Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Philipo D. Ruzige

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
9,412
26,903
Hello Wadau.

Nipo stage ya kupaua nyumba. Nyumba inadai bati 110, sasa ukigusa huku Alaf na kina Sunshare ni mkasi kweli kweli

Nina option mbili mkononi

1. Nipige bati za kawaida tu
2. Nipige bati za rangi toka kampuni ndogo ndogo

Sasa hapo namba mbili nimeona kuna kampuni inaitwa Bati Bomba Ltd inajinasibu sana kuwa na bati konki master.

Naomba mwenye uzoefu kwa namna moja au nyingine na hiki kiwanda au hivi viwanda vidogo vidogo vya bati anisaidie mawazo na uzoefu wake

Hii bei ya bati itaondoa roho yangu aisee

,
 
Hamna bati mle mkuu!

Bati nyepesi kama karatasi,

Mimi pia nilikuwa na shida na bati ila nimezunguka kwenye hivyo viwanda vidogo vidogo bati zao ni nyepesi sana ndio maana bei yao ni kitonga!

Bati linalouzwa elfu 40 kule alaf eti wao wanauza kwa elfu 25 mpka 23 sasa hapo huoni kama kuna shida.?

Bora uende pale shineshere kidogo wao bati zao zina unafuu.
 
Mimi nina uhitaji wa bati reject kwa ajili ya uzio, mwenye connection tujuzane tafadhali
 
Hivi tunapozungumzia ubora wa bati tunaangalia muda mpaka bati ianze kupata kutu au muda ambao rangi itaanza kupauka?

Maana hizo unazosema za bei ndogo zimepitishwa na TBS,na wanatoa warranty ya miaka 10,sasa kigezo cha kuzipitisha ni nini? ina maana zinakidhi viwango.

Mi naona mambo mengine hapa ni mfuko wa mtu,weka bati kulingana na uwezo wako,kwani wengi wetu nchi nzima tunaweka haya viwanda vidogo na hayo maswala ya kutu au rangi tutadanganyana tu humu...
 
Back
Top Bottom