Mlokole apewa notisi kwa kukera wapangaji wenzake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlokole apewa notisi kwa kukera wapangaji wenzake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 29, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mkristo anayeabudu katika dhehebu la Makanisa ya Kilokole amelazimika kupewa notisi na mwenye nyumba wake baada ya kuonekana kuwa kero kwa wapangaji wenzake.
  Mwanamke huyo [jina linahifadhiwa] amekutwa na kadhia hiyo, Aprili 25 mwaka huu, huko maeneo ya Uwanja wa Ndege alipokuwa amepanga nyumba hiyo

  Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 28 amedaiwa kuwa kero kwa wapangaji wenzake kwa kusababisha kelele usiku wa manane wakati akiwa katika maombi ya kumuomba Mungu.

  Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo ambaye alipanga chumba kimoja imedaiwa chumba chake kilikuwa kikitumika na waumini wenzake kama kituo cha kufanyia maombezi mara kwa mara na siku za awali walijaribu kumvumilia lakini miezi mitatu baadae baadhi ya wapangaji walishindwa kuvumilia na kuripoti tukio hilo kwa mmiliki wa nyumba hiyo ili aweze kutatua tatizo hilo

  Imedaiwa kuwa mwanamke huyo amefikisha muda wa miezi mitatu na wiki mbili katika nyumba hiyo toka alipie pango lake

  Imedaiwa mwanamke huyo siku za mwishoni mwa juma huwa na kawaida ya kuja na waumini wenzake na kufanya maombi chumbani kwake na kusababisha kelele mithili ya kuwa na msiba jambo ambalo lilikuwa likileta usumbufu kwa baadhi ya majirani wa nyumba hiyo hata na baadhi ya majirani wa nyumba za karibu kwa kuwa mara kwa mara walikuwa wakidhani alikuwa amefiwa na kukimbilia chumbani humo hadi walipozoea kuwa huwa anasali

  Mbali na kusali na waumini wenzake majira ya mchana ama jioni, pia maombi ambayo yalikuwa yakikera watu zaidi ni yale ya usiku wa manane na kusababisha usumbufu kwa watoto na hata watu wazima kwa kuwa husababisha kelele za hali ya juu.

  Kufuatia hali hiyo wapangaji waliitisha vikao na kukubaliana kuwa wafikishe ripoti hiyo kwa mwenye nyumba na hatimaye mmiliki huyo alifika hapo na kumsihi kuwa awe anafanya maombi hayo bila kusababisha usumbufu kwa wenzie

  Kwa kuwa alishazoea hali hiyo ilimuia vigumu kuacha maombi hayo na baadae mmiliki huyo kuchukua uamuzi wa kumpa taarifa ya kumsimamisha mkataba ama aweze kumrudishia kodi yake iliyobaki aweze akapange nyumba nyingine

  Hata hivyo mwanamke huyo hajaafiki hayo na kumtaka radhi mmiliki wa nyumba hiyo na kumwambia alikuwa ameipenda nyumba hiyo hata hivyo mwenye nyumba alimtaka amalizie mkataba ahame
   
 2. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mmmmh...Hii kali kwelikweli..Inanikumbusha ule msemo usemao Starehe zangu zisiwe kero kwa wenzangu ndio yaliyomkuta huyu mamsapu.Akatafute pango kwenye kotaz za makanisa nadhani starehe zake ndipo zitakuwa mahali pake muafaka.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kumbuka fahari wawili hawawezi kukaa zizi moja!mfano mzuri mbeya utakuta uwanja mmoja wa mpira unatumiwa na wahubiri kibao kila mmoja ana kundi lake halafu unakuta wote ni dini moja walokole na mungu wanaemhubiri ni mmpja kaazi kwelikweli!
   
 4. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hapa kuna mambo mawili ambayo mimi binafsi naona yamefanyika!!!

  1. mbona hao majirani mchana wanapiga taarabu zao na hakuna aliyewaambia wapunguze sauti???????????

  2. huyo dada angetakiwa kujua tu kuwa anaishi pamoja na watu wenye imani tofauti!! "Mungu ni roho na waabuduo halisi katika roho ndio watakaomuona"

  imeandikwa Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba, haikumlazimu kuomba kwa sauti saaana, kwa kuwa anakaa na watu.

  Ila namtia moyo, hayo ni majaribu tu!! anatakiwa amkumbushe Mungu ampe nyumba yake mwenyewe ajifungie ndani kwake aombe kwa raha zake.
   
 5. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye rangi nyekundu ninakataa, hakuna cha jaribu wala nini ni kukosa hEKIMA na kutokuwa na KIASI!! kwanza kwanini aombe kwa nguvu, Mungu wake ana msikio mabovu? maombi ya kelele hayanaga faida yoyote Kiroho, maombi ya kimya huwa yanagusa moyo zaidi, mkumbuke yule mama kwenye bibilia alikuwa anaitwa Hana, mke Eli kuhani alikuwa naomba maombi ya uchungu ni midomo tu ilikuwa inacheza na machozi kumtiririka, na Mungu alimpa mtoto akamwita Samwel

  huyo wa maombi mpaka majirani wanadhani kafiwa ATAKUWA NA MAPEPO!!
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Hana busara huyo dada..
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Akikua ataacha. Sii kwamba ataacha kuomba, hapana! Atabadili style ya kuomba.
  Atapewa hekima ya kutambua kuwa kuomba sii kuwataarifu watu kwamba una haja hii ama ile bali ni kuzungumza na Mungu wa sirini katika chumba chako cha sirini nae hukupa haja yako katika usiri huo huo.
  .
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ana busara sana ..... mimi namualika katika nyumba yangu.....achohitajika ni kuikarabati kwa kiwango atakachoweza ili awe huru zaidi....!
  WANAWAKE "WAOMBAO" NI JESHIM KUBWA...ONA ADUI ANVYOHANGAIKA MPAKA WANAFIKIA KULALAMA JF...! BIG UP GOOD LADY ...YOU HAVE YOUR REWARD
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  hana mum asa mzuka ukiamka usiku hana jingine la kumpa faraja lazma apate wazimu mpaka mzuka utulie hahahaaaa!
   
 10. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  unamaanisha hana mume....?:A S 39:
   
 11. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mimi nilikuwa naishi pamoja na Mlokole nyumba moja yaani kulikuwa hakukaliki, yeye ndiyo yeye yaani anamjua mungu na anajua kila kitu cha ulimwengu huu, lakini kumbe mbali na hayo alikuwa mwanachama mzuri sana wa kuvuta bangi, ukimuona kila wakati kavaa miwani ya jua hata kama ni saa sita usiku, nikawa najiuliza huyu jamaa vp? ndipo watu wanaomjua wakanidokezea.
  Kuhusu maombi kwa kweli ni uhuru wa mtu, lakini walokole wamezidi kipimo, ukisoma biblia kwa umakini kuna mstari unasema '' msiombe kwa kupayuka kama wanafiki wafanyavyo madhabahuni...'' lakini walokole wanafanya kinyume kabisa, tatizo sisi waafrika tunapenda sana kwenda na wakati, kila kipya kikijitokeza lazima na sisi tuige, ni ulimbukeni wa kiimani tu!
   
 12. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mimi pia nasema hana busara. yesu mwenyewe alikuwa akisali faragha sio kupayuka.mfano alipokaribia kuteswa kwake alisali faragha hadi akatoka jasho la damu,
  kabla ya kuchagua mitume alisali faragha,pia katuambia ukitaka kusali ingia chumbani mwako jifungie sali kimya mungu atakujazi MAT 6:6.
  hakuna haja ya kupayuka au kujichanganya maneno kibao tena usiku huku ukisumbua watu hiyo sio sala ni sawa na wale mafarisayo wanaokaa njia panda wakisali sala ndefu ili kila mtu ajue wanasali,ole waooooooo wanafiki hawaa.
  Matthew 6:7
  "When you pray, don't babble on and on as people of other religions do. They think their prayers are answered only by repeating their words again and again
  Ecclesiastes 5:2
  Do not be quick with your mouth, do not be hasty in your heart to utter anything before God. God is in heaven and you are on earth, so let your words be few.

  Prayer is a personal conversation between you and God. Jesus said, "…pray to your Father…in secret…" (Matthew 6:6). The Lord Jesus also told us to talk to God from our heart, and not just say the same things over and over.
   
 13. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Poa Mkuu, huyo ni roho wa shetani anapingana na Roho wa Mungu, mbona kelele za vipaza sauti vya misikitini hawavizuii? Alfajiri hao! Muda wote makelele! Je walijaribu kuongea naye wakashindwa kuelewana? Nuru na giza havichangamani.
  Ila huyo dada pia anapaswa kuwa na hekima ili asiwe kwazo kwa watu wengine.
   
 14. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wewe mawazo yako yote yako kwenye ngono tu! Naam hawa ndo type ya wanawake tulionao kama wewe, ndiyo maana kuolewa inakuwa ngumu. Hakika mwanamke waaina yako hafai ktk ndoa.
  Mungu akusamehe maana kwa mawazo yako unafikiri kuna mwanaume mwenye hekima anayependa mwanamke wa hali yako? Wanakuchora tu.
   
Loading...