Mliyodhihaki mabehewa mapya TRC ombeni radhi!

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,944
Ni ustaarabu kuomba radhi pale tunapokosea, lakini pia ni uungwana kuomba radhi pale tunapokosea wenzetu!

Tuliaminishwa humu kwamba mabehewa yanayopokelewa bandarini Dar es Salaam, ni ya zamani na pia siyo kutoka Korea kama tulivyokuwa tumeahidiwa na serikali ya JMT.

Tulikuwa tunataka kuonyeshwa ubovu mwingine wa JPM na wenye malengo yao!

Sasa tumeona "Uhalisia"ni tofauti na "Uzushi".

 
Mleta mada wewe ndio utuombe radhi. Bado huoni tu.

1. Ni kweli hayo ni mabehewa yaliyotumika (old&used), yamepigwa rangi na kuwekwa nakshi (accessories, decorations). Hiyo ni taarifa rasmi ya serikali na mkataba ndivyo ulivyonukuliwa ukitamka.

2. Muonekano wake ni mabewa ya kizamani sana, uliopitwa na wakati. Kuna nchi ukienda utayakuta makumbusho.

3. Muonekano wake ni tofauti kabisa na taswira tuliyohaidiwa hapo awali. Tumeletewa kitu ambacho hatukukiagiza tuletewe!
 
Sasa hayo mabehewa Yana tofauti gani na yale mabasi ya zamani ya UDA!?...au kwa sababu yamepigwa rangi kwa kutumia compressor na kupachikwa viti vya YUTONG ?!...nadiriki kusema hayo mabehewa hayajafikia ata ubora wa zile Steam Trains walizokua wanatumia wakoloni wetu wakati wanatutawala
 
Wajanja sana wameisha piga rangi na kufunga tumifuko tupya tujuwe mupya?

Si zile zile na rangi yake mbaya kama gari za kingi msukuma mwaza to bariadi?

Ila siasa bana, walituonyeshwa ualisia kitakachokuja ili aone reaction, walivyoona kelele, sasa hivi wamezifunga funga tumifuko tupya rangi wamepaka dah
Mbona huleti picha za nje? Tukaziona ni mtumba nyie leteni kwani tumesema hatutazipanda?

Mnapima kina cha maji na njiti ya kiberiti sio? Watanzania hatunaga tabia za kuzila leteni tu. Ila radhi hatuombi, sisi tunajuwa mlichotuhaidi na kilicholetwa.

Ila nyie kama mabasi ya kwa kwini msibani na rangi zile zile.
 
Mkuu Voice, kwanza naunga mkono hoja ni ustaarabu na uugwana mtu kuomba radhi pale unapokosea ama tunapowakosea wenzetu.

Uungwana huu na ustaarabu huu ni kwa wote, hakuna exceptional.

Hoja kuwa mabehewa haya ni mabehewa ya zamani sana, ni mitumba, used, iliyofanyiwa ukarabati kwa kuwekewa vifaa vipya na kufanyiwa nakshi nakshi haina ubishi,

Mzigo utolea Korea sio issue, mitumba hiyo imenunuliwa nchini Ujerumani ikapelekwa kukarabatiwa Korea!.

Tumeelezwa ni mapya na yametengemezwa Korea, na ndani tulionyeshwa yakiwa na dirisha za upande mmoja
ndio maana sio wote tumebeza, wengne tumepongeza ila kuna maswali ya msingi sana tumeuliza Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!
Maswali yenyewe ni haya Tuambiwe tuu ukweli, Watanzania hatuna tatizo kabisa na kutumia mitumba, tumezoea!. Watu Bongo wanavaa nguo za mitumba na wengine hata naniliu za mitumba!, itakuwa mabehewa!. Sisi wengine hatulalamiki bali tunataka transparency tuu!.

P
 
CC. Kigwabgwala,Pasco na wengineo
 
Wenzetu haya nimesikia 2023 wanataka wabadilishe walete mengine na washaanza baadhi ya mabehewa kuyapeleka chuma chakavu sisi ndio tunaagiza na hayapo kwenye kiwango hiki...
 

Attachments

  • Screenshot_20221127-071623_Google.jpg
    200.5 KB · Views: 12
  • Screenshot_20221127-071723_Google.jpg
    214.9 KB · Views: 12
  • Screenshot_20221127-071735_Google.jpg
    220 KB · Views: 12
  • Screenshot_20221127-071631_Google.jpg
    190.5 KB · Views: 11
  • Screenshot_20221127-071638_Google.jpg
    238.9 KB · Views: 12
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…