Mlipuko tena Arusha, jeshi la Polisi watuhumiwa

Mlipuko tena Arusha, jeshi la Polisi watuhumiwa

hii habari ikiwa rasmi kuna watu humu watatia aibu..
 
Polisi kabisa? seriously?
kuna mtu ameweza kuwapiga picha hao wahuni?
na kwanini kanisa katoliki?? ishiiiiiiii....
Itafika mahali tuanze kuingia makanisani na silaha.
yawezekana ni polisi wanakula njama na hao magaidi na hao hao ndio waliowatorosha wale waliolipua mkutano wa chadema
nimemkumbuka Lowassa,anatakiwa arudie uwaziri mkuu wake,angeshikisha watu adabu...
 
Mkuu nitakuwa sikatizi mitaa yenu sasa, manake hii ishu ya kitengo cha rambi rambi inaelekea mnanionea wivu sana.

Mbona Msigwa akila hamsemi?

Umeanza kukiri taratiiiiiibu, usitafute wa kufa nae.
ukatubu hadharani labda mungu atakusamehe.
 
Jamani watanzania wenzangu tujaribu kuukwepa uchochezi wa namna hii maana unaweza kupeleka taifa letu pabaya.sihamini na sitaki kuhamini kma polisi wetu wazalendo wanaweza kufanya kitu nönsense kma hicho!! Ni vizuri tukasubiri taarifa rasmi ambayo itatupa picha kamili ya tukio na mwisho sisi wadau kuanza kuichambua pasipo kuweka ushabiki wa kisiasa,maana hapa tunazungumzia maisha ya watanzania.

Wakati wakisaidiana kutapeli uhai wa David Mwangosi walikuwa wanafanya kitu sense!!!
 
Serikali yetu inaendeshwa kwa kafara ya damu za raia, hapo jk anataka damu imwagike kwa wingi kabla hajamaliza mda wake,.
 
wanao kanusha wakanushe kwa udhibitisho kuhusu ukweli na siyo kupinga na kumlaumu mtoa taarifa
 
[h=3]MLIPUKO TENA ARUSHA, JESHI LA POLISI WATUHUMIWA[/h]

Taarifa ambazo zimetufikia kupitia kituo cha WAPO Radio FM zinaeleza kwamba kuna bomu limelipuliwa kwenye kanisa katoliki la Mtakatifu Karoli, Ruanga huko USA River jijini Arusha, ambapo wanakwaya takriban 6 wamejeruhiwa.


Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo zimetufikia, zinaeleza kwamba watuhumiwa ni jeshi la Polisi, na kwamba walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu - lililojeruhi 6, ambapo 4 kati yao wameruhusiwa baada ya matibabu kwenye hospitali ya Mission na ya Wilaya ya Arumeru.


Majira ya saa sita na nusu, waumini walidai kuona gari la polisi likipita kwa kasi, na lilipowakaribia walistuka mlipuko ukiwarusha pembeni, ambapo walijikuta na majeraha na usoni, mapajani na maeneo mbalimbali ya mwili. Kisha baada ya hapo gari ilisogea mbele na kuanza kurusha mabomu kwa watu wowote iliokutana nao.


Hadi sasa inaelezwa kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika, huku Kamanda Liberatus Sabas akikataa kuzungumzia zaidi suala hilo. Alipotafutwa na WAPO Radio FM, hakueleza kwa kina, lakini akasema kuwa sio suala la kwaya kama ambavyo imeelezwa, bali ni wakinadada wawili na kwamba hawezi kuzungumza zaidi, bali kesho (Ijumaa) atatoa taarifa rasmi na iliyo kamili kwa vyombo vya habari.


Alipoulizwa kuwa kama ni kweli jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika, alisema kuwa atazungumza kesho kuhusiana na tukio hilo. Tukio hili limetokea ikiwa ni siku mbili zimepita tokea kuapishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Ernest Mangu ambaye amechukua nafasi ya IJP Said Mwema aliyestaafu.

Source: Gospel Kitaa.
arusha bana kama sudani kusini vile..
 
Sio magaidi wa kiislamu hao??sijaskia kauli hiyo up to this very moment haters
 
Kabla hamjampa Mbunge zuzu kama lema nafasi haya yalikuwa yanatokea huko??yan nikiunganisha dots naona huyu pimbi ameigharim sana arusha,2015 chama chenu kisimamishe mtu mwenye weledi wa uongoz bora na sio kuleta wahun wahun wasio jitambua,Arusha mji mkubwa huo,hauwez ongozwa na akili ndogo hata siku moja,mbona moshi kwa mzee ndesa na hai kwa mbowe kuko salama tuh??hatuskii machafuko kama hayo,,Arusha achene ujinga msifanye makosa kama hayo 2015,sisemi muichague CCM la hasha,ila nasema chama chenu kisimamishe mgombea anaejitambua,sio hyu mnaemuita Min Kabaang,,,!
 
Ni haki yao kufanya hivyo walitelekezwa wewe mtu anafanya kama kibarua miaka 12 bila kuajiliwa inabidi wafanye vitu kama hivi matukio ndani ya polisi hayataisha sababu ya upungufu wa sheria
Polisi wa jiji la Arusha ni majambazi wa kutupwa,hakuna kitu wanafanya zaidi ya kuwaza namna ya kuingiza pesa kwa namna yoyote ile,ni hatari sana kudeal na police wa jiji la Arusha hasahasa central ni msala wa hatari.
 
Polisi hawawezi kurusha bomu kwa wananchi hata siku moja. Hao ni watu wabaya wamejivika sare za polsi ili kulichafa jeshi la polisi
 
Back
Top Bottom