokuwa kituoni ingawa hadi sasa idadi kamili ya waliopoteza maisha haijajulikana.
Waliopo njia hiyo ama maeneo hayo watujuze maana mtoa habari alienipa amesema mtu akiona hhiyo ajali huwezi rudia mara mbili kuitazama.