Mlipuko mkubwa waitikisa Arusha!

Mlipuko mkubwa waitikisa Arusha!

Jamani jk amesharudi dar isije ikawa paka ameshaanza fujo zake?
 
Ingekua unavyotaka wewe mangatara wala kusingekuwa na breaking news!

Twilumba;
Kumbe kwako weye breaking news ni nusu habari? Ukisikia pikipiki imepiga back fire tayari unatuandikia kuwa kuna mlio wa risasi huko karibu na kwenu? Pole zako
 
Poleni sana wahanga

Watu wameenda kuondoa stress halafu wanapigwa mabomu....
 
Asante PK kwa kuendelea kuifanya jf, "be the first to know!".

Endelea kufuatilia tukio hilo, haswa chanzo cha mlipuko na matokeo!.

Usiwajali watakaokulaumu kwa nini umeleta habari nusu, hao wamezoea kula chakula kikiwa kimeishaiva, na kupakuliwa kwenye sahani, wao kazi yao ni kula tuu, sisi ambao ni wapishi, hata chakula kabla hakijaiva, huonja kwanza, hivyo tunakushukuru kwa kutuonjesha, tunakisubiri kiive utupakulie tule!.
Pasco

sijawahi huona chenga ktk comment zako, najilaumu kwa kutokulog kwa mfumo ule mwingine ningekugongea LIKE!
 
Nimemaliza kuongea na mdogo wangu yuko jirani na pale, so far yuko ndani ila kanambia kuwa wanahisi ni wafanyabiashara kuharibiana biashara na kadili ya habari zilizomfikia ni kuwa ni bomu lililotengenezwa kienyeji!! Watu wako wanakula bata tu hata Kwaresma hawaogopi kabisa!!!!
 
Manga, lengo ni jf be the first to know, akiishapata habari kamili, atamalizia!.
Pasco

Pasco;
Sio kwamba sikumwelewa ila kuna b/n nyingine bwana si za kuchelewesha. Alitakiwa atuambie kuwa anaenda kuchunguza atuletee haraka. Ar kumetokea matukio mengi ya kinyama siku za karibuni. Ukisikia Ar tu tumbo moto
 
Nimetoka hapo just now,rafiki yangu alikuwa hapo ndani na gari yake imegongwa kwenye purukushani za kutoka baada ya mlipuko but Thx God nimemkuta salama ila anasema kuna aliyekaa jirani yake anahisi amechanika vidole,polisi wameshaweka ile warning tape na pale kwa ndani nimeona watu wanapima (may ni JWTZ-Mabomu).Ila nimeambiwa hakuna aliyepoteza maisha eneo la tukio,wacha tusubirie taarifa zaidi.
 
Mkuu kama unakaa karibu na haujasikia basi tumshukuru Mungu kama sio ukweli, lakini habari yako ya leo manchester city kucheza na Barcelona inanitia shaka, leo Liverpool ilicheza na Man City na Barcelona ilicheza jana na Granada na kufungwa moja bila..

Mods kama hii habari haina ukweli naomba huu uzi ufutwe tuache kutiana presha za bure

Ni kweli mkuu, nimetoka kuongea na aliyenusurika kwenye hilo tukio maana palikuwa pamejaa sana hadi barabarani na lilipuka ndani ya bar wakati mpira huo kati ya liver na man city unaishia. Majeruhi wamepelekwa mount meru hospital, tusikilizie tu kesho tutajua zaidi.
 
Ni bomu mkuu, watu wengi wameumia na wamekimbizwa Selian Hospital na Mt. Meru Hospital, MUNGU awape kupona majeruhi wote.

TANZANIA LEO NI MAJANGA!
poleni sana mkuu. zidi kutupa up dates zaidi ikiwezekana hadi na picha.
 
Hii bar c ndo inaitwa makalio-- bar, na huwa panajaa sana siku ya mechi hasa leo palifurika maana mwenye bar ni mdau mkubwa wa barcelona, na leo barcelona ilicheza na man city

Labda Man City na Barcelona za Kiding'a ndio zimecheza leo...
 
Hii imekaa vibaya... BOMU?? Na kama kawaida, itakua muujiza kujua alolitupa na kwanini. Mungu tusaidie waja wako. Mkuu wa mkoa amefika hapo pia.
 
Back
Top Bottom